Naomba kujuzwa namna ya kutuma simu kutoka Dar es Salaam kwenda mkoani

reyzzap, Mwaka 2016 niliwahi kutuma simu kwa njia hii kutoka Dar kwenda Kigoma kwenye Saratoga. Mzigo ulifika salama salimini japo wao saratoga walifaulisha kwenye bus lingine, tulipokuja kuwatafuta kwenye namba zao wakatuelekeza sehemu ya kuupata.

Simu ilikuwa ndani ya kiboksi chake nikaiweka ndani ya bahasha nikafunga bahasha na pini, niliandika juu ya bahasha jina na namba ya mpokeaji ingawa wao pia waliniambia niongeze baadhi ya maneno juu bahasha ili package iwe kamili/rasmi.

Waniliuza nithibitishe humo ndani kuna mzigo wa aina gani, nikawaambia ni simu(smart phone), wakaniuliza na thamani yake nikawaambia, hadi hapo ndio wakanitajia gharama za usafiri ambayo ilikuwa Tsh 20,000/=

Walinikatia risiti ikiwa inaonesha hela niliyolipia, namba ya mzigo(maana waliandika namba juu ya bahasha ambayo inawezesha mpokeaji kwenda kupokea mzigo kwenye ofisi zao akiwa na ile namba, mimi ndio nilitakiwa nimjulishe hizo namba), namba yangu ya simu na namba zao za simu.

Hadi sasa nina imani mambo yatakuwa yashabadilika sana, umakíni unahitajika katika hizi za kutuma mzigo maana utapeli umeshamiri kila sehemu.
 
Mwaka 2016 niliwahi kutuma simu kwa njia hii kutoka Dar kwenda Kigoma kwenye Saratoga. Mzigo ulifika salama salimini japo wao saratoga walifaulisha kwenye bus lingine, tulipokuja kuwatafuta kwenye namba zao wakatuelekeza sehemu ya kuupata.

Simu ilikuwa ndani ya kiboksi chake nikaiweka ndani ya bahasha nikafunga bahasha na pini, niliandika juu ya bahasha jina na namba ya mpokeaji ingawa wao pia waliniambia niongeze baadhi ya maneno juu bahasha ili package iwe kamili/rasmi.

Waniliuza nithibitishe humo ndani kuna mzigo wa aina gani, nikawaambia ni simu(smart phone), wakaniuliza na thamani yake nikawaambia, hadi hapo ndio wakanitajia gharama za usafiri ambayo ilikuwa Tsh 20,000/=

Walinikatia risiti ikiwa inaonesha hela niliyolipia, namba ya mzigo(maana waliandika namba juu ya bahasha ambayo inawezesha mpokeaji kwenda kupokea mzigo kwenye ofisi zao akiwa na ile namba, mimi ndio nilitakiwa nimjulishe hizo namba), namba yangu ya simu na namba zao za simu.

Hadi sasa nina imani mambo yatakuwa yashabadilika sana, umakíni unahitajika katika hizi za kutuma mzigo maana utapeli umeshamiri kila sehemu.
Utapeli upo sana Mkuu.....
Jamaa yng yeye juzi juzi alilizwa pc, ila ni UZEMBE.

Kipnd ambacho nilitamani kufa (hiki kisa niliandikaga humu)

Kuna shule moja kubwa tuu nilijenga uaminifu nayo ikanipa tender ya kwenda kuwanunulia desktops za wanafunzi za kumwagaa Dar then ziende mkoa...
Nikafanya manunuzi vzr, ule mzigo ni mkubwa sana haukuweza kusafirisha kwa basi, ikabd nitafte zile transits za mafuso ya mikoani yanayoleta mazao k.koo ili zirudi nao, basi mzee nikaongea nao nikapakiza mzigo ile jioni maana usiku ndio zinaondoka.

NGOJA NIFUPISHE.

Inafika kwenye saa 10 hivi usiku nawapigia kuwaulizia wapo wapi, naambiwa..

"ndugu mteja huwezi kuunganishwa na namba unayopiga kwa sbb UNAYEMPIGIA HANA SALIO LA KUTOSHA"

Nilichokaaa aisee, nilihisi michirizi ya shoti ikipita pita kila sehem ya mwili, hii kauli sijawahi isikia hata siku moja, ndani ya sekunde kumi nilijiwa na options si chini ya 50,
Nikawapigia tigo kuwauliza tigo hii kauli inamaanisha nini?

Wakaniambia ukisikia hivyo jua unayempigia yupo mpakani au tayar yupo nchi jiarani....

Automatic nilishangaa simu ipo miguuni huku bado ikiwa hewani....

Mwisho wa siku baada ya Ups and down nyingi Niliupata...

Ila ile ndio ikawa mwisho kujirsk kiasi kile,

Hamna kitu kizuri kama kutulia pindi unapopata mshtuko au tatzo la ghafla, na Hapa ndio uwezo wa kupambana na stress unakuja.
 
Wakuu habari zenu, kuna simu nataka nimtumie mtu kutoka Dar kwenda mkoani...naomba kwa mwenye uzoefu wa mtu ambaye amewahi kutuma simu kwa mtu aliyopo mkoani anipe uzoefu kwenye mambo yafuatayo

1. Njia ipi ya haraka na ya usalama ya kutuma huo mzigo
2. Gharama zake huwa zikoje
Tumia basi mkuu wangu
 
Tumia basi tu! Garama itategemea na mkoa unaoenda na magari yanayokwenda mkoa huo! Cha muhimu angalia gari lenye uhakika na ambalo sio wasumbufu! Km itawezekana tumia makampuni makubwa2..mara nyingi sio wababaishaji hata km garama ni kubwa lkn unakua na uhakika

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Utapeli upo sana Mkuu.....
Jamaa yng yeye juzi juzi alilizwa pc, ila ni UZEMBE.

Kipnd ambacho nilitamani kufa (hiki kisa niliandikaga humu)

Kuna shule moja kubwa tuu nilijenga uaminifu nayo ikanipa tender ya kwenda kuwanunulia desktops za wanafunzi za kumwagaa Dar then ziende mkoa...
Nikafanya manunuzi vzr, ule mzigo ni mkubwa sana haukuweza kusafirisha kwa basi, ikabd nitafte zile transits za mafuso ya mikoani yanayoleta mazao k.koo ili zirudi nao, basi mzee nikaongea nao nikapakiza mzigo ile jioni maana usiku ndio zinaondoka.

Ngoja nifupishee..
Inafika kwenye saa 10 hivi usiku nawapigia kuwaulizia wapo wapi, naambiwa..

"ndugu mteja huwezi kuunganishwa na namba unayopiga kwa sbb UNAYEMPIGIA HANA SALIO LA KUTOSHA"

Nilichokaaa aisee, hii kauli sijawahi isikia hata siku moja...
Nikawapigia tigo kuwauliza tigo hii kauli inamaanisha nini?

Wakaniambia ukisikia hivyo jua unayempigia yupo mpakani au tayar yupo nchi jiarani....

Automatic nilishangaa simu ipo miguuni huku bado ikiwa hewani....

Mwisho wa siku baada ya Ups and down nyingi Niliupata...

Ila ile ndio ikawa mwisho kujirsk kiasi kile.
Mzigo kama una thamani kubwa lazima walale nao mbele(watapeli), ila kama ni thamani ndogo, utapeli na uaminifu unagawa percentage.

Ili kupunguza janga hili tutumie watu tunaowajua vizuri(watu wa karibu) katika usafirishaji wa mizigo
 
Mkuu njia ya ems inakuwaje
Unatuma kwa njia ya posta,
Ni rahisi na nafuu
Nmefanikiwa kutumiwa simu dar to simiyu kwa njia ya posta,
Ilichukua siku mbili na uzuri ni kwamba unaitrack online kujua wapi imefikia.
Ikifika unaenda ofisi za posta kuchukua
Nilichajiwa 12,000 tu
 
Katika njia zote, mabasi wanakuwa na uhuni sometime.
LAKINI, EMS, DHL, CITY DELIVERY uhakika Mkuu. Hawa hawana longolongo kabisa Mkuu. kwa wanaokuja Mbeya, Kuna coasta za jioni wanajiita Hakuna kulala, wamejisajili, unatuma jioni asubuhi mzigo uko Mbeya. Ni waaminifu sana. Wanapatikana Kidongo chekundu Mnazi mmoja.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom