Mwaka 2016 niliwahi kutuma simu kwa njia hii kutoka Dar kwenda Kigoma kwenye Saratoga. Mzigo ulifika salama salimini japo wao saratoga walifaulisha kwenye bus lingine, tulipokuja kuwatafuta kwenye namba zao wakatuelekeza sehemu ya kuupata.
Simu ilikuwa ndani ya kiboksi chake nikaiweka ndani ya bahasha nikafunga bahasha na pini, niliandika juu ya bahasha jina na namba ya mpokeaji ingawa wao pia waliniambia niongeze baadhi ya maneno juu bahasha ili package iwe kamili/rasmi.
Waniliuza nithibitishe humo ndani kuna mzigo wa aina gani, nikawaambia ni simu(smart phone), wakaniuliza na thamani yake nikawaambia, hadi hapo ndio wakanitajia gharama za usafiri ambayo ilikuwa Tsh 20,000/=
Walinikatia risiti ikiwa inaonesha hela niliyolipia, namba ya mzigo(maana waliandika namba juu ya bahasha ambayo inawezesha mpokeaji kwenda kupokea mzigo kwenye ofisi zao akiwa na ile namba, mimi ndio nilitakiwa nimjulishe hizo namba), namba yangu ya simu na namba zao za simu.
Hadi sasa nina imani mambo yatakuwa yashabadilika sana, umakíni unahitajika katika hizi za kutuma mzigo maana utapeli umeshamiri kila sehemu.
Utapeli upo sana Mkuu.....
Jamaa yng yeye juzi juzi alilizwa pc, ila ni UZEMBE.
Kipnd ambacho nilitamani kufa (hiki kisa niliandikaga humu)
Kuna shule moja kubwa tuu nilijenga uaminifu nayo ikanipa tender ya kwenda kuwanunulia desktops za wanafunzi za kumwagaa Dar then ziende mkoa...
Nikafanya manunuzi vzr, ule mzigo ni mkubwa sana haukuweza kusafirisha kwa basi, ikabd nitafte zile transits za mafuso ya mikoani yanayoleta mazao k.koo ili zirudi nao, basi mzee nikaongea nao nikapakiza mzigo ile jioni maana usiku ndio zinaondoka.
NGOJA NIFUPISHE.
Inafika kwenye saa 10 hivi usiku nawapigia kuwaulizia wapo wapi, naambiwa..
"ndugu mteja huwezi kuunganishwa na namba unayopiga kwa sbb UNAYEMPIGIA HANA SALIO LA KUTOSHA"
Nilichokaaa aisee, nilihisi michirizi ya shoti ikipita pita kila sehem ya mwili, hii kauli sijawahi isikia hata siku moja, ndani ya sekunde kumi nilijiwa na options si chini ya 50,
Nikawapigia tigo kuwauliza tigo hii kauli inamaanisha nini?
Wakaniambia ukisikia hivyo jua unayempigia yupo mpakani au tayar yupo nchi jiarani....
Automatic nilishangaa simu ipo miguuni huku bado ikiwa hewani....
Mwisho wa siku baada ya Ups and down nyingi Niliupata...
Ila ile ndio ikawa mwisho kujirsk kiasi kile,
Hamna kitu kizuri kama kutulia pindi unapopata mshtuko au tatzo la ghafla, na Hapa ndio uwezo wa kupambana na stress unakuja.