Naomba kujuzwa taratibu/masharti yanayoandikwa Guest House au Lodge

Habari ya jioni wakuu.

Natarajia kufungua guest house soon hivyo kuna vitu vingi kuhusu hii biashara nahitaji kuvijua..

Kwenye lodge nyingi ukiingia huwa unakuta wamebandika kikaratasi chenye kuelezea taratibu zao au marufuku ya vitu ambavyo mteja huruhusiwi kufanya.

Naomba wenye guest wenzangu au wapendwa ambao mnasafiri mara kwa mara na kulazimika kulala lodge mnisaidie kuorodhesha masharti uliyokutana nayo ktk lodge mbalimbali na iwapo upo lodge muda huu hebu piga picha hiyo karatasi hapo ukutani unibless nayo hdpa!🙏

Vile vile ushauri wowote kuhusu uendeshaji wa lodge utapokelewa kwa moyo wa shukrani.

ASANTENI
Usichukue madem wa wateja
 
Masharti kama haya

20240722_194531.jpg
 
Usipende kuwepo ofisini/gues hapo km unafahamika eneo hilo. Nenda kwenye mahabu tuu, hakikisha unaemuweka hapo awe smart kichwan awe msimimizi mzuri
Asante nimekupata mkuu🙏
Ila nisipokuwepo kuibiwa vipi mana uaminifu ni tatizo
 
Tengeneza mfumo mzuri wa kazi kwenda vzr hara usipokuwepo, maana kuna dharura, kuna kusafiri. Ukiwepo wewe kuna wateja utawakosa km marafiki,ndugu na nk aje ili ujue kagegedwa!?
 
🙏🙏
Taona namna ya kufanya mkuu

Asante
 
Lodge na Guest house nyingi Zina masharti ambayo yamewekwa kwaajili ya kulinda Mali za Lodge.

Mfano kwenye kale ka Lodge kangu nimeweka masharti mawili matatu lakini Kwa uchache ni kama yafuatayo;

Usichafue mashuka Kwa Damu ama Kinyeshi.
Lengo la kuweka sharti hili ni kutokana na kuzuka Kwa tabia ya Vijana wa hovyo kupenda kutumia zaidi njia za vumbi katika kutembea kwako, hivyo kuchafua mashuka na wakati mwingine mataulo ya Lodge.
Lakini pia Kuna wadada wengine wanatoa gemu ili hali wapo Kwenye Siku zao za hedhi hali inayopelekea kuchafua mashuka.

Usifungilie TV ama kupiga kelele zitakazofanya wenzio kukosa Usingizi.

Kuna Vijana wengine wakiingia Lodge basi watafungulia TV Kwa sauti kubwa hali inayoweza kupelekea wenzie katika Vyumba vya jirani kushindwa Kulala, ama wakati mwingine hao Vijana wa hovyo huingia na wapenzi wao ambao hupiga kelele usiku mzima wakati wa kupeana hivyo kupelekea wenzao kukosa Usingizi.

Kwa uchache nawasilisha.
 
Shukran mkuu🙏

Nilichojifunza hapa ni kuwa lodge zote zina masharti yanayofanana.

Mbali ya masharti nitashukuru ukinipa abc mbili tatu za hii biashara.
Nifanyaje nipate wateja wengi kuliko wenzangu?😀

Nifanyaje nihakikishe wateja wakifika hawanihami🙏
Asante mkuu
 
Ili kupata wateja wengi hakikisha unazingatia;

Usafi
Lugha nzuri Kwa wateja (Customers care)
Uaminifu
Kujitangaza
Kufanya ukarabati wa mara Kwa mara Kwa kubadirisha vitu ambavyo vinakuwa vimeharibika mfano taa/charging socket n.k
 
Back
Top Bottom