Nani anayeamua kwamba upande fulani ndo umlipe upande mwingine wakati wote wameumizana ma kutiana hasara.
Mahakama ya Kimataifa, International Court of Justice
Ukraine inabidi afungue kesi, ishawahi kufanyika kwa Japan na US na hata Ujerumani ameilipa Israel, vita ya (Gulf war) Iraq na Kuwait ilbidi Iraq alipie kwa mafuta waliyomnyang/anya
Kwa mfano sasa hivi kwenye vita ya Ukraine na Urusi je wanajua kabisa kwamba mwishoni kuna mmoja inatakiwa amlipe mwenzake fidia.
Russia alishaambiwa tangu awali na UN kwenye resolution za Security Council na Ukraine aliambiwa aorodheshe hasara ya vita mpaka itakapoisha
Juzi tu hapa tarehe 16/12, viongozi wa EU walisaini mkataba jijini The Hague kuanzisha rasmi Tume ya Kimataifa ya Madai ya Ukraine (International Claims Commission for Ukraine). Tume hii ndiyo itakayopokea, kutathmini, na kuamua kiasi cha fidia ambacho Urusi inapaswa kulipa kwa uharibifu wa nyumba, shule, na hospitali.
Na je nchi moja ikigoma kumlipa fidia mwenzake hatua gani zinachukuliwa? Kwa mfano sasa hivi Urusi agome, je watafanya nini maana kama ni vikwazo washamuwekea muda tu.
Vikwazo vinaendelea, assets zake zinakuwa frozen ili alipe, akigoma zinataifishwa jumla kulipia fidia kama walivofanya kwa mafuta ya Iraq kumlipa Kuwait na mafuta ya Libya kulipia gharama za kumtoa Ghadafi