Naomba kuongea na wadogo zangu wa kiume 18-30years

Naomba kuongea na wadogo zangu wa kiume 18-30years

1f2d7f5e39edd6ca7909f171fcf9d154.jpg

Tafsiri.!
Usiwe muhanga wa nafsi hasi,ongea kumbuka unajisikiliza....
 
b6aef57fca180e4629442218499b3d05.jpg

Tafsiri.:
Kuwa wewe
Jikubali
Jithamanishe (jipe thamani)
Jisamehe
Jibariki (usijilaani)
Jitambulishe (usijifiche)
Jiamini
Jipende
Jipe mamlaka
 
1ad56368d34e7bcb80e791b72a9e1275.jpg

Tafsiri:
Usitoe muhanga vitu vitatu
Familia yako (ili ufanikiwe jambo fulani)
Moyo wako (ili upended)
Utu wako (ili upate kitu fulani)
 
1f2d7f5e39edd6ca7909f171fcf9d154.jpg

Tafsiri.!
Usiwe muhanga wa nafsi hasi,ongea kumbuka unajisikiliza....

View attachment 487299
Tafsiri :
Usibadilike ili watu wakupende,! Kuwa wewe na watu sahihi watakupenda wewe halisi...!

View attachment 487300
Tafsiri.:
Kuwa wewe
Jikubali
Jithamanishe (jipe thamani)
Jisamehe
Jibariki (usijilaani)
Jitambulishe (usijifiche)
Jiamini
Jipende
Jipe mamlaka

View attachment 487301
Tafsiri:
Usitoe muhanga vitu vitatu
Familia yako (ili ufanikiwe jambo fulani)
Moyo wako (ili upended)
Utu wako (ili upate kitu fulani)

View attachment 487302
Tafsiri:
Acha
-ndoto zako ziwe kubwa kuliko hofu zako
-matendo yako kuliko maneno yako
-imani yako iwe imara kuliko hisia zako
 
Hapa ni kipindi ambapo kijana anaanza kujitambua na angependa ajinasibu na kaliba ya watu tofauti..akipenda aonekane naye ni mtu katika watu (hii huendelea mpaka ukubwani)
Ni kipindi hiki anapoanza kuvutiwa na hisia nyingi za mapenzi na ikitokea akampata mpenzi utaona mabadiliko makubwa sana
Zamani aliweza kutoka vyovyote vile lakini sasa ataoga atajipodoa atachagua nguo nzuri na safi... (mitindo mpya ya nguo nywele viatu na mapambo vinahusika sana hapa )pata picha kama akikosa chochote atajisikiaje!
Mkuu hii ni kweli kabisa. Nayapitia haya
 
Yaani umejibu malalamiko mengi sana ambayo thread zake zilikuwa zikianzishwa na wengi na zilikuwa zikitawala JF. Sawa wameelewa tumeelewa nimeelewa!....nimejifunza kitu.
 
Utu uzima dawa! Mnakopita sasa sisi tulishapita salama, lakini kuna uhitaji wa kukumbushana machache, kupeana mbinu na kutiana moyo pia (hapa kwa sehemu hata wadogo zangu wa kike watahusika). Naongelea mabadiliko ya makuzi kihomoni, kimtazamo, kimahusiano na kifikra pia.

Kwanza lazima niwapongeze kwa uamuzi wenu wa hiari wa kuachana au kutoka kwenye mitandao mingine isiyo na faida wala tija na kuja kujiunga JF(JamiiForums) penye kisima cha maarifa, ujuzi na hata ushauri.

Niwapongeze pia wengi wenu kwa kuwa wawazi kwa yale mnayopitia, wengi wenu hamfahamu kuwa ni sehemu ya makuzi hivyo kujaa hofu na woga mwingi hasa kwenye maeneo haya;

1. Haiba - hapa kila mmoja anajitahidi awezavyo ili aonekane wa kisasa kwa mavazi lugha na hata mikogo mingineyo, kukosa baadhi ya hivyo vitu husababisha maumivu makubwa sana bila kutambua kuwa wakati wako wa kupata bado

2. Ukakamavu/confidence ya kuongea na hadhira au jinsia tofauti, hapa ni kimbembe, wengi hujichukia na kujistukia na hivyo kusababisha kujitenga na jamii muda mwingi kwa kudhani wengine wanajiona bora au ni mahiri kuliko wao! Hiki ni kipindi tu na kitapita lakini siri ya kuongea na hadhira ni kutowaangalia watu machoni bali kuwaangalia juu ya macho yao kwenye paji la uso.

3. Mahusiano kipengele hiki ni muhimu sana na hapa namaanisha kwenye ishu nzima ya kufanya mapenzi. Asikudanganye mtu, mapenzi utayajua baada ya kuvuka miaka 30, hapo utakuwa umewazoea na kuwafahamu wanawake na utakuwa huna hofu tena. wengi sana hapa wanalalamika kukosa nguvu au kumaliza haraka hii yote inaletwa na hofu na mara nyingi kudate mpenzi ambaye tayari keshakutana na wataalam, usitegemee kamwe katika miaka yako 26 umridhishe mwanamke wa 18-23 atakuwa anakuibia tuu.

2f86b25967a46f4e7000116a585bef02.jpg


Mabinti wengi below 25 wapenzi wao ni 35+years. Hapo huwezi weka ligi.
Kinachowatisha wengi ni story za wanawake kufikishwa kileleni au kupiga show 30 nonstop wakati wewe dak5 nyingi. Usihofu, muda wako bado, wewe bado mchanga hujakomaa.

Lakini vile vile kuna wakati maungo yako huhitaji mapumziko. Hii hutokea yenyewe automatically, ndio maana kuna wakati unakuwa na ashiki sana na kuna wakati unakuwa kama hanithi. Usitishike, jitahidi mazoezi, epuka vyakula vya mafuta na makopo, jizuie kadiri uwezavyo kupiga punyeto labda mpaka uzidiwe sana.

7a426246fd98a6d03e3c266e7e110d6a.jpg


4. Uko kwenye kipindi cha kuingia ukubwani, kwahiyo akili ya kiutu uzima inafunguka, hii hali huja na side effects kama za mama mjamzito. Hasira za ghafla, kukata tamaa, kulia au kutamani kulia, kuzira, kujitenga, kuwa mtu wa mawazo muda mwingi ni vitu visivyoepukika.

Hapa ndipo unapojishape kuwa wewe wa kesho, kwahiyo jitahidi sana yanapokutokea haya usiyaendekeze, vijana wengi huwin na kushindwa hapa. Ukiyapuuza na kusonga mbele mafanikio yako yataanzia hapo, utayachukulia kuwa ndio sehemu ya maisha yako, kushindwa kwako kutaanzia hapo.

Kama bado uko below 30 usiangalie mwili ulionao bali jipange kwa kuwa hii ndio hatua muhimu ya kuwa wewe wa kesho. Mustakabali wako umeubeba mwenyewe.

decdd0ee21928acc5bbf4b8eefe0b405.gif
Asante kwa ushauri mzuri. Ubarikiwe
 
Back
Top Bottom