Naomba kuongea na wadogo zangu wa kiume 18-30years

Naomba kuongea na wadogo zangu wa kiume 18-30years

Utu uzima dawa! Mnakopita sasa sisi tulishapita salama, lakini kuna uhitaji wa kukumbushana machache, kupeana mbinu na kutiana moyo pia (hapa kwa sehemu hata wadogo zangu wa kike watahusika). Naongelea mabadiliko ya makuzi kihomoni, kimtazamo, kimahusiano na kifikra pia.

Kwanza lazima niwapongeze kwa uamuzi wenu wa hiari wa kuachana au kutoka kwenye mitandao mingine isiyo na faida wala tija na kuja kujiunga JF(JamiiForums) penye kisima cha maarifa, ujuzi na hata ushauri.

Niwapongeze pia wengi wenu kwa kuwa wawazi kwa yale mnayopitia, wengi wenu hamfahamu kuwa ni sehemu ya makuzi hivyo kujaa hofu na woga mwingi hasa kwenye maeneo haya;

1. Haiba - hapa kila mmoja anajitahidi awezavyo ili aonekane wa kisasa kwa mavazi lugha na hata mikogo mingineyo, kukosa baadhi ya hivyo vitu husababisha maumivu makubwa sana bila kutambua kuwa wakati wako wa kupata bado

2. Ukakamavu/confidence ya kuongea na hadhira au jinsia tofauti, hapa ni kimbembe, wengi hujichukia na kujistukia na hivyo kusababisha kujitenga na jamii muda mwingi kwa kudhani wengine wanajiona bora au ni mahiri kuliko wao! Hiki ni kipindi tu na kitapita lakini siri ya kuongea na hadhira ni kutowaangalia watu machoni bali kuwaangalia juu ya macho yao kwenye paji la uso.

3. Mahusiano kipengele hiki ni muhimu sana na hapa namaanisha kwenye ishu nzima ya kufanya mapenzi. Asikudanganye mtu, mapenzi utayajua baada ya kuvuka miaka 30, hapo utakuwa umewazoea na kuwafahamu wanawake na utakuwa huna hofu tena. wengi sana hapa wanalalamika kukosa nguvu au kumaliza haraka hii yote inaletwa na hofu na mara nyingi kudate mpenzi ambaye tayari keshakutana na wataalam, usitegemee kamwe katika miaka yako 26 umridhishe mwanamke wa 18-23 atakuwa anakuibia tuu.

2f86b25967a46f4e7000116a585bef02.jpg


Mabinti wengi below 25 wapenzi wao ni 35+years. Hapo huwezi weka ligi.
Kinachowatisha wengi ni story za wanawake kufikishwa kileleni au kupiga show 30 nonstop wakati wewe dak5 nyingi. Usihofu, muda wako bado, wewe bado mchanga hujakomaa.

Lakini vile vile kuna wakati maungo yako huhitaji mapumziko. Hii hutokea yenyewe automatically, ndio maana kuna wakati unakuwa na ashiki sana na kuna wakati unakuwa kama hanithi. Usitishike, jitahidi mazoezi, epuka vyakula vya mafuta na makopo, jizuie kadiri uwezavyo kupiga punyeto labda mpaka uzidiwe sana.

7a426246fd98a6d03e3c266e7e110d6a.jpg


4. Uko kwenye kipindi cha kuingia ukubwani, kwahiyo akili ya kiutu uzima inafunguka, hii hali huja na side effects kama za mama mjamzito. Hasira za ghafla, kukata tamaa, kulia au kutamani kulia, kuzira, kujitenga, kuwa mtu wa mawazo muda mwingi ni vitu visivyoepukika.

Hapa ndipo unapojishape kuwa wewe wa kesho, kwahiyo jitahidi sana yanapokutokea haya usiyaendekeze, vijana wengi huwin na kushindwa hapa. Ukiyapuuza na kusonga mbele mafanikio yako yataanzia hapo, utayachukulia kuwa ndio sehemu ya maisha yako, kushindwa kwako kutaanzia hapo.

Kama bado uko below 30 usiangalie mwili ulionao bali jipange kwa kuwa hii ndio hatua muhimu ya kuwa wewe wa kesho. Mustakabali wako umeubeba mwenyewe.

decdd0ee21928acc5bbf4b8eefe0b405.gif
Ushauri mzuri sana na hii ni reality

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu asante kwa madini mazuri.. Natamani ungetoa somo la aina kama hii kwa mara nyingine, inasaidia ku lift our spirits na kujiona tunayopitia ni sehemu ya kawaida ktk maisha na inatufanya tusi panick
[emoji123][emoji120][emoji106]

Jr[emoji769]

silent_ocean
 
Mkuu asante kwa madini mazuri.. Natamani ungetoa somo la aina kama hii kwa mara nyingine, inasaidia ku lift our spirits na kujiona tunayopitia ni sehemu ya kawaida ktk maisha na inatufanya tusi panick

silent_ocean
Tuombe heri nitafanya hivyo tukijaaliwa[emoji120][emoji120][emoji120]

Jr[emoji769]
 
Vijana wengi tunasahau kua kujenga ni kazi ila kubomoa ni rahisi.

Hivi fikiria fikta, mtazamo na maadili uliyojengewa na wazazi wako Pamoja na juhudi zako binafsi kwa 25yrs yana kuja kuporomoshwa na bwege mmoja mliokutana naye ndani ya wiki mbili tu.

Jamaa anakushauri kwa kutishia ‘ Mwanaume gani hata ganja huvuti?’ anakuambia wanaume hatupo hivyo! Na ww unaona jamaa atakudharau unaanza ganja na unga within short time umekwisha.[emoji12]
 
Big up
Mna sehemu yenu muhimu hapa mabinti wengi ndoto zao zimekatishwa katika umri wa 18-25 na hii yote inatokana na kuingia kwenye usichana bila maandalizi
Kuiga na kutaka makubwa bila uwezo kumewaharibia wengi
Vifo
Mimba za utotoni
Kuharibika vizazi
Wizi na matumizi ya madawa na vilevi (kwa jinsia zote mbili)
Broken hearts in the first love experience (ina impact mbaya sana hii)
Na kwa bahati mbaya sana hakuna vipindi vya kufundisha haya mambo mashuleni wala walimu wa saikolojia, sana sana utafundishwa kutumia kondomu na kujikinga na mimba
Vipindi vya kidini navyo ni vya kukariri huku vikiepuka kabisa kuongelea mambo haya kwa uwazi
Wazazi na walezi wako busy na maisha na changamoto zake hawana muda wa kujadili haya...hao wenye muda huko vijijini ni kufundishwa unyago jinsi ya kumridhisha mwanaume na kukata viuno
Mwisho wa siku wengi hujikuta mwalimu wao ni dunia tena baada ya kuingizwa chaka
 
Back
Top Bottom