Naomba kuuliza kuhusu chimbo zuri la kununua mitumba balo za mitumba

Naomba kuuliza kuhusu chimbo zuri la kununua mitumba balo za mitumba

Ma balo gani mazuri ambayo nikinunua siwezi kujutia?
 
Napendekeza kununua Sana yanayotoka Korea japo makampuni ya upakiaji pia yanatofautiana. Unataka kuchukua la kilo ngapi?. Kuna 70 kg, 45, 30, 100 n. K

Kwahiyo hizi belo za korea zinapatikana huko huko mnazi mmoja ulipoelekeza au zenyewe zina supplier tofauti na mahali tajwaa apo juu?
 
Kwahiyo hizi belo za korea zinapatikana huko huko mnazi mmoja ulipoelekeza au zenyewe zina supplier tofauti na mahali tajwaa apo juu?
Hukohuko mnazi mmoja mkuu. Ningesaidia walau kuwaubganisha na watu wanaoyajua maduka Lakin italeta shida. Nitakuwa nadalalia.
 
Habari za muda huu wanajua ii. Gt na professionals wa mambo mbalimbali. Poleni Kwa kadhia, hasa wale wanaosumbuliwa na mapenzi, ajira na siasa. Niseme tu tuendelee kupambana, hamko peke yenu.

Nimeona Kuna uhitaji mkubwa wa watu kufahamu biashara ya mitumba kwani wengi wetu wamekuwa wanaulizia Mara Kwa mara na wengine kutoa baadhi ya wanachokijua kujibu maswali Kwa wasiojua. Nianze kwa kusema kwamba hili la majibu mafupi na uhitaji wa Kujua limenisukuma niandike haya.

Mitumba si biashara rahisi kama tunavyofikiria. Ina utaalamu mchache ambao ni Basic. Utaalamu huu ndio unanisukuma kuandika machache.

Kwanza kabisa, wauza mitumba wapo wa Aina nyingi. Kuna suppliers, ambao wananunua robota 20,10 au 50 Kwa wahindi na kuweka mzigo stoo na kuuza kwa WAFUNGUAJI. Kwa namna hiyo, mnyororo wa Belo unaweza kupita mikono zaid ya mitatu mpaka Belo kumfikia anaefungua Belo kuuza nguo Kwa wavaaji/wuazaji.

Mfunguaji (mfungua Belo) ni mfanya biashara ambae anaweza kuwa na mtaji Kati ya laki 5 (Belo 1/2 kutegemew na uzito au bei Husika) ambae anamiliki kizimba (sokoni n. K) anetegemea Sana kuuza nguo moja moja Kwa wateja wa Aina 3. Napendekeza ukiwa na mpango wa kufungua Belo wateja hawa uwe nao. Hapa nitazungumzia Mtumba grade 1.

1. Mteja wa JUMLA
Ni lazima ukubali kwamba, nguo za mitumba zinaweza kutoka Belo moja lakini ubora ukatofautiana. Kuna nguo unaweza kuuza Kwa elfu 10 (tisheti hii bei ni kubwa mno), Kwa jinzi (ukauza mpaka elf 30). Lakini Belo hilohilo litakupa nguo ambayo hata elfu 1 Mia tano huuzi. Hivyo kadri unavyouza lazima uwe na utambuzi wa bei halisi ya nguo iliyo mkononi. Usikatae kuuza elfu 10 ukaione nzur Sana ukaja kuiuza elfu 7 upate hela ya kula kwanza.Au kinyume chake, ukauza nguo elf 10 kumbe hata elfu 25 ungeuza.

MTEJA WA JUMLA NI YULE ANAEKUJA KWAKO KUNUNUA NGUO ZOTE ZILIZOBAKI MKONONI/KIZIMBANI MWAKO,ILI AKAZIUZE (HAWA MARA NYINGI WANA MWAGA CHINI AIDHA KANDO YA BARABARA AU MINADANI) . Mara nyingi Kwa tisheti wananunua bei ya jumla Kati ya 700 mpaka 1300 inategemea na mapatano.

2. MAWINGA (MAPOINTA)
Hawa pia ni wateja muhimu Sana unapofungua Belo. Ni viungo muhimu Sana kuchagua NGUO KALI kutoka kwenye Belo lako wakauze. Hawa huwa na tabia ya kuchagua Sana, kwenye nguo 300 katika Belo lako ni kawaida kupata nguo 3, 4 au 10 usiawchoke. Wanakuaga na "strong negotiation skills". Wasumbufu. Ila ni muhimu kwani wanasaidia Sana kukutoa kwenye msongo wa kutokuuza, mzigo mbaya au wanakubusti kurudisha mtaji kwani wanaoweza kusababisha ukarudisha nusu ya hela yako mapema mno. Kwa tisheti wengi wapo Nje ya jengo la CHINA PLAZA. Wanakuaga na MAGOLI yao. Kwa tisheti huwa wananunuaga Kati ya elf 5 mpaka 8.

PIA, MAPOINTA, wengine wanaitwaga MAWINGA hawa ni watu ambao hawanunui nguo kwako. Hawa wanaleta mteja kizimbani kwako na kuuza kama za kwao. Ni wazuri pia kuropoka bei. Tisheti ya elf 5 wanaoweza kumropokea mteja kuwa bei ni 12. Ni moja Kati ya watu wanaoharibu biashara za mitumba sokoni zinaonekana ghali. Karume na ilala wamejaa Sana hawa. Ni wa muhimu ila hutakiw kuwaamin, wanaoweza kukudhulumu au kuiba. Lakini pia, ikitokea unawaamini unaweza kuwapa nguo wakauze wakulete hela. Kuwajua pia kunahitajika apa. Wanakuaga na uwezo wa kuuza idadi nyingi ya nguo kuliko mwenye Mali yako. Very potential.

3. WAVAAJI
Hawa ni watu kam mimi na wewe. Ambao wanapita au wanvutiwa Kuja kununua. Hawa wanaoweza kuuziwa na wewe au mawinga. Mara nyingi huwa hatuwajali Sana sabab WANAPITA TU. tunaweza kubambika nguo zilizotoboka wasipoona. Ni biashara, ni rizki. Lakini pia wakijenga uaminifu na kurudi rudi huwa tunawachagulia saizi nzur/dizaini wanazopenda tunawtunzia au kuwapigia simu waje kuziona/ kununua.

Aina nyingine ya wauza mitumba ni hawa MAWINGA /MTUKATI /MAPOINTA. hawa Mara nyingi huwa wanachagua nguo chache NZURI TU. Wanakuaga na teknik za kuchagua nguo nzur Kwa JICHO LA MTEJA. hawa ndio ambao tunawakuta wamebeba nguo mkononi kando kando ya barabara au kukuleta majumbani wengine wanaposti mitandaoni (what's ap status, insta nk). Tabia yao kubwa ni kununua nguo nzur tu (Kam nlivyoeleza). Hawana mitaji mikubwa hawa hata elf 50 inawatoshaga. Pia muda mwingine wanalindwaga na uaminifu tu, wanapewa wakauze walete hela.

Aina ya mwisho ya wauza mitumba ni WAUZA JUMLA. Hawa jamaa huwa na kelele kweli kweli. Kokte wakikaaga hawa lazima kuwepo na kelele za kutangaza biashara yao. Hawa wanatumia hesabu za paukwa pakawa. Mfn. Wananunua tisheti bei ya jumla (nimewaeleza juu hapo Kam wanunuzi wa jumla) Kwa kiasi cha shilingi 800 au 900 Kwa tishet 1 kwa mana tishet 350 *900 (bei) = na Laki 4 mfano. Wanazobeba kwenda kuzimwaga chini na kunadisha elfu tatu 1 (ndani ya siku 2). Mfano umeuza tisheti 80 *3000= na Laki 3 na 20. Siku ya tatu unaanza kunadisha Kwa elfu mbili mbili na kuuza tisheti (260 zilizobaki). Unauza elf mbili-mbili tishet 100 (ndani ya siku 2) Sawa na laki tatu. Siku inayofata unaanza kuuza bukubuku. Tu nategemea kupata faida nyingi Kwa kadri tunavyoshusha bei kila siku Kwa sabb ya kulindwa na yile bei iliyoanza kutumika Mara ya kwanza kabisa. Ukisharudisha mtaji zinazobaki hata Mia tano-tano unauza tu.

NB: HAKUNA UWEZEKANO WA KUUZA TISHETI ZOTE.

HAWA WOTE WANAWEZA KUWA WAUZAJI WA JUMLA KULINGANA NA MASLAHI YAO. SAMAHININI KWA MUANDIKO MBOVU WENYE UHITAJI KARIBUNI HAPAHAPA JUKWAANI KWA KUTAKA UELEWA ZAIDI
Safi mkuu asante sana, hila mitumba ni biashara nzuri sana hasa ikifanyika minadani au sehemu yenye watu wengi.

Sent from my SM-A207F using JamiiForums mobile app
 
Anhaa robota Mara nyingi zinagawanywa Kwa gredi. Kuna gredi A (1), B (2). Hizi zinatofautiana bei kwani gredi B huwa na nguo zlizochoka sana/Chanika kabisa NYINGI. hata bei huwa chini. Pia, hizi robota zinatofautiana nchi I. E Korea, China, Canada, Turkey. Mara nyingi ncchi hizi huathiri Sana Uonekanaji wa nguo (Fasheni, ukubwa au kuchoka).

Zinazotoka kanada Mara nyingi huwa saiz kubwa mnooo. Hapa tunawauzia vibonge /vipande Kam Msechu. Uturuki zinakosaga fasheni nzuri, ila waarabu wale wanapuliziaga udi sijui. Nguo zao hazitoi haruf y mtumba uliyoizoea (Karaha). Nguo za Korea na China ni nzur mno kwenye fasheni za kisasa. Nchi mbili hizi zinatoaga brand saw na tunazoziona madukani Kam starwar, Balenciaga n. K lakini pia Korea inajitahd kutoa nguo chache zlizochoka kufananisha na China.

SUALA LA UBORA WA NGUO NI RISKI. HUWA TUNATUMIA KUZIVUTA ZICHUNGULIE NJE THEN TUNAZIKAGUA MN'GAO. ZINAZOONYESHA KUN'GAA SANA TUNABEBA ROBOTA HILO. KWA KAWAIDA KILA ROBOTA HUWA LINAPEWA STICKER( NDANI YA NAILONI LAKE) KARIRI HIYO STIKA ITUMIE KAMA RIFAA, ZIKITOKA NGUO MBAYA HIZO STICKER ZIEPUKE UKIWA UNACHAGUA BARO. HII IMEKAA KIENYEJI ZAIDI
Mjomba uko vizuri
 
Hukohuko mnazi mmoja mkuu. Ningesaidia walau kuwaubganisha na watu wanaoyajua maduka Lakin italeta shida. Nitakuwa nadalalia.

Nimekuelewa mkuu ila naomba kujua ata majina ya maduka na mitaa yake maana mnazi mmoja ni kubwa sana mwishoe niishie kuzunguka na kurudi mtupu
 
kuna miaka flani hapo Ilala nilikua nachukua mzigo wa robota za tshet,blauz na boksa za kiume chata ya Canam kwa jamaa mmoja hivi anaitwa Ally a.k.a tolu nyoka.
 
Back
Top Bottom