Naomba kuuliza kuhusu chimbo zuri la kununua mitumba balo za mitumba

Nenda Karume kwa wanaouza viatu vya mtumba ulizia Mustafa atakupa connection
 
Nenda Karume kwa wanaouza viatu vya mtumba ulizia Mustafa atakupa connection
Sorry mkuu huyu jamaa Mustafa naskia ni tapeli hauupo hapo inabidi ufike Karume uulizie kimya kimya
 
Mbona nilisikia biashara ya mitumba ilipigwa marufuku Tanzania? ukweli ni upi
 
Nenda mnazi mmoja, mtaa wa Narung'ombe. Ila hakikisha unajua ujanja ujanja wa biashara hiyo la sivyo utakula mzinga
 
Mkuu ninaweza kupata kupata mawasiliano yako?
 
Maduka yapo mengi nitumie namba yako inbobo nikuunganishe nao. Ukifika kagua duka moja baada ya jingine kwanza ujiridhishe then Ndio uchukue maamuz.
 
Watu wasikuzungushe ndugu, nenda mnazi mmoja upande wa ciy center kwenye maduka ya wa Lebanon wengine wanawaitaga wapalestina. Mtaa wa indiragandi huku juu au nkurumah juu na maeneo yanayozunguka hapo au nenda kisutu mkabala na shule ya msingi. Pia unaweza kwenda vingunguti pembeni ya kiwanda Cha Ok Plast na hata keko ilipokuaga coca cola ya zamani. Huko kote wanauza mitumba ya kila aina. Una swali lingine?
 
Viatu vya mtumba vizuri wengi wanafata Nairobi hapo naona viatu vinavyofunguliwa kule ni daraja tofauti na vya daslm kuanzia vya kike na vya kiume vingine vinauzwa sana hapo soko la Moshi na watu wa Arusha harafu bei yao sio kubwa kivile..
 
Hilo bello la viatu vya mtumba ambavyo n grade nzuri.linaweza fika tsh ngapi? Na quantity zinakuwa ngapi ndani..
 
Viatu vya mtumba vizuri wengi wanafata Nairobi hapo naona viatu vinavyofunguliwa kule ni daraja tofauti na vya daslm kuanzia vya kike na vya kiume vingine vinauzwa sana hapo soko la Moshi na watu wa Arusha harafu bei yao sio kubwa kivile..

Halafu nilikua najiuliza memorial mbona wana mtumba classy kuanzia mashuka, makapet ya ndani, viatu nikiwauliza najibiwa wanachukua Dar wakati Dar sijawahi ona class ya vitu vile kumbe siri ni Nai City?
 
Vinapitia Tarakea au Holili huko na ukiangalia vile vitu ni mtumba ila vina ubora sana wahuni huwa hawapendi kutoa siri za kazi...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…