Naomba kuwaaga rasmi Wana JF, nikipona tutakuwa pamoja tena

Naomba kuwaaga rasmi Wana JF, nikipona tutakuwa pamoja tena

1624487142091.png
 
Joseph na Julius
kuna wengine wawiali ambao sikumbuki majina yao zaidi ya hao uliowataja. Mmoja alisema ukweli kuwa alikuwa diagnosed na kansa, na akapita makaburini pale kinondoni kuangalia sehemu atakapozikwa; huyu alikuwa mkweli na wala maneno yake hayakuwa yamepinda. Yule mwingine alikuwa anatoa lawama sana na kutishia kujiua kumbe kweli akajiua kweli kweli; hakueleweka kwa watu wengie mpaka baada ya kuwa amejiua.
 
Pole mkuu mungu akufanyie wepesi upone haraka
 
Mkuu umesema ukipona tutakuwa pamoja. Lakini hata usipopona tutakuwa pamoja baadaye. Kuwa pamoja haliepukiki. Kumbuka sisi ni wa Baba mmoja!

Tunakuombea upone, na utupe mrejesho.
 
Unaondoka kwa maumivu ya Ugonjwa au maumivu ya Ukosefu wa Katiba Mpya Tanzania?
Anaondoka kwasabbb ya maumivu ya ukosefu wa katiba mpya mbona kaeleza kwa kirefu tu. Na kasema hata comments hatazijibu.
 
Remember you can’t convince everyone.

Binadamu wanatofautiana uwezo wa kufikiri, priority za maisha yao, attitudes, affiliations zao, imani zao, mitazamo yao, opportunities they see in life na mambo mengine luluki ndio maana kukawa na watu wenye maisha tofauti.

Unaposimamia kitu remember you can’t can’t convince everyone, but aim at the group who will understand you.

Tesla’s electricity innovation did not win the battle with Edison’s invention. Though he died a poor man but now the world uses his electricity innovation.

Kubali you can’t win everyone that’s life, but if you are right you are right; sometimes it just takes time the world to understand you.
 
Mungu alie juu ya kila kitu akujalie wepesi wa ugumu unao kukabili ndugu mleta mada.

Swala la katiba na uongozi lina mapana na marefu yake.

Wao viongozi wameonelea swala la katiba ni hisani yao kwa wananchi hivyo wana Uhuru was kuitoa ama la.

Lakini pia hio katiba hata ingelikuja leo au Jana au kesho bado haitakuwa ni dawa ya changamoto zinazohitajika taifa hili.

Imekuwa ni rahisi kiongozi kuvunja katiba lakini kidogo dhamiri itamsuta iwapo atavinja moja ya sheria iliopo kwenye kitabu anachokimini cha kiroho.

Hii maana yake Ni vile wengi wetu tulivyojengwa tokea utoto kwenye dini zetu zikakaa kwenye dhamiri hivyo ni Mara chache sana mtu huvunja kwa makusudi sheria ya dini, nanhusumbuliwa Sana na dhamiri kiasi Cha kutotamani kuruda tena.

Linapokuja swala la sheria za nchi hajiulizi mara mbili kwa haina msingi kwenye dhamiri, hivyo hata zije katiba mpya Mara ngapi bado zitavunjwa tu.

Wakati tukiendelea kujanga palipoharibiwa Jana lakini pia tukumbuke kujenga na kesho ili kesho kazi isiwe kubwa.

Tuwafundishe watoto wetu toka wakiwa wadogo juu ya katiba Kama tufanyavyo kwenye dini.


Lakini yote ya yote ndugu mleta mada nakutakia heri zote njema, Mungu yupo na ndie mwenye ujuzi mwingi kuliko alie yoyote, anaijua Jana Leo na kesho, Tumaini langu kesho itakuwa njema kwako. Pole mno jipe moyo mkuu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Niwashukuruni sana na niwaombe msisite kuendelee kumkumbusha kuhusu maumivu yangu juu ya Tanzania mpya. Endapo lolote litatokea may be ntarudi ila nimefika ukomo. Mwenyenzi Mungu mtoa maarifa na njia akawajaze ufunuo na maono ya mwisho mwema Kama Mimi. Mkaondoke mkiwa kwenye toba na siyo mkiwa dhambini.

Naitwa Beatrice Kamugisha (nick name), naandika kutoka Regency Dar es salaam Tanzania.

[emoji3064][emoji3064][emoji3064][emoji3064][emoji3064][emoji3064][emoji3064][emoji3064][emoji3064]Nahisi siku yangu kuingiwa na simanzi[emoji2815][emoji2815][emoji848][emoji848][emoji848][emoji848][emoji2827][emoji2827][emoji2827][emoji2827][emoji2827][emoji2827][emoji2827][emoji2827][emoji2827][emoji2827][emoji2827][emoji2827]
 
Pole, inaonyesha umekata tamaa ya kuishi. Ikatae hiyo roho ya mauti na kumbuka haya mambo ya dunia hii hakuna ataepita akaweka kila kitu sawa maana binadamu hatufanani mawazo.
 
Back
Top Bottom