Hakuna dini iliyo bora kuliko dini nyingine. Hakuna dini itakayoingia mbinguni.
Mbinguni hakutakuwa na swali la "ulikuwa ukiabudu dini gani" wanaoabudu katika roho na kweli tu ndio watakao ingia. Wasiofungwa na misingi ya kidini bali ya Roho mtakatifu.
Kama ukimwona mtu anagalagala anakaribia kufa kwa kukosa maji na pembeni yako kuna kisima cha maji, wewe kama binadamu lazima uingiwe na roho ya huruma ya kutaka kumsaidia kuteka maji umpe lakini ukikumbuka sheria za dini zitakuambia leo huruhusiwi kufanya kazi, kwahiyo utaamua wewe usikilize roho au dini.