Dr, vijana ni wengi sana wenye haya mawazo na nasema hivi kwa kujiamini kabisa kwasababu nipo kwenye hii industry ya IT hivyo nakutana na vijana wengi wenye bunifu nyingi sana! Changamoto yao kuu ni CAPITAL, kwasababu huo ndio msingi wa kilakitu kama kupata timu ya kufanya nayo kazi, vitendea kazi, vibali, nk.
Project kama WhatsApp from scratch ni kazi kubwa mno, sio ya siku moja, wiki, mwezi, au mwaka bali inahitaji muda, timu na vitendea kazi vya kutosha! Kama umefanya research ndogo tu, angalia ni project ngapi za IT za hapa bongo zilizokuwa funded kwa namna tofauti tofauti ambazo zipo hai hadi leo? Nyingi zimekufa na ni kwasababu wanakuwa na wazo zuri ila wanakuwa funded kwa mtaji utakaotosha kuunda bunifu yao na kui-test tu, wanapofikia kwenye ku-launch na kuendesha mradi ndio wanagundua kuwa wanahitaji 20x ya mtaji waliotumia hadi wafikie watumiaji watakaosababisha mfumo ujiendeshe na kuanza kutengeneza faida, mwisho wa siku bunifu zao zinapotea chap!
Kwa takwimu za
reveliolabs inasema WhatsApp ina wafanyakazi 2600+ na kwa takwimu za
comparably zinasema kwamba mishahara ya WhatsApp ina-range kati ya $48K hadi $194K (annual) kwa wafanyakazi wa kawaida kulingana na vitengo vyao (tena hao wa $48K ni cutomer support, haha). Sasa hebu tuachane na hayo madola, unadhani kijana mwenye wazo lake hata akipewa mtaji tuseme labda Tsh 50M atengeneze app yake, kiasi hicho hicho kitaweza kulipa designers, devs, running costs, marketing, office, mishahara, chakula, nk kwa at least timu ya watu 10 wa kuanza nao?