JF kuna wataalam wa kila nyanja.....Wadau ninamtaji wa mil 9 ambazo nimezipata kwenye uchimbaji wa dhahabu,
Ila nahofia kizirudisha kwenye uchimbaji maana ni kazi ya bahati.
Natamani sana kufanya biashara ya nafaka dar, ila sina uzoefu. na yalikuwa matamanio yangu ya mda mrefu kufanya hii biashara.
Tadhari mwenye uzoefu anisaidie.
Wadau ninamtaji wa mil 9 ambazo nimezipata kwenye uchimbaji wa dhahabu,
Ila nahofia kizirudisha kwenye uchimbaji maana ni kazi ya bahati.
Natamani sana kufanya biashara ya nafaka dar, ila sina uzoefu. na yalikuwa matamanio yangu ya mda mrefu kufanya hii biashara.
Tadhari mwenye uzoefu anisaidie.
Nafaka zote kwa dsm zinahitajika.Kwa sasa niko kahama
Kwa hyo ni bora kuchukua nafaka mkoani na kupeleka dar kuuza kwa jumla na siyo kufungua duka la nafakaNafaka zote kwa dsm zinahitajika.
Ila nakushauri deal na nafaka ambazo zinawalaji wengi.
Hasa mahindi..mchele..maharage na karanga.
Kwasasa sembe ni 1450/=
Karanga 2800 hadi 3000/=
Inshu kubwa huwa ni gharama za usafirishaji..soko la uhakika lipo.
#MaendeleoHayanaChama
Kuna mtu juu kakushauri uwe unanunua dhahabu na kuuza?Sawa ndugu yangu
Hiyo biashara Ni Kama betting tu siku unaweza kuamka masikini ,siku unaweza kuamka tajiri..Mkuu Mimi nakushauri kwanini usiwekweze kwenye Dhahabu?
Nafaka ni biashara pasua kichwa….faida ndogo + slow turnovers ukicheck una gharama za pango, kulipa mfanya kazi, na gharama za kusafirisha. Kama unataka unataka kufanya biashara ya chakula fungua genge….hela ipo kwenye genge.
Sokoni vitu bei chee ukija ushuani au sehem za makazi unauza hata double the price (fatilia utanikumbuka yet mtaji wake mdogo tu i.e. pango ya frame au kutengeneza banda)
Kikubwa anza kdgo kdgo usiweke mzigo mkubwa wa kuharibika na kama ukiweka mzigo mkubwa uza very fair prices ili uwahi maliza kesho ulete stock mpya na ku attract wateja kuwa mbunifu tu na genge lako lionekane la kishua / lenye utofauti.
Nafaka for me is a No, Duka La Mangi nalo No, Kama hutaki kuchafuka nunua gari used fanya uber na ukomae mwenyewe.
Kwenye kutafuta mshipa wa noma weka pembeni kabisa maana aibu ya umasikini na fedheha ni kubwa sana kuliko aibu ya kutafuta.
Mtazamo Wangu Tu. Ahsante