Ukiachana na matangopori tuliyolishwa kuwa ukifanya hivi unakufuru ama ukifanya vile utapata dhambi na kufikiri kwa fikra huru utagundua juu ya dhima halisi ya hizi dini.
1. Dini ni Social institutions ambazo zilibuniwa mahususi ili kumdhibiti binadamu kwa kumlisha itikadi na kumjengea hofu ili aweze kukaa kwa amani na jamii inayomzunguka. Kwa maana hiyo dini inafanya jukumu kama taasisi zingine zilizo kwenye jamii mfano; Mahakama, Shule, vyuo, Magereza na Polisi.
2. Imani ni zao la utamaduni, mafundisho ama experience ya maisha juu ya jambo, mtu, kitu ama tabia. Kwahiyo imani imejengwa katika msingi huo kwa maana imani inatokana na dhana ya kuamini.
3. Kwa muktadha wa sasa Dini inatumika kama chombo cha kubebea imani. Ni kama vile makahama ambayo ni social institution inavyotumika kutafsiri sheria ambayo ni mafundisho jambo sahihi na lisilo sahihi kwa mujibu wa taratibu za jamii husika. Kwahiyo mahakama na sheria ni vitu viwili tofauti ila vinafanya kazi kwa pamoja.
HITIMISHO:
Dini na imani ni vitu viwili tofauti ila vinavyofanya kazi kwa pamoja. Dini ni chombo kinachotumika kubeba imani.
Vyote kwa pamoja vilibuniwa na watu wenye akili nyingi sana kwa lengo la kumdhibiti Binadamu kifikra, kimatendo na kutengeneza ustaarabu kwenye jamii. Hutumia njia njia ya mafundisho, kujenga hofu na uwoga, pamoja na ahadi za adhabu na tuzo kwa wanaotenda kwa mujibu wa mafundisho na wale wanaoenda kinyume. Dhana kama vile dhambi, kukufuru ni nyezo kuu za kudhibiti uwezo wa Binadamu kuwa na hofu ya kuhoji mamlaka zilizoasisi imani hizi na mapungufu ambayo kwasasa yanadhihirika katika imani hizi
Dini ni mifumo iliyotengenezwa na watu ila imani ni hisia ya mtu moyoni kuhusu muumba wake.Imani haina tofauti na itikadi. Imani inakupa mwelekeo wa kusimamia masuala yanayohusu utawala usioonekana kwamba ndiyo unaotawala fikra na hisia kuhusu uwepo, uumbaji na yanayodhanika kujiri baada ya nafsi na roho kuachana na mwili. (Hii ni tafsiri yangu)
Dini, ni utaratibu uliobuniwa na unatumika kudhibiti aina ya imani ambayo mtu anapaswa kufuata. Dini inasajiliwa lakini Imani haisajiliki.
Basi nimeona wazimu sana kuwa mwanadamu amelazimisha Imani na Dini vifungamane na kwenda pamoja ilihali kimoja ni bangi kingine ni kitakatifu.
Haya, wanazuoni akina Mzito Kabwela na wengineo, mnaweza kunielimisha beyond hayo madhanifu yangu kwenye Imani na Dini?
nisaidie wew unavyoelewaHii maana umeikariri
Naamini unayo maelezo namna ulivyoelewa hii phrase
Ukisoma post ya kwanza nimefanya ulivyoomba.nisaidie wew unavyoelewa
ni kweli dini inadhibiti je haisaidii kumfanya mtu kuwa na utambuzi na itikadi kwenye fikra zake?Ukisoma post ya kwanza nimefanya ulivyoomba.
Wewe unaelezea void inayoweza kuwa dhahiri na umejielekeza kwenye imani inayoleta miujiza.
Tujadili imani kama msingi unaosimika utambuzi, uwepo na itikadi kwenye fikra na siyo matumaini
Eneo la dini ni mfumo dhibiti na siyo saidizi
asante kwa kunielimisha inamaana ukifuata dini fulan unakuwa hauko huru kiiman?1. Malezi
2. Jamii anayokulia
3. Mazingira
4. Mtiririko wa matukio
Sina maana hiyoasante kwa kunielimisha inamaana ukifuata dini fulan unakuwa hauko huru kiiman?
jamii ndo imetufanya tuwe watumwa wa kukubali iman wanayotupatia ukioji sana wanakuona mkorofi na msumbufuSina maana hiyo
Muktadha ni kuruhusu ufahamu wako kupokea elimu pana kuhusu Mungu. Hoji kila kitu na mwishowe utakuwa na uamuzi.
Huwa tunakwepa kutumia HIYARI zetu, tunasubiri tupewe mwelekeo
Nakumbuka nilimuuliza marehemu baba yangu (ambaye baada ya kustaafu alikuwa mchungaji wa kanisa lake) kuhusu uwepo wa majina ya Mungu kwenye makabila yetu. Nikihoji kuhusu Waafrika kuitwa wapagani, makafiri wasio na imani.jamii ndo imetufanya tuwe watumwa wa kukubali iman wanayotupatia ukioji sana wanakuona mkorofi na msumbufu
upo sahihi dini mtego na inavyoonekana huna dini maana kwenye dini ukihoji sana wanakuita mataifa au kafiriNakumbuka nilimuuliza marehemu baba yangu (ambaye baada ya kustaafu alikuwa mchungaji wa kanisa lake) kuhusu uwepo wa majina ya Mungu kwenye makabila yetu. Nikihoji kuhusu Waafrika kuitwa wapagani, makafiri wasio na imani.
Alibaki kushangaa maana majina hata ya watoto kiafrika yanathibitisha uwepo wa Mungu.
Hizi dini ni bangi za watu kuwavuna kiakili wanajamii na kujimilikisha limitation ya kufikiri, kuhoji hata kupokea mawazo mapya
Mkuuupo sahihi dini mtego na inavyoonekana huna dini maana kwenye dini ukihoji sana wanakuita mataifa au kafiri
Imani ni kuwa na hakika na mambo yatarajiwayo ni bayana ya mambo yasiyoonekana!Imani haina tofauti na itikadi. Imani inakupa mwelekeo wa kusimamia masuala yanayohusu utawala usioonekana kwamba ndiyo unaotawala fikra na hisia kuhusu uwepo, uumbaji na yanayodhanika kujiri baada ya nafsi na roho kuachana na mwili. (Hii ni tafsiri yangu)
Dini, ni utaratibu uliobuniwa na unatumika kudhibiti aina ya imani ambayo mtu anapaswa kufuata. Dini inasajiliwa lakini Imani haisajiliki.
Basi nimeona wazimu sana kuwa mwanadamu amelazimisha Imani na Dini vifungamane na kwenda pamoja ilihali kimoja ni bangi kingine ni kitakatifu.
Haya, wanazuoni akina Mzito Kabwela na wengineo, mnaweza kunielimisha beyond hayo madhanifu yangu kwenye Imani na Dini?