Naomba mnielimishe umuhimu wa Imani na Dini

Naomba mnielimishe umuhimu wa Imani na Dini

Huwezi kusema akili ya binadamu ni kama akili za viumbe wengine na hapo hapo unakiri kuwa binadamu ana uwezo wa juu sana wa akili.

Yaani kwa lugha rahisi maelezo yako yanakinzana.
Hata binadamu tu tunatofautiana uwezo wa kiakili sembuse itakua viumbe vingine mkuu?

Akili za viumbe vyote akiwemo binadamu ni kupambana na mazingira ili kuishi as long as possible ili kuzaliana.

Binadamu hana umaalumu wowote dhidi ya viumbe wengine…….. anaweza akatoweka na Dunia ikaendelea fresh tu( tena in fact the World is better palace kwa mazingira na viumbe wengine without us).

Tofauti na watu wa IMANI mnao AMINI tumeumbwa MAALUMU kwenye Ulimwengu na tuna wajibu wa kumtafuta Muumba au kutafuta “kweli za akili” au sijui kutafuta lengo la maisha wakati maisha ni mafupi sana na ni mapambano ku survive na unakufa wakati wowote either wakati unazaliwa, ukiwa mdogo au mtu mzima the same kwa viumbe wengine
 
Huu ni uelewa wako. Na hii ndio inafanya tofauti kati ya wanyama (utambuzi) na mnyama mwenye busara (akili).
Mkuu hiyo ni FACT na sio uelewa wangu……… unless upinge kwa hoja.

Sina shaka tunakubaliana Lengo baada ya kujikuta umezaliwa ni kupambana uendelee kuishi as long as possible, kisha fursa utazaliana ili existence ya binadamu iendelee kuwepo Duniani utakapo kufa

Sasa nje ya LENGO hilo ambalo analo Panzi, Samaki, Kunguru na viumbe wengine wote……… ni nini IMANI inafanya haswa kwenye MAISHA ya Binadamu.
Tofauti ya Baadhi ya Wachina wasio AMINI na Wakristo au Waislam au Wewe wenye IMANI ni nini KIMAISHA?
 
Hata binadamu tu tunatofautiana uwezo wa kiakili sembuse itakua viumbe vingine mkuu?

Akili za viumbe vyote akiwemo binadamu ni kupambana na mazingira ili kuishi as long as possible ili kuzaliana.
Kutofautiana huko ndio kunafanya binadamu awe mnyama na binadamu awe mtu mwenye busara(intellect).
 
wewe ukishaona kuna mambo mengi yapo tu hata binadam hajui yalifanyikaje jua IPO Nguvu yenye mamlaka zaidi ya chochote. We unaona jua lina toka Mashariki kwenda magharibi na hakuna wa kubadilisha hilo;

Wewe unaona kila siku watu wanazaliwa na kufa hata hujui, wanakwenda wapi...
Au pengine; wewe unakula chakula kina chakatwa hadi uchafu unatoka huoni maajabu
Wewe ukiamua kufanya kitu, miguu na mikono yako inaelewa unachotaka na kufuata maelekezo; huoni maajabu na mengine mengi

Ungekuwa umesoma Biology vizuri ukafuatilia utendaji kazi wa mwili wako; Ukaona grid ya umeme kwenye moyo; ungeamini kuna mtaalam kuliko hawa waote walipo duniani.
Utendaji kazi wa mwili wa mtu; ni muujiza kuliko hata miujiza mingine unayo ona huko...

Ili kuijuia hiyo Nguvu yenye mamlaka kuliko vyote; ndio hapo ikawepo elimu ya dini...
Kimsingi dini ni Elimu Inayotolewa kufundisha watu kutukuza ukuu wa hiyo Nguvu yenye mamlaka yote...
Sisi tuna amini kuwa, hiyo Nguvu ni Mungu mmoja tu mwenye mamlaka yote, ambaye hana mshirika, haja zaa wala hajazaliwa na hafanani na kitu chochote.
Hata wewe umeelewa ulichoandika?

Soma heading na passage uelewe. Hayo uloyoyaandika hayahusiani na lengo la mada.
 
Acha mimi, hata babu yangu hajui vizazi vitano tu nyuma yake, anamjua babu yake tu, baba mzaa babu yake anamsikia sikia tu kwambali, wanyuma yake hanataarifa zake kabisaaa

Sivijui vizazi vyangu vitano vya nyuma, vizazi vyangu 10 mbele hawatajua lolote kuhusu mimi…….. sababu hilo sio lengo mama la MAISHA

Kikubwa kwenye maisha sio family tree……. Lengo kuu Ni kwamba umejikuta umezaliwa, utampambana kuishi as long as possible, utazaliana then unakufa………kwisha habari yako

Hapo utakapo jikuta umezaliwa ndio kwa asilimia kubwa patakufanya wewe UAMINI nini.
Mtoto aliyezaliwa na Rabi wa Kiyahudi pale Haifa Israel ana nafasi ndogo sana KUAMINI vinginevyo zaidi ya kuwa Myahudi………..same applied kwa atakaye zaliwa Gaza, Viunga vya Tehran na wazazi washiah, Pyangyong China, India kwa wahindu, Waadzabe Arusha nk nk

Mkuu Dunia ina mamiaka Dahali, hakuna anayejua huku nyuma kabla ya utunzaji kumbukumbu wa kudumu kuanza mambo yalikuaje……… kuna theories na Imani tu ilikuaje.

Binadamu ni social animals, social animals wote duniani wanaishi kwenye vikundi(jamii) na kufuata miongozo na taratibu ilikuepuka migogoro isiyo na lazima……. Na kwa msingi huo basi ni rahisi zaidi kwa kikundi cha jamii kua na imani moja ya Mungu na kuwa na taratibu za kufanya(dini) ili kumuadhimisha Mungu wao.
Ni ngumu kufikiri kwamba eti jamii fulani walianza kwa kila mmoja kuamini Mungu anavyojua yeye kuliko kufikiri walikua wanafanya hivyo kwa ummoja wao na taratibu maalumu kwa wote(ritual) kupitia viongozi wao ambao kwa sehemu kubwa ndio walikua watoa miongozo

Ndio maana nikaandika kwamba IMANI ya Mungu inatekelezeka zaidi kupitia DINI ingawaje wapo Tusio amini kabisa, wapo wanaotilia mashaka, wapo pia ambao wanaamini lakini hawavutiwi na DINI

Kukinzana na DINI ni kukinzana na asili ya binadamu kama social animal…….Kufanya mambo kwa utaratibu maalamu wa umoja
Unajua unatamani kujenga hoja lakini unashindwa kuelewa unalosimamia.

Haujaweka precedence yeyote inayotupa uthibitisho kuwa IMANI ithibati yake ni dini.

Dini ni nini
Imani ni nini

Tafakari
 
Unajua unatamani kujenga hoja lakini unashindwa kuelewa unalosimamia.

Haujaweka precedence yeyote inayotupa uthibitisho kuwa IMANI ithibati yake ni dini.

Dini ni nini
Imani ni nini

Tafakari
Kwa lugha rahisi kabisa ipo hivi

IMANI ni kukubali jambo ambalo Halithibitiki

DINI ni utaratibu na muongozo wa utekelezaji wa IMANI fulani………..mara nyingi ni IMANI ya MUNGU

DINI haiwezi kusimama peke yake bila IMANI…….. DINI zote msingi wake ni IMANI

IMANI zipo nyingi sana, Ila IMANI ya MIUNGU inatekelezeka zaidi kupitia DINI.
85% ya watu Duniani wana AMINI Mungu kupitia DINI, na Religiously Unaffiliated ni chini ya 7% ya watu wote Duniani

Watu wengi ambao ni Religiously unaffiliated ni watu ambao mwanzo waliamini Mungu kupitia DINI, lakini kwakuwa DINI zinaongozwa na Binadamu wenye Madhaifu mengi wakaachana na kumuhushanisha Mungu na DINI na wakabaki wana IMANI ya Mungu kwa namna anayoina inafaa yeye(jambo ambalo ni gumu kidogo)

Precedence yangu kuhusu ithibati ya IMANI ya Mungu ni DINI ni hii

1, ASILI YA BINADAMU
Binadamu ni social animals wanaoishi kwa pamoja na kufanya mambo yao yote kwa uumoja na utaratibu maalumu(sheria, kanuni, Mila, Tamaduni nk)……… kwahiyo hata NADHARIA ya Mungu ilipoibuka ni rahisi zaidi wao kuwa na utaratibu na miongozo ya kumuadhimisha Mungu wao kwa pamoja ambayo ndio DINI yenyewe……… Ni ngumu kudhani labda Wamasai kila mmoja alianza kuabudu Mungu wake lakini ni rahisi zaidi kudhani kwamba IMANI ilipo ibuka viongozi walitoa muongozo wa namna ya kumuadhimisha Mungu wao ambao ndio DINI yenyewe.

MITUME na MANABII
Ukiachana na DINI za kale, DINI zote zilizoletwa na watu wanaodai wametumwa na Mungu ndio hao hao waliileta IMANI hiyo kupitia DINI.
Mfano Mudi na Fundi selemara wao walidai wametumwa na Mungu kuleta Miongozo ambayo ndio DINI zenyewe…………. Hapo inakua ngumu kutenganisha IMANI ya Mungu na DINI

ZAMA HIZI
Kwa karne yetu hii tunaijua IMANI ya Mungu kupitia DINI za wazazi/walezi/jamii zetu……….. HAKUNA anaye anza na IMANI ya Mungu tu bila kupitia DINI.

Ni ngumu kidogo kuwa na IMANI ya Mungu tu bila DINI(miongozo) kwasababu Dini(miongozo) ndio hutoa misingi ya kusimama na IMANI ya Mungu

Sio rahisi kwa “makosa ya kiakili” kumpa kila mmoja muongozo wa IMANI ya Mungu inataka nini kwasababu tupo tofauti sana, kuna watu wana mawazo na fikra za ajabu huwezi kuamini, na wao akili zao zina watuma wako sahihi kabisa bila tone la mashaka.
 
Nakumbuka nilimuuliza marehemu baba yangu (ambaye baada ya kustaafu alikuwa mchungaji wa kanisa lake) kuhusu uwepo wa majina ya Mungu kwenye makabila yetu. Nikihoji kuhusu Waafrika kuitwa wapagani, makafiri wasio na imani.

Alibaki kushangaa maana majina hata ya watoto kiafrika yanathibitisha uwepo wa Mungu.

Hizi dini ni bangi za watu kuwavuna kiakili wanajamii na kujimilikisha limitation ya kufikiri, kuhoji hata kupokea mawazo mapya
Hapa umemaliza kila kitu mkuu. Hii ni miradi ya watu kuvuna sadaka za kondoo wao (cf Mwamposa) huku kondoo wakidhibitiwa wasihoji kitu chochote. Kuna watu wanaijua biblia au korani barabara lakini ukiwachunguza vizuri utagundua hawana imani. Wanaichukulia dini kama kazi zingine zinazowaingizia kipato.
 
Siwabezi washika dini. Lakini hebu tuangalie huo uraibu wa kidini husababishwa na nini?
Uraibu wa kidini hutokana na imani iliyopitiliza inayovuka akili ya kawaida ya mwanadamu. Yaani mtu unakuwa kama umeshikiwa akili.
 
 
Imani haina tofauti na itikadi. Imani inakupa mwelekeo wa kusimamia masuala yanayohusu utawala usioonekana kwamba ndiyo unaotawala fikra na hisia kuhusu uwepo, uumbaji na yanayodhanika kujiri baada ya nafsi na roho kuachana na mwili. (Hii ni tafsiri yangu)

Dini, ni utaratibu uliobuniwa na unatumika kudhibiti aina ya imani ambayo mtu anapaswa kufuata. Dini inasajiliwa lakini Imani haisajiliki.


Basi nimeona wazimu sana kuwa mwanadamu amelazimisha Imani na Dini vifungamane na kwenda pamoja ilihali kimoja ni bangi kingine ni kitakatifu.

Haya, wanazuoni akina Mzito Kabwela na wengineo, mnaweza kunielimisha beyond hayo madhanifu yangu kwenye Imani na Dini?

UPDATE
nimeyajibu maswali yako yote hapa karibu.


 
Back
Top Bottom