Naomba mnielimishe umuhimu wa Imani na Dini

Naomba mnielimishe umuhimu wa Imani na Dini

Mfano wako wa kikombe cha babu wa Loliondo na maji ya Mwamposa ni ushahidi kuwa watu hao (watanzania wengi) hawana uelewa wa kina wa mambo na elimu ya vitu.

Jambo hilo la kikombe cha babu au maji ya Mwamposa sio mambo ya imani wala hayahusiani na imani kwa sababu hayana sifa hizo.

Imani sio kukubali bila kuwa na uelewa au kujua jambo unalolikubali. Kwa sababu kukubali kitu ambacho hukijui(hujui) ni kukubali kufanya makosa isipokuwa kama jambo hilo ni la kweli.

Kuhusu imani kutoka kwa Mungu (faith). Hii inahusu na inaeleza 'kweli za kiakili'. Jinsi mambo yalivyo.

Kutothibitika kisayansi kwa 'kweli za kiakili' hakuelezwi kuwa jambo hilo halipo. Kunaweza kuwa kwa sababu za maarifa au huruki ambazo zinapita uelewa wetu wa sasa.
Hii ndio CHANGAMOTO kubwa sana ya watu wa IMANI kwa kila mmoja kuona IMANI ya mwenzake sio SAHIHI ila anachoa jua na kuAMINI yeye.

Wewe unawaona Wanaoamini Kikombe cha Babu au Maji ya upako kwamba wamekengeuka kwa kukosa sifa za IMANI lakini wenzako wana IMANI hiyo, na wanakuona wewe umekengeuka na IMANI yako.

Mkuu The likes of Kikombe na maji ya upako havijaanza TZ vipi Dunia nzima toka enzi na enzi na vitaendelea kuwepo…… sio issue ya waTz kukosa uelewa…….. ni issue ya kwamba IMANI haitaki LOGIC ndio maana kila mmoja anamuona mwenzake hana uelewa

Inawezekana vipi kusema kitu fulani kipo wakati HAKITHIBITIKI kwa namna yoyote ile?

Wewe ulizijuaje hizo kweli za akili halafu wengine washindwe kuzijua, ulitumia metrics/criteria zipi kujua jambo ambalo “limepita uelewa wetu”?………. Kama UMELIJUA basi halijapita uelewa wetu
 
Mkuu sio sahihi kubishana. Yafaa kujiuliza na kufuatilia (kuchunguza): hapa tulipo ndio mwisho wa kila kitu?
Akili ya binadamu ni halisi?
Imani ni nini? Sayansi ni nini?
Imani inatoka wapi na sayansi inatoka wapi? Uthibitisho maana yake ni nini? Tunajuaje? Na tunajuaje kuwa tunajua?
Kwa nini tunajua?
Na mwisho kabisa vitu vyote vilivyopo maana yake ni nini? Nini maana ya mambo haya?

Pamoja na kasoro zinazoweza kuwepo za uelewa, za utamaduni lakini hiyo haimanishi kuwa kuna 'Kweli' mbili au nyingi. Ukweli ni mmoja tu na unawahusu watu wote popote. Kuuwa, wizi, uzinzi, uharibifu wa mazingira, kupenda miungu, uongo, kutoheshimu wakubwa, kushindwa kuwajibika kufanya hivyo kwa sababu zozote zile ni kosa dhidi ya akili.
Kwa sababu hiyo ni wajibu wa kila mtu katika umri wake wa kuanza kutumia akili kutafuta na kujua ukweli hasa ukweli kuhusu dini.
 
Mfano wako wa kikombe cha babu wa Loliondo na maji ya Mwamposa ni ushahidi kuwa watu hao (watanzania wengi) hawana uelewa wa kina wa mambo na elimu ya vitu.

Jambo hilo la kikombe cha babu au maji ya Mwamposa sio mambo ya imani wala hayahusiani na imani kwa sababu hayana sifa hizo.

Imani sio kukubali bila kuwa na uelewa au kujua jambo unalolikubali. Kwa sababu kukubali kitu ambacho hukijui(hujui) ni kukubali kufanya makosa isipokuwa kama jambo hilo ni la kweli.

Kuhusu imani kutoka kwa Mungu (faith). Hii inahusu na inaeleza 'kweli za kiakili'. Jinsi mambo yalivyo.

Kutothibitika kisayansi kwa 'kweli za kiakili' hakuelezwi kuwa jambo hilo halipo. Kunaweza kuwa kwa sababu za maarifa au huruki ambazo zinapita uelewa wetu wa sasa.
Wengi watakukosoa lakini umeandika jambo zuri na muhimu.

Shida ya wengi ni kuukabili ukweli.
 
Mkuu sio sahihi kubishana. Yafaa kujiuliza na kufuatilia (kuchunguza): hapa tulipo ndio mwisho wa kila kitu?
Akili ya binadamu ni halisi?
Imani ni nini? Sayansi ni nini?
Imani inatoka wapi na sayansi inatoka wapi? Uthibitisho maana yake ni nini? Tunajuaje? Na tunajuaje kuwa tunajua?
Kwa nini tunajua?
Na mwisho kabisa vitu vyote vilivyopo maana yake ni nini? Nini maana ya mambo haya?

Pamoja na kasoro zinazoweza kuwepo za uelewa, za utamaduni lakini hiyo haimanishi kuwa kuna 'Kweli' mbili au nyingi. Ukweli ni mmoja tu na unawahusu watu wote popote. Kuuwa, wizi, uzinzi, uharibifu wa mazingira, kupenda miungu, uongo, kutoheshimu wakubwa, kushindwa kuwajibika kufanya hivyo kwa sababu zozote zile ni kosa dhidi ya akili.
Kwa sababu hiyo ni wajibu wa kila mtu katika umri wake wa kuanza kutumia akili kutafuta na kujua ukweli hasa ukweli kuhusu dini.
AKILI ni uwezo wa kiumbe kupokea taarifa, kisha kuchakata na kutoa maamuzi……….. mchakato huu ndio AKILI
Na ndio maana kuna genius na vichaa wasio na akili

Akili inatoa maamuzi kutokana na ilivyolishwa kulingana na Mila, Tamaduni,Imani na nyakati…….
Native Chinese, Afaghanistan, Jews, Masai, Adzabe……. Hizi jamii zinatafsiri tofauti kabisa kuhusu uzinzi, mazingira, Miungu nk
Wewe unaona hayo mambo ni kosa dhidi ya akili sababu Dunia hivi sasa imestaarabika na kuset standard(human rights) inayofanya uone ni kosa la kiakili…….. soma historia ya dunia uone Dunia ilikopitia mkuu,
Au unadhani miaka 5000 nyuma mitazamo iko sawa na sasa?

Binadamu hana tofauti yoyote na panzi au samaki au kunguru au kiumbe kingine chochote kile linapokuja swala la MAISHA

Atazaliwa,atapambana kuishi, atazaliana kisha atakufa……… HAKUNA maana zaidi ya hiyo.

Wakati unapambana kuishi unaweza kuamua kutafsiri vyovyote upendavyo kudhani hilo ndio kusudi lako la maisha

Viumbe vyote Duniani vinaishi kulingana na Sayansi
Sayansi haina maajabu yoyote…….. ni logics tu ambayo mtu yeyote akijua anafanya na tokeo linakua moja tu

IMANI/dini na mambo ambayo binadamu ameyaibua pale anaposhindwa kujua baadhi ya mambo.

Kinacho tushughulisha sana binadamu dhidi ya viumbe wengine ni kwamba tuna intelligence kubwa sana kuliko viumbe wengine na ndio maana tunahangaika kutafuta maana ya kila kitu jambo ambalo linatufanya tunazidi kuvumbua mambo mapya kisayansi(sio IMANI)kila leo kusaidia kurahisisha mapambano ya maisha
 
Wengi watakukosoa lakini umeandika jambo zuri na muhimu.

Shida ya wengi ni kuukabili ukweli.
Mkuu IMANI au DINI zina UKWELI upi ambao watu wanashindwa kuukabili?
 
Mkuu IMANI au DINI zina UKWELI upi ambao watu wanashindwa kuukabili?
1.
Imani ni njia sahihi ya mtu kuwa karibu na Maker wake. Lakini ni Hiyari kuifuata

2.
Dini ni ujanja, ghiliba na hadaa na inalazimishwa kufungamana na Imani. Lengo kuu ni kupindisha ukweli, kumiliki hiyari na kuhodhi mamlaka, uweza na Omnipotence ya Maker
 
Kwa ufahamu wangu IMANI zipo nyingi sana…..,,, Lakini IMANI ya Maker aka Mungu inatekelezeka zaidi kupitia DINI

IMANI zote za Mungu zinasadiki Maker aliumba ulimwengu na kutoa miongozo ya kufuata ambayo ndio DINI yenyewe

Huwezi kumuamini ALLAH au YEHOVA halafu usifuate Uyahudi au Ukristo au Uislam…….. same applied kwa dini zote

Watu hao hao waliomtengeneza Mungu ndio hao hao waliotengeneza na miongozo(dini) ya kufuata………..ukikataa Uislam umkatae na Allah, Ukimkataa Yehova ukatae na Uyahudi na ukristo halafu umtengeneze Maker wako binafsi ambaye utajua wewe unamuabudu vipi na kwa miongozo ipi

Haiwezekani umuamini Mudi kuhusu Allah tu halafu usimuamini kwenye Quran na uislam
 
Akili inatoa maamuzi kutokana na ilivyolishwa kulingana na Mila, Tamaduni,Imani na nyakati…….
Native Chinese, Afaghanistan, Jews, Masai, Adzabe……. Hizi jamii zinatafsiri tofauti kabisa kuhusu uzinzi, mazingira, Miungu nk
Wewe unaona hayo mambo ni kosa dhidi ya akili sababu Dunia hivi sasa imestaarabika na kuset standard(human rights) inayofanya uone ni kosa la kiakili…….. soma historia ya dunia uone Dunia ilikopitia mkuu,
Au unadhani miaka 5000 nyuma mitazamo iko sawa na sasa?
Watu wote wa nyakati zote tuko chini ya sheria moja (universal laws). Kile ambacho ni kosa dhidi ya akili kinawahusu watu wote wa nyakati zote.

Imani potofu huleta uelewa potofu na hivyo tamaduni na mila mbaya. Imani potofu na tamaduni mbaya sio sababu au kisingizio (excuse) cha makosa dhidi ya akili. Kwa sababu wajibu wa kwanza wa mtu ni kutafuta ukweli hasa ukweli kuhusu dini.

Historia ya dunia inaonyesha jambo moja dhahiri, 'ujinga'. Ujinga ni tatizo kubwa duniani na kwa sababu hiyo watu wengi ni wahanga.

Matukio ya historia ya duniani yana sura mbili. Kwanza yanaonyesha ujinga kama tatizo kubwa la binadamu. Na pili maarifa ya binadamu ambayo yanakua kutoka kipindi hadi kipindi. Na hili la mwisho linahusu ukweli.
 
AKILI ni uwezo wa kiumbe kupokea taarifa, kisha kuchakata na kutoa maamuzi……….. mchakato huu ndio AKILI
Maana hii ya akili inamweka mtu kundi moja na wanyama wengine which is somehow correct.

Wanyama wote wana uwezo wa kupokea taarifa, kuchakata na kutoa maamuzi (utambuzi). Lakini akili ya binadamu ni nini?

Akili ya binadamu maana yake ni kufikiri na kufanya uchunguzi na kujua na kujua kufanya mambo bila kukosea.

Makosa yanaendelea, kwa mfano tamaduni mbaya, umasikini, migogoro kwa sababu ya 'utambuzi' na si 'akili'.
 
Binadamu hana tofauti yoyote na panzi au samaki au kunguru au kiumbe kingine chochote kile linapokuja swala la MAISHA

Atazaliwa,atapambana kuishi, atazaliana kisha atakufa……… HAKUNA maana zaidi ya hiyo.

Wakati unapambana kuishi unaweza kuamua kutafsiri vyovyote upendavyo kudhani hilo ndio kusudi lako la maisha

Viumbe vyote Duniani vinaishi kulingana na Sayansi
Sayansi haina maajabu yoyote…….. ni logics tu ambayo mtu yeyote akijua anafanya na tokeo linakua moja tu
Binadamu ni sawa na viumbe vingine kwa msingi huu, wote wanatoka kwa chanzo kimoja. Lakini hadhi yao ni tofauti.

Panzi ana akili ya utambuzi. Tofauti na akili ya binadamu panzi hawezi kufikiri na kufanya uchunguzi na kujua na kujua kuleta au kuunda vitu vingine vipya kwa kutumia vitu vya asili vilivyopo, uvumbuzi na ugunduzi.

Jinsi hii ya akili ya binadamu inaeleza zaidi ya uzoefu wa kawaida. Kile ambacho maarifa ya binadamu yametupatia na yanatupatia na kutusaidia kuelewa kwa undani kuhusu ulimwengu ni hali ambayo haiwezi kuwa tu mchezo wa vitu usio kuwa na lengo.

Kwa sababu hata katika shughuli za kila siku za mtu hakuna wazo wala tendo ambalo linafanyika bila kuwa na sababu au lengo.
 
IMANI/dini na mambo ambayo binadamu ameyaibua pale anaposhindwa kujua baadhi ya mambo.

Kinacho tushughulisha sana binadamu dhidi ya viumbe wengine ni kwamba tuna intelligence kubwa sana kuliko viumbe wengine na ndio maana tunahangaika kutafuta maana ya kila kitu jambo ambalo linatufanya tunazidi kuvumbua mambo mapya kisayansi(sio IMANI)kila leo kusaidia kurahisisha mapambano ya maisha
Imani na hapa namaanisha imani kutoka kwa Mungu ni uelewa wa kina au wa hali ya juu wa mambo na elimu ya vitu (kujua). Kwa lugha rahisi ni jinsi mambo yalivyo, ukweli.

Ubongo wa binadamu ambao ndio mahali pa shughuli za kiakili unafanya kazi katika hali ya kusadiki (believe). Hii maana yake ni kwamba hatuwezi kujua, na au tunajuaje kuwa tunajua ila kwa kusadiki kwanza. Kwa hiyo kila mtu anasadiki (everyone is believing either in God or gods) kwa sababu hiyo ni hali ya kiakili yaani ndivyo ubongo wa binadamu unavyofanya kazi.

Hivyo basi, mtu anaweza kudai haamini Mungu kwa sababu za ujinga lakini mtu huyo hawezi kusema haamini chochote. Jambo muhimu si kama kuna Mungu au hakuna Mungu. Jambo muhimu ni 'kujua ukweli' na hasa ukweli kuhusu dini.

Imani inashughulikia kweli za kiakili na dini (Kanisa) ni chombo cha kufundisha, kufafanua na kutekeleza mambo matakatifu ya Mungu.
 
Kwa ufahamu wangu IMANI zipo nyingi sana…..,,, Lakini IMANI ya Maker aka Mungu inatekelezeka zaidi kupitia DINI
Hii sentensi inadhihirisha namna upuuzi unaoitwa DINI ulivyofanikiwa kuua independent thinking capability ya wengi kwenye jamii zetu.

Endelea kushika dini ambao imekuja baada ya IMANI
 
Hii sentensi inadhihirisha namna upuuzi unaoitwa DINI ulivyofanikiwa kuua independent thinking capability ya wengi kwenye jamii zetu.

Endelea kushika dini ambao imekuja baada ya IMANI
Mimi siamini katika Mungu, uchawi, shetani nk nk…….. Mimi nasimama na Sayansi(logic)

Wewe hizo taarifa za DINI imekuja baada ya IMANI umezitoa wapi mkuu?……….. Hivi kwanini watu wa IMANI mnapenda kuforce unacho AMINI wewe ndio SAHIHI?

Nimetoa mfano, aliye mtengeneza Allah ndio aliutengeneza na Uislam
Kuukataa Uislam maana yake ni kumkataa Allah………. Wewe unatoa wapi uhalali wa kumkataa Mungu wa wenzako kupitia DINI na uka muhalalisha Mungu wako uliyemtengeneza wewe ambaye hataki DINI?

IMANI yoyote ile ikiwemo Dini, Mungu ni vitu ambavyo havitaki matumizi sahihi ya AKILI na ndio vinaongoza kuua independent thinking capacity
 
Binadamu ni sawa na viumbe vingine kwa msingi huu, wote wanatoka kwa chanzo kimoja. Lakini hadhi yao ni tofauti.

Panzi ana akili ya utambuzi. Tofauti na akili ya binadamu panzi hawezi kufikiri na kufanya uchunguzi na kujua na kujua kuleta au kuunda vitu vingine vipya kwa kutumia vitu vya asili vilivyopo, uvumbuzi na ugunduzi.

Jinsi hii ya akili ya binadamu inaeleza zaidi ya uzoefu wa kawaida. Kile ambacho maarifa ya binadamu yametupatia na yanatupatia na kutusaidia kuelewa kwa undani kuhusu ulimwengu ni hali ambayo haiwezi kuwa tu mchezo wa vitu usio kuwa na lengo.

Kwa sababu hata katika shughuli za kila siku za mtu hakuna wazo wala tendo ambalo linafanyika bila kuwa na sababu au lengo.
Mkuu Akili ya binadamu ni kama akili za viumbe wengine…… zinatofautiana uwezo tu
Binadamu ana uwezo wa juu sana kiakili

Kumbuka hata Nyuki anatengeneza Asali kwa namna ya kipekee kabisa.

Akili za viumbe zipo kumuwezesha kiumbe husika kupambana ili kuishi as long as possible ili kutimiza lengo Mama la viumbe vyote ambalo ni Kuzaliwa, kupambana kuishi na kuzaliana

Toka enzi na enzi binadamu ametumia akili nyingi sana katika kupambana kuishi kufikia hapa tulipo kimaendeleo LAKINI hakuna maendeleo yoyote KIIMANI…..most of them bado wanatumia scriptures zilizoandikwa zama za UJINGA kabisa

Hakuna tofauti yoyote kati ya anaye anaye amini katika imani na asiye amini ila wote wana lengo mmoja wamejikuta wamezaliwa, watapambana kuendelea kua hai, watazaliana kisha watakufa………. IMANI haitawaongezea chochote wala haita punguza chochote labda uwe kiongozi wa kiimani na utumie sadaka kama means yako ya kipato( mapambano ya kuishi)

Binadamu hana umaalumu/upekee wowote wa ziada dhidi ya viumbe wengine………. Ila ana ziada ya AKILI tu
Maisha yako na ya Simba porini yana maana na lengo mmoja tu.
Ni ziada yetu ya akili ndio inatufanya TUAMINI tuna LENGO maalumu la kuwa Duniani.
 
Mimi siamini katika Mungu, uchawi, shetani nk nk…….. Mimi nasimama na Sayansi(logic)

Wewe hizo taarifa za DINI imekuja baada ya IMANI umezitoa wapi mkuu?……….. Hivi kwanini watu wa IMANI mnapenda kuforce unacho AMINI wewe ndio SAHIHI?

Nimetoa mfano, aliye mtengeneza Allah ndio aliutengeneza na Uislam
Kuukataa Uislam maana yake ni kumkataa Allah………. Wewe unatoa wapi uhalali wa kumkataa Mungu wa wenzako kupitia DINI na uka muhalalisha Mungu wako uliyemtengeneza wewe ambaye hataki DINI?

IMANI yoyote ile ikiwemo Dini, Mungu ni vitu ambavyo havitaki matumizi sahihi ya AKILI na ndio vinaongoza kuua independent thinking capacity
Wewe ulijuaje family tree yenu?
 
Wewe ulijuaje family tree yenu?
Acha mimi, hata babu yangu hajui vizazi vitano tu nyuma yake, anamjua babu yake tu, baba mzaa babu yake anamsikia sikia tu kwambali, wanyuma yake hanataarifa zake kabisaaa

Sivijui vizazi vyangu vitano vya nyuma, vizazi vyangu 10 mbele hawatajua lolote kuhusu mimi…….. sababu hilo sio lengo mama la MAISHA

Kikubwa kwenye maisha sio family tree……. Lengo kuu Ni kwamba umejikuta umezaliwa, utampambana kuishi as long as possible, utazaliana then unakufa………kwisha habari yako

Hapo utakapo jikuta umezaliwa ndio kwa asilimia kubwa patakufanya wewe UAMINI nini.
Mtoto aliyezaliwa na Rabi wa Kiyahudi pale Haifa Israel ana nafasi ndogo sana KUAMINI vinginevyo zaidi ya kuwa Myahudi………..same applied kwa atakaye zaliwa Gaza, Viunga vya Tehran na wazazi washiah, Pyangyong China, India kwa wahindu, Waadzabe Arusha nk nk

Mkuu Dunia ina mamiaka Dahali, hakuna anayejua huku nyuma kabla ya utunzaji kumbukumbu wa kudumu kuanza mambo yalikuaje……… kuna theories na Imani tu ilikuaje.

Binadamu ni social animals, social animals wote duniani wanaishi kwenye vikundi(jamii) na kufuata miongozo na taratibu ilikuepuka migogoro isiyo na lazima……. Na kwa msingi huo basi ni rahisi zaidi kwa kikundi cha jamii kua na imani moja ya Mungu na kuwa na taratibu za kufanya(dini) ili kumuadhimisha Mungu wao.
Ni ngumu kufikiri kwamba eti jamii fulani walianza kwa kila mmoja kuamini Mungu anavyojua yeye kuliko kufikiri walikua wanafanya hivyo kwa ummoja wao na taratibu maalumu kwa wote(ritual) kupitia viongozi wao ambao kwa sehemu kubwa ndio walikua watoa miongozo

Ndio maana nikaandika kwamba IMANI ya Mungu inatekelezeka zaidi kupitia DINI ingawaje wapo Tusio amini kabisa, wapo wanaotilia mashaka, wapo pia ambao wanaamini lakini hawavutiwi na DINI

Kukinzana na DINI ni kukinzana na asili ya binadamu kama social animal…….Kufanya mambo kwa utaratibu maalamu wa umoja
 
Mkuu Akili ya binadamu ni kama akili za viumbe wengine…… zinatofautiana uwezo tu
Binadamu ana uwezo wa juu sana kiakili
Huwezi kusema akili ya binadamu ni kama akili za viumbe wengine na hapo hapo unakiri kuwa binadamu ana uwezo wa juu sana wa akili.

Yaani kwa lugha rahisi maelezo yako yanakinzana.
 
Hakuna tofauti yoyote kati ya anaye anaye amini katika imani na asiye amini ila wote wana lengo mmoja wamejikuta wamezaliwa, watapambana kuendelea kua hai, watazaliana kisha watakufa………. IMANI haitawaongezea chochote wala haita punguza chochote labda uwe kiongozi wa kiimani na utumie sadaka kama means yako ya kipato( mapambano ya kuishi)
Huu ni uelewa wako. Na hii ndio inafanya tofauti kati ya wanyama (utambuzi) na mnyama mwenye busara (akili).
 
Imani haina tofauti na itikadi. Imani inakupa mwelekeo wa kusimamia masuala yanayohusu utawala usioonekana kwamba ndiyo unaotawala fikra na hisia kuhusu uwepo, uumbaji na yanayodhanika kujiri baada ya nafsi na roho kuachana na mwili. (Hii ni tafsiri yangu)

Dini, ni utaratibu uliobuniwa na unatumika kudhibiti aina ya imani ambayo mtu anapaswa kufuata. Dini inasajiliwa lakini Imani haisajiliki.

Basi nimeona wazimu sana kuwa mwanadamu amelazimisha Imani na Dini vifungamane na kwenda pamoja ilihali kimoja ni bangi kingine ni kitakatifu.

Haya, wanazuoni akina Mzito Kabwela na wengineo, mnaweza kunielimisha beyond hayo madhanifu yangu kwenye Imani na Dini?

UPDATE
wewe ukishaona kuna mambo mengi yapo tu hata binadam hajui yalifanyikaje jua IPO Nguvu yenye mamlaka zaidi ya chochote. We unaona jua lina toka Mashariki kwenda magharibi na hakuna wa kubadilisha hilo;

Wewe unaona kila siku watu wanazaliwa na kufa hata hujui, wanakwenda wapi...
Au pengine; wewe unakula chakula kina chakatwa hadi uchafu unatoka huoni maajabu
Wewe ukiamua kufanya kitu, miguu na mikono yako inaelewa unachotaka na kufuata maelekezo; huoni maajabu na mengine mengi

Ungekuwa umesoma Biology vizuri ukafuatilia utendaji kazi wa mwili wako; Ukaona grid ya umeme kwenye moyo; ungeamini kuna mtaalam kuliko hawa waote walipo duniani.
Utendaji kazi wa mwili wa mtu; ni muujiza kuliko hata miujiza mingine unayo ona huko...

Ili kuijuia hiyo Nguvu yenye mamlaka kuliko vyote; ndio hapo ikawepo elimu ya dini...
Kimsingi dini ni Elimu Inayotolewa kufundisha watu kutukuza ukuu wa hiyo Nguvu yenye mamlaka yote...
Sisi tuna amini kuwa, hiyo Nguvu ni Mungu mmoja tu mwenye mamlaka yote, ambaye hana mshirika, haja zaa wala hajazaliwa na hafanani na kitu chochote.
 
Sisi tuna amini kuwa, hiyo Nguvu ni Mungu mmoja tu mwenye mamlaka yote, ambaye hana mshirika, haja zaa wala hajazaliwa na hafanani na kitu chochote.
Binafsi naheshimu sana mtu anayetambua kua “ANA AMINI KUNA MUNGU”
 
Back
Top Bottom