Naomba mnipe ushauri wa sehemu gani nzuri na affordable ya kuweza kupata eneo zuri la kujenga makazi kwa ajili ya kuishi

Naomba mnipe ushauri wa sehemu gani nzuri na affordable ya kuweza kupata eneo zuri la kujenga makazi kwa ajili ya kuishi

Bunju kwenda mbele usithubutu Kuna matapeli wa viwanja kama wote hata ujitie mjuaji vipi utalizwa
Yani Bunju wanakutoa kamasi darisalama hii, basi wewe huwezi kuishi popote, hupaswi kutoa ushauri humu ndani.
 
Ndugu zangu hongereni kwa majukumu ya kujenga uchumi wenu kwa manufaa ya familia zenu bora.

Mimi naomba mnipe USHAURI wa sehemu gani nzuri na affordable ya kweza kupata eneo zuri la kujenga makazi kwa ajili ya kuishi mimi na familia yangu ambayo Mungu atanibariki hapo baadae.

KUSUDIO: ni kupata eneo lenye ukubwa kuanzia Sq. Mita : 900 - hadi 1200.
Naamini nikipata eneo la ukubwa huo naweza jenga nyumba nzuri ya kisasa na kuweka mazingira mazuri kwa ajili yangu na familia ambayo naamini Mungu atanibariki.
MAWAZO YA AWALI: Kabla sijapata USHAURI wenu nimewaza maeneo kama KIBAMBA, GOGONI na kwa mbali nilikuwa nawaza maeneo kama ya CHANIKA, VIKINDU, MWANDEGE.
NOTE; Sijawahi kuwa na interest hata kidogo na KIGAMBONI.

BAJETI YANGU: Kwa ajili ya huo uwanja ina range kuanzia Million 10 - 15.

Kwa kuwa JF ni kisima cha maarifa, na wengi mna uzoefu wa maisha ya Dar basi naombeni USHAURI wenu ambao utanifanya ndoto yangu iweze kutimia.

NATANGULIZA SHUKRANI ZANGU ZA DHATI KWENU NDUGU ZANGU.
Kibamba kiluvya, Hapo hujakosea. Usafir uhakika na soon kutakuwa hot cake. Hii barabara ya Morogoro road haina shida.

Huko chanika achana napo, kwanza mbali, Usafiri ishu, sio ustaarabuni, kama kumsuswa ikitokea hata miundo mbinu kuharibika it takes forever. Maji ya dawasco ni sehem chache utapata, Utaambiwa mbona wengine wanaishi, sijui hivi vile lakini kwa kiwaki.

Kibaha, na huo ukanda ulio utaja una angalau.
 
Kilwa road uchawi Sana utauza eneo lako achana nako huko hakufai utaja nikumbuka nenda morogoro road au bagamoyo road huko sijui mbagala kisemvule vikindu achana napo utakufa maskini
MOROGORO ROAD nenda kibaha huko Kuna kujenga barabara ya njia 6 to chalinze
 
Kilwa road uchawi Sana utauza eneo lako achana nako huko hakufai utaja nikumbuka nenda morogoro road au bagamoyo road huko sijui mbagala kisemvule vikindu achana napo utakufa maskini
MOROGORO ROAD nenda kibaha huko Kuna kujenga barabara ya njia 6 to chalinze
Asante sana kwa ushauri wako
 
Ndugu nakushuru sana kwa observation zako na mchango wako.

Kimsingi so far naishi mkoani LAKINI lengo kuu ni kuwa na makazi ya familia Bora Dar es salaam. Huku nipo kujitafuta kimaisha tu.
Mtazamo wangu wa awali ni kufuata mwelekeo wa Morogoro road 🛣️ ambapo hata ninapokuwa natoka mkoani yanilazimu kutumia Morogoro road.
Sina shuguli za kufanya Dar kwa sasa, na wala huyo partner bado hajapatikana huenda atapatikana hapo baadae but kikubwa makazi Bora na sehemu nzuri, partner akipatikana ata-adjust shuguli zake kulingana na makazi ambayo Mungu atakuwa amenibariki kuyajenga DSM.

ASANTE SANA MKUU 🙏
Umeshapata
 
Back
Top Bottom