Naomba msaada jinsi ya kusoma Mita ya maji (DUWASA)

donlucchese

JF-Expert Member
Joined
Mar 23, 2011
Posts
17,128
Reaction score
21,885
Salam wakuu,

Kama kichwa kinavyojieleza hapo juu, naomba msaada jinsi ya kusoma hizi Mita maana muda mwingine nahisi wananibambika bili.

Matumizi ya kawaida tu ya maji na hapo ni familia ya watu wanne tu lakini jana wamenitumia bili elfu thelathini.

Ningesema pengine labda kwakuwa nilipanda migomba ila tangu mvua zianze December migomba hatumwagilii tena. Naomba msaada wakuu!

Issue siyo kusoma Mita, unapaswa kujuwa bei ya maji ya per unit.

Kila tarehe ya usomi mita unaambiwa ili uhakiki, na bili ikitumwa inaonesha ni kutoka unit Fulani mpaka unit Fulani, sasa hapo unaibiwa vipi?

Ukitaka kuthibitisha kama Una simtak jaza maji kwenye simtak soma meter yako andika pembeni, yakiisha jaza tena andika pembeni usimtumie direct Bombay linaleta maji then mwisho wa mwezi utajuwa meter yako ulitumia unit ngapi.
 
Nashukuru mkuu japo simtank bado sijajaliwa. Issue ni kwamba hata ile sms hua wanasema usomaji uliopita ni unit kadhaa, usomaji wa sasa NI kadhaa hamna, wanaleta tu bill
 
Pia Kuna kipindi maji yanakuwa hayatoki wanafungua Bomba wanaacha wazi Ili yakitoka wasikie ule upepo nao unazungusha mita.... Ama anafungua maji anayaona. Yanafoka zaidi kuliko kutoka lakini anaendelea tu kuacha yanafoka weee yanatoka kidogo yanafokaaaa yanatoka kidogo nayo hiyo inakimbiza mita.... Na pia matumizi ya maji kila saa bombani ni Bora kuwa na vifaa vya maji unajaza unatumia yakiisha unajaza Tena sio matumizi mazuri kutumia maji mara Kwa mara Moja Kwa Moja kutoka bombani ... Kingine watoto na majirani kama anawarusu kutumia Bomba.....
 
Nashukuru mkuu japo simtank bado sijajaliwa. Issue ni kwamba hata ile sms hua wanasema usomaji uliopita ni unit kadhaa, usomaji wa sasa NI kadhaa hamna, wanaleta tu bill
Sasa soma hiyo bill lazima inaonesha unit ulizotumia, Anza kufuatilia mwenyewe.

Haiwezekani Mita yako inasoma upo kwenye unit 200 halafu bill isome upo unit 250 hapo unaweza hata kuwashtaki mahakamani.

Ila nyinyi ndio mtasababisha tuletewe Mita za Luku za maji sasa.

Kuna huduma post paid ina faida yake kuliko prepaid.
 
Pale kwenye meter usiache on Bila kulock, hizo meter hata ule upepo hakuna maji huwa zinarekodi.

Ukitaka kwenda sawa na watowa huduma za maji tumia tank, tank likijaa lock kwenye meter hakuna kuleta maji bombani.
 
Wewe soma hapo kwenye 00495 m3. Mfano mwezi ujao ikasoma 00500 m3 maana yake umetumia 5 m3. Kwa bei ya huku kwetu 1 m3 ni tshs 1772 au tshs 2000 kama utatumia 5 m3 au zaidi.
Sasa fanya hesabu Ile za kkk hazihitaji hata darasa.
 
Nashukuru mkuu!
 
Tarehe 08Jan24 walinitumia meseji kwamba bill iliyopita ni .00 (kumaanisha niliclear sidaiwi), Jana tarehe 31Jan24 sijaambiwa previous bill ni kiasi gani ila moja kwa moja kwamba nadaiwa shekeli 30,502/=
 
Acha uongo wewe ilikuwa 00 au 00000? Maana yake umetumia 495 m3? Hapo bili yako ni 495 *200 = 98000/- sasa hiyo 30000 kivipi? Au huko kwenu maji bei gani?
Kua basi mwerevu kidogo mkuu kabla ya kuprovoke
 
Nashukuru mkuu japo simtank bado sijajaliwa. Issue ni kwamba hata ile sms hua wanasema usomaji uliopita ni unit kadhaa, usomaji wa sasa NI kadhaa hamna, wanaleta tu bill
Lazima wakuambie usomaji uliopita na wa sasa kisha tofauti ule na huu ni uniti kadhaa sawa na shilingi kadhaa, hapo mmemaliziana.
 
O8Jan24 ilisoma hivi, halafu Jana kweli bili iwe elfu thelathini?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…