Naomba msaada jinsi ya kusoma Mita ya maji (DUWASA)

Naomba msaada jinsi ya kusoma Mita ya maji (DUWASA)

Ilikua 00 mkuu
Basi kalipe unit 495.
Though hizi ni units nyingi sana! Ulikuwa na ujenzi wowote? Una watoto ?Kuna umbali gani toka kwenye mita hadi kwenye nyumba?
Maji huwa yanakatika?
 
Acha uongo wewe ilikuwa 00 au 00000? Maana yake umetumia 495 m3? Hapo bili yako ni 495 *200 = 98000/- sasa hiyo 30000 kivipi? Au huko kwenu maji bei gani?
Kwann uzidishe na 200

Na kule juu umezidisha na 1772 au 2000
 
Basi kalipe unit 495.
Though hizi ni units nyingi sana! Ulikuwa na ujenzi wowote? Una watoto ?Kuna umbali gani toka kwenye mita hadi kwenye nyumba?
Maji huwa yanakatika?
Niliwapigia simu wakaniambia hizo 495 inamaanisha ni tangu wanifungie mita ambapo ni mwaka 2022 ndio nimetumia units hizo zote. Sasa leo nalipia halafu nataka nianze kufanya monitoring mwenyewe na ninunue vile vidude vya kufunga kwenye lock
 
Sasa soma hiyo bill lazima inaonesha unit ulizotumia, Anza kufuatilia mwenyewe.

Haiwezekani Mita yako inasoma upo kwenye unit 200 halafu bill isome upo unit 250 hapo unaweza hata kuwashtaki mahakamani.

Ila nyinyi ndio mtasababisha tuletewe Mita za Luku za maji sasa.

Kuna huduma post paid ina faida yake kuliko prepaid.
Hizo luku za maji zitakuwa more efficient kuliko utapeli unaofanyika sasa. Mtu akijiskia kukubambikia bill anakutwisha tu
 
Niliwapigia simu wakaniambia hizo 495 inamaanisha ni tangu wanifungie mita ambapo ni mwaka 2022 ndio nimetumia units hizo zote. Sasa leo nalipia halafu nataka nianze kufanya monitoring mwenyewe na ninunue vile vidude vya kufunga kwenye lock
Hapo sawa lakini monitoring huwezi kufanya mwenyewe labda kama unaishi mwenyewe. Monitoring inafanywa na wote wanaotumia hayo maji.
 
Pole mkuu huku kwetu wanajitahidi kutuma sms za kuhakiki unit zako na wanakuambia kama usomaji siyo sahihi uwapigie na ninajitahidi kweli kusoma mita yangu

Kwa mfano mpaka sana unit zangu zinasoma 84 zaidi ya miezi mitatu kwa hiyo bill yangu ni 0 maana ninajitahidi kwenda sawa na hii mvua ikinyesha tu nachota maji najaza kwenye matenki Dawasa nawasahau
 
Pia Kuna kipindi maji yanakuwa hayatoki wanafungua Bomba wanaacha wazi Ili yakitoka wasikie ule upepo nao unazungusha mita.... Ama anafungua maji anayaona. Yanafoka zaidi kuliko kutoka lakini anaendelea tu kuacha yanafoka weee yanatoka kidogo yanafokaaaa yanatoka kidogo nayo hiyo inakimbiza mita.... Na pia matumizi ya maji kila saa bombani ni Bora kuwa na vifaa vya maji unajaza unatumia yakiisha unajaza Tena sio matumizi mazuri kutumia maji mara Kwa mara Moja Kwa Moja kutoka bombani ... Kingine watoto na majirani kama anawarusu kutumia Bomba.....
Ushauri mzuri, ni vitu vidogo ila vinagarimu..mtu anaacha bomba wazi mita inasoma tu..au maji ya kujaza ndoo moja inachukua dakika 20, mita inasoma tu..

Hongera kwa ushauri wako
 
Niliwapigia simu wakaniambia hizo 495 inamaanisha ni tangu wanifungie mita ambapo ni mwaka 2022 ndio nimetumia units hizo zote. Sasa leo nalipia halafu nataka nianze kufanya monitoring mwenyewe na ninunue vile vidude vya kufunga kwenye lock
Nimesoma maelezo yako kuwa units 495 ni matumizi yako tangu mita ifungwe. Hiyo ni sawa.

Sasa mwezi uliopita ulilipa kiasi gani?

Kama hujawahi kulipa basi unatakiwa kulipa zaidi ya milioni moja. Lakini kwa kuwa bili uliyoletewa ni 30,000/= basi inaelekea huwa unalipa kila mwezi, hivyo ungeweka usomaji wa mita uliopita ungesaidiwa kirahisi.
 
Back
Top Bottom