Naomba msaada jinsi ya kusoma Mita ya maji (DUWASA)

Ilikua 00 mkuu
Basi kalipe unit 495.
Though hizi ni units nyingi sana! Ulikuwa na ujenzi wowote? Una watoto ?Kuna umbali gani toka kwenye mita hadi kwenye nyumba?
Maji huwa yanakatika?
 
Acha uongo wewe ilikuwa 00 au 00000? Maana yake umetumia 495 m3? Hapo bili yako ni 495 *200 = 98000/- sasa hiyo 30000 kivipi? Au huko kwenu maji bei gani?
Kwann uzidishe na 200

Na kule juu umezidisha na 1772 au 2000
 
Basi kalipe unit 495.
Though hizi ni units nyingi sana! Ulikuwa na ujenzi wowote? Una watoto ?Kuna umbali gani toka kwenye mita hadi kwenye nyumba?
Maji huwa yanakatika?
Niliwapigia simu wakaniambia hizo 495 inamaanisha ni tangu wanifungie mita ambapo ni mwaka 2022 ndio nimetumia units hizo zote. Sasa leo nalipia halafu nataka nianze kufanya monitoring mwenyewe na ninunue vile vidude vya kufunga kwenye lock
 
Hizo luku za maji zitakuwa more efficient kuliko utapeli unaofanyika sasa. Mtu akijiskia kukubambikia bill anakutwisha tu
 
Niliwapigia simu wakaniambia hizo 495 inamaanisha ni tangu wanifungie mita ambapo ni mwaka 2022 ndio nimetumia units hizo zote. Sasa leo nalipia halafu nataka nianze kufanya monitoring mwenyewe na ninunue vile vidude vya kufunga kwenye lock
Hapo sawa lakini monitoring huwezi kufanya mwenyewe labda kama unaishi mwenyewe. Monitoring inafanywa na wote wanaotumia hayo maji.
 
Pole mkuu huku kwetu wanajitahidi kutuma sms za kuhakiki unit zako na wanakuambia kama usomaji siyo sahihi uwapigie na ninajitahidi kweli kusoma mita yangu

Kwa mfano mpaka sana unit zangu zinasoma 84 zaidi ya miezi mitatu kwa hiyo bill yangu ni 0 maana ninajitahidi kwenda sawa na hii mvua ikinyesha tu nachota maji najaza kwenye matenki Dawasa nawasahau
 
Ushauri mzuri, ni vitu vidogo ila vinagarimu..mtu anaacha bomba wazi mita inasoma tu..au maji ya kujaza ndoo moja inachukua dakika 20, mita inasoma tu..

Hongera kwa ushauri wako
 
Niliwapigia simu wakaniambia hizo 495 inamaanisha ni tangu wanifungie mita ambapo ni mwaka 2022 ndio nimetumia units hizo zote. Sasa leo nalipia halafu nataka nianze kufanya monitoring mwenyewe na ninunue vile vidude vya kufunga kwenye lock
Nimesoma maelezo yako kuwa units 495 ni matumizi yako tangu mita ifungwe. Hiyo ni sawa.

Sasa mwezi uliopita ulilipa kiasi gani?

Kama hujawahi kulipa basi unatakiwa kulipa zaidi ya milioni moja. Lakini kwa kuwa bili uliyoletewa ni 30,000/= basi inaelekea huwa unalipa kila mwezi, hivyo ungeweka usomaji wa mita uliopita ungesaidiwa kirahisi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…