Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mshana na wewe unamaruweruwe,🤔Niko hapa nijuavyo mimi mtu akifa namba yake haipaswi kutumika na mwanafamilia yeyote tena! Hata mimi mtu akishakufa na nanba yake naifuta kwenye phone book yangu
Nina kisa kinachofanana na hicho kidogo..
Kuna bibi mmoja tulifahamiana katika mazingira ambayo nisingependa kuyaweka wazi hapa, nikawa na ukaribu naye kiasi cha kuniita mjukuu wake aliyepewa na Mungu .. Nikiri wazi alinisaidia kwa mengi sana na mimi pia hivyohivyo
Namba yake ya simu nimeikariri hata sasa! Lakini alipofariki 2012 niliifuta kwenye phone book yangu
Sasa mwezi uliopita ile namba ikanipigia.. Nikastuka sana lakini nikaipokea hakukuwa na majibu upande wa pili.. Nikiipiga ni kama inapokelewa lakini hakuna sauti.. Hiyo hali iliendelea karibia wiki nzima mpaka nilipoamua kuiblock
Nimeyakomesha. YamekomaMshana na wewe unamaruweruwe,[emoji848]
Wapo wenye maruweruwe😂Aisee nileteeeni mwamposa nileteeeni Mwamposaaaa nileteeni Mwamposaaaa
wafu hawajui neno loloteKama kichwa cha habari kinavyoeleza, ni jambo lililotushtua kama familia kutokana na uajabu wake.
Ipo hivi, siku ya juzi tar 19 majira ya saa sita kasoro usiku nikiwa nimelala fofofo, simu yangu ambayo ilikuwa kwenye 'vibration mode' ilikuwa ikiita.
Wife kwakuwa alikuwa bado hajalala akawa ananiamsha niipokee lakini kabla hajafanikiwa kuniamsha akashangazwa kuona namba iliyokuwa inanipigia ni namba yake mwenyewe ambayo anatumia kwenye simu yake na wakati huo simu yake akiwa nayo mkononi, cha kushangaza zaidi ni kuwa simu yake haikuwa na salio la kuweza kupiga wala kubeep na haikuwa inaonesha kama inapiga simu, lakini kwenye simu yangu inaonekana ni namba yake ndiyo inapiga, namba yake ambayo nimeisave vizuri kabisa.
Wife akaamua kupokea mwenyewe tu ili aone ni kitu gani. Hakukuwa na sauti yoyote iliyosikika na yeye pia hakuongea chochote. Akawa ameiskilizia mpaka sekunde ya 31 akakata.
Kwakuwa nilikuwa nimechoka sana wife hakutaka kuniamsha na badala yake akaja kunielezea kila kitu asubuhi ambapo iliingia habari nyingine ya kushangaza tena.
Mama yangu mzazi alimpigia simu wife kumuuliza kwanini alikuwa anampigia usiku wa manane, hii ikiwa na maana kuwa namba hii ya wife ilionekana ikimpigia mama yangu mzazi pia usiku ule ule hali ya kuwa haikuwa na salio na kwenye simu ya wife hakuna call history wala hakuna salio la kupiga wala kubeep.
Sasa kitu kinachochagiza wasiwasi kwenye hili ni kwamba namba hii anayotumia wife ni namba iliyokuwa ikitumiwa na marehemu bibi yangu mzaa mama kama namba ya akiba na ina usajili kamili wa marehemu bibi ambae alifariki mwaka jana.
Hapa ndo kidogo pamefanya tuwe na wasiwasi.
Mimi kichwani mpaka sasa nina maswali mawili, kwamba je inawezekana likawa ni swala la kimtandao? au ni jambo linalohusiana na mambo ya giza kutokana na kua namba hii ilikua ikitumiwa na marehemu bibi yangu?
Kiukweli nimeshindwa kabisa kuelewa mpaka sasa. Naombeni msaada wa mawazo yenu jamani kwa ambao huenda mnafahamu au mmewai kuona mambo kama haya.
[emoji28][emoji28]Kwahiyo unashauli sie tusio na namba za NIDA tupewe taraka??Hatuna namba ila upendo na utulivu tunao[emoji28]
Very Good!Nje ya mada mkuu, nakukumbusha tu kutumia namba ya mtu mwingine akiwa Hai au amekufa ni kosa kisheria!
watanganyika tunapenda kuhifadhi vitu chakavu bila sababu wengi wetu tuna vitu ambavyo tunavyo na hatuvitumii lakini tunaona fahari kuwa navyo. sasa fikiria huyu hata hajui kuwa kuendelea kutumia hiyo namba ni kinyume cha sheria na anaona sawa tu.Imetokeaje mkeo akarithi namba ya marehemu wakati hawana undugu?
Sina hamu na itel zamani kuna siku nipo kwenye ofisi kubwa hapa mjini posta nafanya presentation pale katikakati ya presentation nasikia vikelele vya mahaba mara vinaongezeka vinapungu..matatizo ya kutumia tecno,itel na infinix hayo.ujui jina lipo dublicate
Very good qestionImetokeaje mkeo akarithi namba ya marehemu wakati hawana undugu?