Tafadhali msaada kwa wenye kujua...halafu ni ipi kwa hapo ipo marketing
Dunia ya leo hakuna kozi yenye market, madakitari wako mitaani, maengeneer wako mitaani, Computer scince wapo mitaani. Kila sekta ina watu wana hang. Ushauri wangu hii kitu inaitwa tourism management kama hauna mjomba au baba ana kampuni achana nayo. Bora ufanye specialization huko kwenye tourism nenda NCT Fanya kozi ya food production ambapo unaweza kuchukuwa Ordinary Diploma in Culinary Arts, AU nenda Mweka soma wildlife management ya hapo.
Ushauri mwingine kuna industry ambayo watanzania wengi mmeisahau kabisa na hamjui kama ina exit lakini watu tunapiga hela nayo ni cooperate security. Soma kozi kama Business Admnistration, IT/Law enforcement baada ya hapo fanya kozi moja online google hii link
ISMI | Welcome to the CSMP Level 6 Diploma Fanya kozi hii Certified Security Management Professional (CSMP). Mitihani inafanyika British Council unatakiwa kuwa serious la sivyo utapoteza hela make hawana mchezo. Baada ya hiyo fanya mojawapo ya hizi , CSA, CISA, CISM, CISSP, CEH.
Achana na kozi za mlango mmoja kama hizo tourism, ualimu nk.
Siku moja utarudi kwenye huu uzi kunishukuru. Cha msingi tu uwe umepitia JKT na ukubali kuanzia chini kwenye haya makampuni makubwa ya security.