Wewe unapoteza muda wako bure. Najua shida yako ni kwamba uachwe kukatwa 2%. Kila idara ina chama chake cha wafanyakazi na hairuhusiwi kuwa na vyama viwili vya wafanyakazi idara moja. Kama umechoka na cwt nenda kasome sheria uungane na akina tundu lissu tls au jiunge na chama cha madaktari cha akina ulimboka.
Sijawahi kuona chama kinachofanya kazi Tanzania kama cwt na sijawahi kuona chama chenye maendeleo kama cwt na sijawahi kuona chama kinachopigwa mawe na wanachama wake kama cwt?.
Wana vitega uchumi vya adabu kila mkoa na wameanzisha benki ambayo tayari inafanya kazi wamebaki kusupplly matawi nchi nzima tu tena kwenye majengo yao si ya kupanga.
Hata nmb ni benki kubwa lakini haina asset kama za benki ama Cwt.
Haraka ya wanachama na uelewa mdogo wa members utakigharimu chama baadaye kwani uongozi si jambo jepesi.
Wakati ukifika hata wewe unayetamani kutoka utatamani urudi tena wakati ambapo meli itakua imengoa nanga. Mwisho utabaki kufa na uzazi wako.
Sent using
Jamii Forums mobile app