Naomba msaada namna ya kujitoa chama cha waalimu Tanzania (CWT)

Unachouliza si relevant na hoja iliyopo mezani. Hebu eleza tatizo lako mfano unaposema wewe ni kiongozi jibu likawa ndiyo ama hapana wewe unapata nini. Muwe na uwezo wa kujenga hoja siyo vioja.

Sent using Jamii Forums mobile app
Kama ndiyo naelewa wewe ni mmoja wa wachache mnaonufaika na hivi vyama ambavyo haviwasaidii wanachama wake.na zaidi ya hapo punguza povu jibu hoja kwa hoja hata kama unafikiri ni mbovu ijibu kwa kwa hoja

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nasikia Jamaa wezi sana hata ikitokea Mwalimu amepata tatizo akienda ofisin kwao hawana msaada nawanakutreat kama umeenda kuomba msaada kumbe kwa pesa yako ndio wananenepesha matumbo na kuhudumiwa ni haki yako.

Poleni Teachers a.k.a Sir's/Madam's

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Naomba msaada namna ya kujitoa chama cha waalim Tanzania.
Kujitoa CWT ni process fupi na isiyo na Usumbufu. Andika barua kwa Katibu wako wa Wilaya ukipitia kwa Mwajiri wako. Utatoka haraka sana. Hakuna haja ya kutoleana lugha za kuudhi ninazoziona humu. Ila take my word: huwezi kufikia retirement age kabla hujajutia uamuzi huu wa kujitoa!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kama ndiyo naelewa wewe ni mmoja wa wachache mnaonufaika na hivi vyama ambavyo haviwasaidii wanachama wake.na zaidi ya hapo punguza povu jibu hoja kwa hoja hata kama unafikiri ni mbovu ijibu kwa kwa hoja

Sent using Jamii Forums mobile app
Sijaona hoja wewe umedai uelekezwe namna ya kujitoa usikatwe umeambiwa huwezi jitoa bado unauliza nini tena. Wilaya yako ina uongozi umeshindwa kuwauliza wakusaidie mwalimu gani unaogopa hadi ofisi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tanzania kuna CWT Na CHAKAMWATA ,kusema hairuhusiwi vyama viwili kidogo ninapata shida kukuelewa
 
Kenya kuna vyama vingapi vya Walimu?
 
Wanachama wanafaidikaje na hizo assets?
 
Hv lile jengo yalipo makao makuu ya CWT pale Kinondoni karibu na Morocco ni mali ya CWT? Naomba kujuzwa hilo tu.
 
mkuu vitega uchumi vyote ivyo. je walimu wanapata mgawo wa uwekezaji wao?
 
kumbe wewe ni chizi usiyehusika? maumivu waachie wahusika.je walalamikia nini haswa ?kaa kimya hao madam na sirs waendelee na vinavyowahusu !
 
Tanzania kuna CWT Na CHAKAMWATA ,kusema hairuhusiwi vyama viwili kidogo ninapata shida kukuelewa
Chakamwata haina uwezo wa kuongea na mwajiri kwa kigezo cha members. Mwajiri huongea na chama chenye member wengi.
Kwa hiyo Cwt watakukata 2% kama ada ya uwakala na chakamwata watakukata1% kama ada ya uanachama so utakatwa 3%.Hiyo si sheria ya Cwt bali ya serikali. Nilishawahi tupia barua ya kisheria humu kwenye post hii ipo.
Ninachokiona hapa ni mgogoro wa kimaslahi. Kuna watu waliogombea wakashindwa hivyo wakajenga chuki na propaganda za uongo kuhusu Cwt mfano haikaguliwi, haitetei Mwakajoka ya walimu sasa mimi najiuliza toka imekuwepo chakamwata ni miaka zaidi ya saba hata ofisi wamepanga Uwamu saccos Uyole Mbeya na wanakusanya ada za walimu kila mwezi wanapeleka wapi.
Leo nchi nzima wakuu wa sekondari, wakuu smsingi, waratibu elimu kata wote wanalipwa posho ya madaraka si chini ya 200000/= hadi 250000/= nje ya mishahara yao. Mpiganiaji wa hilo jambo aliyefanikisha Mr Olouch amewekwa ndani mara kadhaa na sasa anahangaika na kesi ya kufukuzwa kazi kisa haki za walimu hiyo Chakamwata imewasaidia nini.
Leo mmepewa hisa na chama kupitia michango yenu ya kila mwezi sasa hiyo chakamwata nayo inawakata kama Cwt ni benki gani ilikowanunulia hisa kwa faida yenu.Au ina kitega uchumi gani kwa manufaa yenu angalau hata mtoke pale mlipopanga saccos Uyole mnakodaiwa kodi mkalipe.
Msidanganyike wala kudanganya watu kwani hata Mwenyekiti wa chakamwata anakatwa na Cwt ni Mwalimu mbeya vijijini na mara ya mwisho nimeona makato yake July 2016.Asidanganye watu kama haipendi Cwt akauze hisa alizopewa.
Tatizo la walimu wengi ni wakurupukaji hawatafiti mambo huingia kichwa kichwa na kuwaumiza mbeleni.
Cwt ilipofikia ni Lulu na mfano wa kuigwa nchini.
 
Uongooooooo mkubwa kuna walimu wamejitoa CWT wapo CHAKAMWATA Na wanakatwa asilimia moja.
 
Huyo Oluoch kafukuzwa kazi CWT hawajamtetea.Itakuwa mwalimu wa kawaida.CWT ni wezi Na Fitina nyingi plus rushwa
 
Unasikia tu, how far are you sure that you listen is true. Acheni kuamini mambo bila kuhakiki. Itachukua zaidi ya miaka 40 hiyo chakamwata kuifikia Cwt ya sasa now sijui miaka hiyo cwt nayo itakuwa wapi. Vijana tumieni akili kuwaza.
 
Uongooooooo mkubwa kuna walimu wamejitoa CWT wapo CHAKAMWATA Na wanakatwa asilimia moja.
Rudi kusoma nilichoandika uelewe. Najua hujui hata hiyo chakamwata ilikoanzia hata ofisi zao za makao makuu huzijui.
Wakati ukifika mtaiona chakamwata kama Desi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…