Naomba msaada namna ya kujitoa chama cha waalimu Tanzania (CWT)

Hivyo vitega uchumi vinawasaidiaje walimu ? Kujitoa inawezekana , hiko chama sio cha taalumu
 
Kwa hiyo hata wewe ukichaguliwa utabadilika maana unadai huwa mwanzoni wako vizuri lakini baadaye tunawabadilisha.
Sasa nakushauri gombea nafasi ni nyingi sana uza sera kwa hoja utachaguliwa.
Kulikuwa na baadhi ya makatibu wazembe wasiowatembelea wanachama na kujua kero zao wameonywa na wengine kupewa majukumu mengine yanayowafaa.
Ukweli cwt iko vizuri mkuu.
 
Hivyo vitega uchumi vinawasaidiaje walimu ? Kujitoa inawezekana , hiko chama sio cha taalumu
Hilo nimeshajibia tayari. Ukitaka mengine zaidi nenda kwa katibu wako wa chama atakusaidia zaidi huko ndiko utapata mapato na matumizi yote ikiwa mwakilishi hakuletei.
 
Siyo kila mtu ana karama ya kuongoza
 
Hao makatibu wa wilaya ni kama Miungu fulani.Nilishuhudia Katibu anawaingiza mjini walimu waliokuwa wanadai mishahara yao.Mwanzoni alianza nao sawa wakisapotiana.Alipofanikiwa kukaa kikao yeye Katibu,Afisa Elimu Na Mkurugenzi kilichofuata ni Katibu kuwatoroka walimu Na kuongeza ugumu katika kufuatilia suala lao.Walimu baada ya kuona CWT imeungana Na mwajiri wakakata shauri walimu wenyewe wakajiorganize wakaenda Hazina Dar wakafuatilia mambo yao,withini one month mambo yakawa super .Sasa walimu kama Hawa wataipenda CWT inayowahujumu?
 
CWT ijichunguze haya malalamiko ya walimu si bure kuna kitu hakipo sawa
 
Kuna mahali humu nimeandika jinsi chama kilivyopambana kuwawajibisha makatibu waliofanya usaliti kwa kuahidiwa vyeo na serikali wakiwasaliti walimu.
Naibu katibu mkuu Olouch ni moja kati ya waliofanya kazi hiyo ya kuwadhibiti makatibu hao wachache kama wapo na sasa unaona yaliyomkuta kwa kuwa yeye ni mwiba kwa chama.
Usaliti upo mahali pote what's needed is to be against totally kwa kuondoa msaliti.
Ikiwa yesu mwenyewe alisalitiwa itashindikanaje watusaliti chama kwa vyeo na pesa.
Tuko vizuri kuwabana kwa njia nyingi tatizo mkimjua mnaweka siri. Akishindwa katibu wa wilaya vuta waya mpigie wa mkoa naye akizingua vuta waya piga makao makuu kwa katibu mkuu.
 
Hivi Email zenu Huwa mnajibu?Kupiga simu kwenye kituo chetu sidhani kama kuna mtu kafanya Ila Email Barua watu wameandika sana tu.Je Huwa mnajibu?
 
Kweli wewe mjini chai, umenichekesha sina mbavu mimi daaaah una vituko mpaka hunogi wewe[emoji23][emoji23]
Ni kweli Mkuu MJINI KUNOGA CHAI.......................Ingawa wengine kama wewe huona HAINOGI...................!!!!!
 
Hivi Email zenu Huwa mnajibu?Kupiga simu kwenye kituo chetu sidhani kama kuna mtu kafanya Ila Email Barua watu wameandika sana tu.Je Huwa mnajibu?
Super Sub Steve acha kuhangaika na email vuta waya ongea na mhusika moja kwa moja. Faida yake atakuuliza maswali kadhaa, atajua ulipo, atahitaji evidence kama unazo, atapanga ziara elekezi huko uliko nawe utapata majibu mazuri na kwa wakati.
 
Ainisha hayo matatizo.................!!!
Mkuu hapa hatushindani Ila nimesema CWT ijichunguze kuna sehemu HUENDA hapapo sawa.
Sasa kama CWT hawana kawaida ya kufanya Tathmini Na kuona kila wanachofanya ni perfect akitokea mtu mwenye ushawishi akaweza kuweka ushawishi mzuri kuwa CWT ni cha ovyo cjui kama huo muda wa kuuliza kuwa ainisha matatizo utakwepo.Sana sana utaanza kujitetea kuwa CWT ipo vizuri kitu ambacho kitakuwa ni too late.

[HASHTAG]#Swali[/HASHTAG] Chonganishi nini maoni yako kwenye uongozi mpya ulioingia madarakani? Maana kuna mtu aliwekwa kwanza lock up ili uchaguzi upite.Mwisho akaachiwa Bila kufunguliwa mashtaka
 
Kwanza kabisa sipo kwa ajili ya kushindana......wewe ni wale wale nathibitisha hili kwenye hiyo Tag yako.........Toeni maoni viongozi wayashughulikie......Uchaguzi umepita Mnatafuta nini.....? kuweni wavumilivu SOOON ''mtashiba''..........
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…