Naomba msaada namna ya kujitoa chama cha waalimu Tanzania (CWT)

Tumezoea togwa hiyo chai inaunguza
Kitu hiki mkuu karibu sumbawanga.
Ruksa kutemea Mate........nadhani hii kitu inaitwa RUBISA kama sijakosea.......Ukitoka hapo unakwenda kupata kitu kinaitwa PINGU..................

MJINI KUNOGA CHAI.........!!!
 
Kwanza kabisa sipo kwa ajili ya kushindana......wewe ni wale wale nathibitisha hili kwenye hiyo Tag yako.........Toeni maoni viongozi wayashughulikie......Uchaguzi umepita Mnatafuta nini.....? kuweni wavumilivu SOOON ''mtashiba''..........
Hayo majibu ya wewe ni wale wale tumeyazoea kutoka Viongozi wa CWT.Kwa akili yako unafikiri maoni hayajawahi tolewa? unafikiri mpaka mjadala umefika hapa watu wanafikiria kujitoa unafikiri watu hawajawahi kutoa maoni?
Maoni yametolewa sana tu Na kujibiwa wakati mwingine kwa jeuri wakati mwingine kwa maneno matamu yasiyo Na utekelezaji.Sasa wewe unataka maoni gani badala ya kujiuliza tatizo liko wapi unasema tutoe maoni ,maoni gani tena wakati watu wametoa maoni mpaka imeshafika point watu hawaoni tena umuhimu wa kutoa maoni isipokuwa kujitoa?
CWT ndiyo wanapaswa kujiuliza shida ni nini? Maoni yalishatolewa mengi mno.Naona mnatumia mbinu ya kudelay.CWT Haina tofauti Na Serikali iliyojificha kwenye mwavuli wa uhakiki.CWT imejificha kwenye mwavuli wa toeni maoni yatafanyiwa kazi.Na soon mtaneemeka.Hizo story ni za miaka nenda rudi tunazisikia.

Endeleeni kusema we ni wale wale baada ya kushiba hela zetu Za michango
 
Naona umeandika kwa uchungu Mkubwa sana, ila nina neno moja tu la kukuambia kwa sasa ya kuwa kama wewe ni Muumini wa DINI basi juwa ya kuwa HAKUNA IBADA NGUMU KAMA SUBIRA......Mvumilivu hula Mbivu................ wote COOL DOWN.....Uongozi una muda Mfupi sana tangu uingie Madarakani kuna Mambo mazuri yanaendelea Baina ya CHAMA(CWT) na Serikali..........!!!! sasa kuanika kwenye Mitandao Kizaliwe nini? je ni kupanda CHUKI, KUCHONGANISHA, NK.............???

''UNAWEZA KUMTETEA MTU THEN HUYO HUYO AKAKUUA..................!!!!''
 
Serikali inapoingiza mtu wake then akawepo mwingine ambaye yupo kwa maslahi ya walimu figisu huwekwa.
Hiyo si cwt pekee angalia yaliyotokea uchaguzi wa rais TLS Tundu lissu aliwekwa ndani vizuizi kibao mpaka akatoka dakika za majeruhi.
Ikiwa kwa wanasheria wanaoishi kwa kuziishi sheria inakuwa hivyo vuta picha cwt.
Olouch kaibana serikali kwa hoja nzito wakaona isiwe kesi wamnyime kibali cha miaka mitano arudi kufundisha kwa kisingizio kuwa walimu wa sayansi ni wachache alipowagomea kwa hoja akapewa barua ya kufukuzwa kazi.
Huyo ni kiongozi mkuu wa chama imagine wewe ingekuwaje.
Dunia ni mapambano, figisu zipo tena kubwa.
 
Siku kiongozi wa CWT akiweza kutoa time frame,kwa mfano aweke ahadi hii,
"UKIONA MPAKA TAREHE 24/6/2018 HAKUNA MAMBO MAZURI BASI WALIMU WOTE JITOENI CWT" Ikiwekwa ahadi kama hiyo naweza kuwa Na subira.Ila ikiwekwa ahadi Za kisiasa kuwa endeleeni kuwa Na subira kuna siku mambo mazuri yatakuja kamwe sitaamini.
 
Kwa maneno mengine CWT wapambanaji ni wachache mno.Na kweli wote hawawezi kuwa wabovu.Lazima atakwepo mzuri.Sasa Hawa waliopo nadhani ndio serikali inawapenda.Hapo ndio pa kuunganisha Nukta
 
Kwa maneno mengine CWT wapambanaji ni wachache mno.Na kweli wote hawawezi kuwa wabovu.Lazima atakwepo mzuri.Sasa Hawa waliopo nadhani ndio serikali inawapenda.Hapo ndio pa kuunganisha Nukta
Kuna vyama serikali ilishabana wote hakuna wa kufurukuta wala huwezi kusikia wametoa notisi yoyote kwa serikali mfano wa serikali za mitaa Talgwu.
Si kwamba wazuri hawapo tatizo ni pale mtu anapoona vitisho ni vizito kwake. Chukulia mfano wa Ulimboka Dr.
 
''Mwalimu'' Punguza ''kengele'' zilizopo akilini mwako unganisha NUKTA.......Mazuri yaja muda si mrefu........
 
Cwt ni tawi la chama cha mapinduzi, ningeshauri uwasiliane na chakubanga atakupa utaratibu jinsi ya kujitoa, hongera kwa kuanza kujitambua!
 
ukweli walimu wengi awana taarifa ya mengi uliyoyaeleza kinaonekana ni kama chama cha wachache na mgao sio lazima yawe mamilioni ni kile kinachopatikana ndio kinagawiwa.
 
Acha kutetea ujinga hata kama wewe ni mnufaika. Wanachama hawalipendi hilo li chama lenu. Mnawakata watu wakipata matatizo mnabaki kuwazungusha tu.
 
Umeongea vyema sana mzee nirudi hapo uliposema benki ulisha wahi nunua hisa katika benki na ukawa mwanahisa kisha usiitwe hata katika kikao kimoja cha wanahisa kwa miaka sita mfululizo?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…