Naomba Msaada: Ushauri, Kazi, Mtaji, au Vifaa vya Kusikilizia

Naomba Msaada: Ushauri, Kazi, Mtaji, au Vifaa vya Kusikilizia

ALENI WAKALA

Member
Joined
Oct 31, 2023
Posts
33
Reaction score
28
Habari wanajamii,
Naitwa Allen, Samahani Kwa usumbufu, natambua mna mambo mengi ya kufanya ila kwa MDA wako umeamua kupitia Uzi huu🙏🏿,
Napitia changamoto ya Usikivu hafifu Kwa takribani miaka mitano (5) hali ambayo imeathiri sana maisha yangu ya kila siku. Nimezunguka HOSPITALI tatu (3) vipimo vinaonesha tatizo lilelile (hearing loss at first stage or mild level) Daktar alinishauri kutumia hearing aids (vifaa vya kusikilizia). Kwa Bahati nzuri Nilipata msaada wa vifaa vya kusikilizia kutoka Hospitali ya Tumbi, lakini vifaa hivyo havijatatua changamoto yangu. Vinapiga makelele na kufanya iwe vigumu kutambua sauti kwa usahihi, jambo ambalo limeongeza ugumu wa kushirikiana kijamii na kuonyesha uwezo wangu nilionao.

Pamoja na changamoto hii, nimehitimu chuo, Shahada ya awali ya Utawala WA umma (PUBLIC ADMINISTRATION) Pia Nina Computer Skills kwani nimebahatika kwenda mafunzo ya computer.

Ndugu, Wana JF Naomba msaada katika maeneo yafuatayo:
Kazi ya kuajiriwa: Naomba KAZI yoyote isiyoathriwa na Usikivu Ikiwezekana, kazi inayohusiana na taaluma yangu au nafasi nyingine yoyote. NIPO TIYARI 🙏🏿
Mtaji wa kujiajiri: Mbali na kuajiliwa Nina ndoto ya kujiajiri kwa kuanzisha biashara ndogondogo inayohitaji mtaji mdogo. biashara ninayoweza kufanya ni pamoja na Kuuza vyombo vya ndani, Kuuza mishikaki (nyama choma, Vidali-nyama ya kukua) Na Kuuza matunda.
Vifaa bora vya kusikilizia: Vifaa vya kisasa zaidi ambavyo vinaweza kusaidia kutatua changamoto hii ya Usikivu na kunipa nafasi ya kuimarisha mawasiliano yangu.
Ushauri wa kitaalamu: Mawazo na mbinu za kushinda changamoto hizi na kuimarisha mustakabali wangu wa maisha.

Naamini kuna wanajamii wenye uzoefu, maarifa, au hata fursa zinazoweza kunisaidia kupiga hatua mbele. Msaada wenu, iwe wa hali au mali, utakuwa wa thamani kubwa katika maisha yangu. Natumaini ujumbe huu utawafikia wale wanaoweza kunisaidia kwa njia yoyote. mawasiliano 0624513983 (usipige tuma ujumbe Wa maandishi)
NATANGULIZA SHUKRANI 🙏🏿🙏🏿.
 

Attachments

  • PXL_20241206_173442604.PORTRAIT.jpg
    PXL_20241206_173442604.PORTRAIT.jpg
    263.3 KB · Views: 5
  • PXL_20241206_173436307.PORTRAIT.jpg
    PXL_20241206_173436307.PORTRAIT.jpg
    262.3 KB · Views: 5
Back
Top Bottom