Naomba msaada wa kifedha nilipie pango. Mwenye nyumba kaja kutoa vitu

Naomba msaada wa kifedha nilipie pango. Mwenye nyumba kaja kutoa vitu

Nipo Nala leta hiyo laki na nusu uishi kwangu Nina chimba kipo free kina Kila kitu. Joo uishi usianze kusumbua watu humu...nitafute pm nikuelekeze nilipo uje unione

Sent from my TECNO B1f using JamiiForums mobile app
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] daaah vijana akili mbovu kweli ninyi
 
Kama unasoma DECA na upo Nala njoo Nala Park saa 10:00 jioni hii na uje na Kitambulisho chako cha Chuo nihakiki,nitakuongezea tsh 10,000
 
Mungu akubariki sana, maisha ni safari ukikuwa utaijuwa dunia.
Kuna wazazi wengine hata hilo shamba la kuuza hawana. Yaani hawana chochote cha kuuza. Kuna watu wanaweza kukaa miezi bila kula nyama na siyo kwamba ni ma-baniani, la hasha. Hawana uwezo wa kuipata. Hii dunia ni kubwa na tunatofautiana. Nilipokuwa mdogo kwenye miaka 18 hivi hakuna watu niliokuwa nawakejeli kama ombaomba. Baada ya kukua na kupata busara nimekuwa najilaumu kweli nikijiona nililikuwa mjinga.
 
Kwa kujibu hoja zako ambazo utaona zitakuondolea shaka kama si utapeli
Habar wa wakuu, heri ya mei mosi.

Mi nimekuja hapa kuomba msaada wenu , ninaashida ya shs 100,000/= , nikiasi cha pesa kilicho pungua kwenye kodi ya chumba nacho kaa, maana leo mwenye nyumba kajakutaka kutoa vitu vyangu , nikamwomba anivumilie mpaka kesho asubuh ili nimtafutie pesa yake

Ni mwanafunz wa chuo cha afya hapa Dodoma, nimejaribu kupambania kupata hela ya kulipa kodi nimepata nusu ya deni ninakiasi cha tshs 150000, bado hiyo laki moja,

Kwa upande wa mzazi kwa sasa siwezi mtegemea maana ameyumba kiuchumi, hata kumwelezea shida zangu naona ni kumwongezea mawazo tu, naomben msaada wenu tafadhali

Natumain hapa JF naweza pata msaada, natanguliza shukran zangu za dhati kwenu

Kwa chochote kile mawasiliano
0655680282
Aisee, Pole kwa masaibu yaliyokupata. Nakushauri hivi:
1. Endelea kuomba msaada
2. Omba chuoni dharura ya siku 10 na Hapo Dom wapo mafundi wengi sana wa Ujenzi nyumba wanatafuta sana saidia Fundi na kwa siku 1 hulipa cash 10,000/= hadi 15,000/=
 
Hutakiwi kumuonea huruma mzazi wako. Maana hili ni jukumu lake kukusomesha na kukulea mpaka pale utakapo jitegemea!
Wewe muongezee tu mawazo ili akili imkae sawa.


Ifikie wakati tuishi maisha kama ya Wazungu. Haya masuala ya kufyatua tu, halafu watoto wanakuja kuteseka na kusumbua watu wengine hayana tija hata kidogo.

Samahani sana mtoto/mdogo wangu 🙏 kama nitakukwaza kwa haya maneno yangu.
Huwezi jua nini kimejiri kwa wazazi wake,maisha hayana mwenyewe.
Dunia duara,msaidie kama una nafasi.
 
View attachment 2207254
HUYU KIJANA NI OMBA OMBA SANA MPAKA KWENYE KUBETI KULE ANAOMBA SANA HELA.

NA ANA URAIBU NA KAMARI. KUWENI.MAKINI SANA
View attachment 2207255
Hela zake anazielekeza huku. Kuweni makini sana
Bora hata Mzee wa kufukua makaburi umekuja kutusaidia. Maana sisi wengine tumejaribu kujenga hoja humu, lakini tumeishia tu kutukanwa na watu wanao jiona wana akili nyingi vichwani mwao, kumbe ni mapoyoyo tu.
 
Inbox yako imefungwa
Sijafunga inbox yangu, wewe tuma namba mimi nitaongea naye, nitampa gurentee ya kulipwa pesa yake, lakini hakikisha maelezo yako ni kweli tupu ili usaidiwe na uache michezo ya kamari.

Hapa JF watu wakiingia kwenye id yako na kufanya screening ya post zako kama ni mpuuzi fulani tu huwezi kusaidia.

Nakuandika haya wewe ni sawa na mtoto wangu wa kumzaa nimeingiwa na huruma ya mzazi hata mimi nisingependa watoto wangu wapitie haya kama umetueleza kweli tupu.

Kama unachotuambia hapa ni kweli tupu utalipiwa hiyo pesa inayotakiwa.
 
Mwanafunzi unapewa boom la shilingi Elfu kumi kwa siku (kwa mwezi laki tatu), sasa umeshindwaje kulipa elfu 40 kwa mwezi?

Yaani wanachuo wenzako wote na majirani wameshindwa kukukopesha laki moja hapo ulipo mpaka uje huku mitandaoni (ambapo hatujuani) kuomb msaada?

Naona una shida kubwa zaidi kifikra na kitabia.
 
Bora hata Mzee wa kufukua makaburi umekuja kutusaidia. Maana sisi wengine tumejaribu kujenga hoja humu, lakini tumeishia tu kutukanwa na watu wanao jiona wana akili nyingi vichwani mwao, kumbe ni mapoyoyo tu.
Wengine humu tunasimama kama wazazi kuwapa miongozo hawa watoto, bado wapo kwenye foolish age kukosea kupo ni sehemu ya kujifunza.

Cha muhimu na msingi je maelezo yake ni kweli?

Dhiki za maisha ndio zinawapeleka vijana kujaribu bahati zao kwenye kubet, si busara kuwahukumu watoto badala ya kuwaekekeza jema na baya.

Hawa vijana wa sasa wanakwenda chuoni akili bado hazijakomaa, mimi nakumbuka kipindi naanza form one kuna tuliowakuta form two, three na four ni wakubwa sana wananyowa ndevu kabisa, mimi nakumbuka wapo tuliokuwa tunawaamkia na hata head Master alikuwa anawatreat tofauti ni watu wazima na akili zao kabisa.

Sasa usishangae Graduate wa leo kichwani hamna kitu, kuna transformation ya kizazi.
 
Back
Top Bottom