Naomba msaada wa kuanzisha mradi huu

Tutoke jamiiforum tujuane nje ya hapa kama wpo walioomba msaada kama ilivyo kwangu tusisite kusaidia pale panapokwa na ukweili na tukemee pale palipo na udanganyifu.
Na mimi nilipata hilo tatizo mwaka 2000,lakini nipo tofauti sana,sijawahi kuomba msaada,huwa naona fedhea sana,ninajiamini sana,nime learn self defense in advance,nafanya vitu kwa upekee sana,ninaheshimika,pia ninaogopwa sana! Nina sauti kwa maana ninaweza kutoa mawazo sehemu na yakafuatwa,nina familia imara, nyumba nk.sijioni kama nina mapungufu,sema huwa nawaonea huruma wanaonionea huruma pia, hali hii ilioonitokea ilinipa ujasiri wa kutohofia chochote,sasa wewe unalialia,nakuchoraa tu,aisee,sijaajiliwa,mission town tu!
 
Sasa ungeumwa figo,kansa ,au macho usione. Tena huwa najisemea bora mungu alichagua masikio aisee,yangekuwa macho ingekuwa habari nyingine
 
Kaka nashukuru kwa ushauri na busara zako.

Napenda sana kupata hizo kazi ulizozitaja na si hizo tu bali hata udobi,mzoa taka,usafi n.k nazitafta sana lakin vile watu huamin hivi vibrua vya chini vipo mtaai so watu tunazikimbia sio kweli mkuu,maisha haya fundi ujenzi anamchukua mwanae mtoto wa shangazi na mdogo wake yani hazipo bwerere kama watu tunavyoweza kudhan

Nimeeleza pia sababu za kuomba msaada ni mtazamo wa jamii kwetu wenye changamoto za kasoro za ulemavu,kwa mfano niliomba kazi ya usafi katika hospitali moja ya kanisa wahusika walinitukana kisa tu ni mlemavu kbaya zaid wakiwemo masista!,tukio jingne niliambiwa wew nenda kwenu kwani huli au haunyi sisi hapa hatuajiri viziwi,tukio jingne niliambiwa nisepe coz viziwi hwana akili timamu n kesi zingine kama hizo nyingi tu

Kwa sasa wanaohitaji hivyo vibarua na ajira zingne ni wengi na hawana changamoto ya ulemavu wowote na bado wanakosa pia unaweza vuta picha hapo! Sisi wenye changamoto tunapta ugumu mara 10 zaidi ya hawa walo wazima na mwisho wa siku wananufaika wao zaidi na ndio maana nimeomba msaada mazingira si rfiki kwangu napambana sana naagaika sana bro napenda sanakazi halali tatizo ni kuipata na kulingana nasa scale ya mtaji huo nilioomba laiti ningekua na kibarua mbona ningeshaanza mradi kaka

Hayo ni mambo yanayonifany niombe msaada
 
Mkuu kwanini usinipe mwenzio maujanja nahangaika mno mwenzio bila mafanikio dah
 
M
Sasa ungeumwa figo,kansa ,au macho usione. Tena huwa najisemea bora mungu alichagua masikio aisee,yangekuwa macho ingekuwa habari nyingine
Mkuu naomba usinidharau kwa maamuzi niiyochukua tafadhali nisaidie mwenzio napata tabu sana
 
Hiyo hali chukulia ni changamoto tu,usitafute watu,fanya watu wakutafute wewe,ona vitu ambavyo wengine hawawezi kuviona, mimi hali iliponitokea uamuzi mgumu wa kwanza kabisa niliacha chuo,niliona mambo yameshakuwa mengi,hii vita mpya ngoja nibadili strategy! Ingawa mzazi hakukubali,nilimwambia this is war!! Let me get me!!
 
Mkuu wazazi wako walikuwa na sshughuli gani wakati unaacha chuo na baada ya kuacha chuo ukafanyaje?
 
Mkuu wazazi wako walikuwa na sshughuli gani wakati unaacha chuo na baada ya kuacha chuo ukafanyaje?
Mkuu hiyo ni vita yako! Haijalishi wazazi wako wana shughuli gani? Kiufupi nimelelewa single mother,my mom...she is fighter too.ni story ndefu kukueleza nimefanyaje, kiufupi badili kwanza mind set yako,kuwa mpambanaji haswa,fanya kitu kwa ufanisi mara mbili ya unaodhani wamekamilika, ngoja nikupe mfano tu,niliwahi kwenda mkoa fulani kimahangaiko,sifahamiki huko,siku moja. Nikaamua kwenda mazoezini (mpirani) nikapangwa no 10, na sikuwaaambia tatizo nililonalo, sasa basi zile dakika 45 za kwanza mambo niliyofanya yalishangaza watu wengi,niliupiga mpira wa kipekee sana, sasa half time,watu wananizunguka kia mtu anataka anione kwa ukaribu,katika maongezi ndio nikawaambia hali yangu,kitu kilichowashangaza wengi,hawakuamini, kwahiyo hatua ya kwanza jipe deni la kufanikiwa kuzidi watu unaowaona wewe wamekamilika.
 


unaniinspire balaa...
 
Ushauri wako ni mzuri pengine aufanyie kazi, laki kwa sasa kama kijana unapambana hasa possibility ipo kubwa ya kuipata, that is one, lakini kama alivyosema mtoa mada kuna shule anajitolea ingekuwa vyema akaenda apo akaongea na Mwalimu mkuu na walimu wengine bahadhi yao wanaweza kumuelewa, kama itashindikana apo aache biashara ya kujitolea vyeti aweke kwenye begi kwanza apambane mtaani au uko vijijini hata kufanya vibarua, dunia haitaki watu dhaifu, kujishusha ili upate sympathy ya watu sometimes ni kujidhalilisha bure. Sorry for saying this πŸ™πŸ™πŸ™
 

Mkuu naona bado hujanielewa.
Nimekushauri vitu viwili cha kwanza nimekwambia itoe io kasumba ya kuomba msaada kwa kila jambo kichwani mwako ni mbaya mno na itaendelea kukutafuna masisha yako yote.
Inavyoonekana wewe ni mtu wa kulaumu sana jamii inayokuzunguka pasipo kujua matokeo makuu kwenye maisha yetu ni results za matendo yetu wenyewe. Bado hujabadilika kwenye ilo wacha kupenda kutegemea misaada kutoka kwa watu utakuja angukia pua maisha ni vita inakupasa kupambana.
Nimekupa mfano wa saidia fundi naona bado unalalamika mno unataka sijui mpaka upewe kazi kabisa acha uo ujinga kwenye bongo wako unapotea, nimekupa huo mfano kwa sababu nipo kwenye sector ya ujenzi site byingi ukiwai asubui na mapema ukipanga foleni hakuna atakaekuzuia usipangiwe kazi na jion kupokea ujira wako hata kama unekuja mpya tatizo lako naona wewe ni mbishi na unadirect kilakitu upewe tu msaada.

Kitu cha pili nimekushsuri uache kutafta huruma kutoka kwa watu kwa uo ulemavu wako naona bado hujanielewa. Unautumia uo ulemavu wako ili kiwe chanzo cha wewe kupata misaada kwa watu hio sio sawa tatizo lenu walemavu mmekuwa hamtaki kujishughulisha kwenye mambo kwa asilimia 100 mkiamini katika kuonewa hutuma na watanzania. Io kasumba itoe kichwani mwako naona bado unarudiarudia tu hapa ooh sijui nimetukanwa ooh sijui nimenyimwa iki kisa ni mlemavu nk ili watu humu wakuonee huruma acha kutumia uo ulemavu wako kama sababu ya wewe kupata kitu piga kazi dogo wewe bado kijana mdogo watu wametoka mbali sana pasipo kulialia na kuomba misaada kila mda.
Narudia tena badilika maisha ni kama vita ukiendelea hivi ata leo ukiipata io kilo moja kesho utapata tatizo lingine utakimbilia tena humu kuomba msaada nk nk


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
mkuu nashindwa kukuelewa maanaproud zako bado hazinipi mwanga kabisa,

Pia najitambua sana na najiheshimu pia nachukia kuonekana inferior

Nahitaji kujua baada ya kuacha chuo ulifanyje? Mimi nimemaliza chuo nipe mbinu ulianzaje!
 
Nashukuru kwa ushauri na mungu akubariki
 
mkuu nashindwa kukuelewa maanaproud zako bado hazinipi mwanga kabisa,

Pia najitambua sana na najiheshimu pia nachukia kuonekana inferior

Nahitaji kujua baada ya kuacha chuo ulifanyje? Mimi nimemaliza chuo nipe mbinu ulianzaje!


Hapa kuna m1 anafikiria mbinguni mwingine anafikiria ardhini...unaweza usimuelewe kwa sasa..!
 
No need to say sorry bro,hapa napojitolea niliwaambia hilo so they all know na huwa siulizwi why too late pale napofika shuleni saa tatu kwa sababu wanaju simudu nauli kila siku hutembea kwa mguu 1.5 km kwenda na kurudi

Laiti mtaani ningekua na vibarua hivi unadhani ningeendelea kujitolea? Ningekua na kazi haa ya kuearn 2000kwa siku ningesema ahsante mungu,sina mengi ya kusema tena acha ninywe kikombe hiki kichungu nilichopangiwa hapa duniani kiumbe mzembe na dhaifu kama mimi
 
mkuu nashindwa kukuelewa maanaproud zako bado hazinipi mwanga kabisa,

Pia najitambua sana na najiheshimu pia nachukia kuonekana inferior

Nahitaji kujua baada ya kuacha chuo ulifanyje? Mimi nimemaliza chuo nipe mbinu ulianzaje!
@mcgregor kakushauri utafute sait za ujenzi kusaidia fundi,fanya hiyo kazi huku ukijifunza ufundi,(wakati huo unalipwa mshahara wa fundi saidia) ukifanikiwa kujua ufundi jichanganye kwenye kampuni yoyote ya ujenzi,fanya kazi zako kwa ufanisi mara mbili ya wenzio na kwa spidi nzuri,injinia ataziona kazi zako nzuri,itapelekea upande cheo ,utakuwa msimamizi (foremen). Hapo kupiga milioni mbili tatu ni kawaida sana.but inachukuwa muda na jasho jingi, ndio maana maisha ni vita,faida ni kwamba,fundi hanyanyaswi,kazi zako zinajieleza, nadhani umenielewa kidogo,si lazima upitie njia nilizopitia mimi.
 
Asante sana
 
pole sana...usijiskie mpweke
I'm totaly heart brocken,im so sad i blame my self why didn't i notice this early? I was only just trying to employ my self instead it looked like i prefer myself to pass through hard time,no way i have to pass through this we can't know if it is my destiny, then let it be..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…