Naomba msaada wa kunichagulia sofa zuri kati ya izi

cold water

JF-Expert Member
Joined
Oct 6, 2021
Posts
238
Reaction score
954
Naomba kunichagulia sofa nzuri nataka kununua,na kama una lako zuri zaidi,naomba utume picha kama nitalipenda nitapeleka order kwa fundi.

Kingine naomba kuuliza kama miguu ya sofa hizi inadumu? Nina wasiwasi na kuharibika miguu yake, yaani iyo miguu ya sofa. Nasoma comments zenu.....

Asante.

 
MIMI naenda na Namba 1 kwa sababu zangu binafsi napenda kugeuza Sofa kitanda sasa hio Namba 2 nitalalaje hapo na urefu huu? Kichwa changu nitaweka wapi hapo hadi niweke foronya? Namba 1 limekaa Safi sana ingawa material yake ndio yanaonekana km ya kizee fulani hivi hata muundo wake ni wa kizeezee fulani hivi
 
Sina uchaguzi hapo. Kama huna hela ya kutosha nunua sofa plain zenye material iliyonyooka, chukua ngozi ile ngumu achana na materials zinaitwaje sijui hizo za kuteleza. Sio mara sofa lina vishimo, mara lina vimisumari chini, mara stripes rangi ya gold.

Uzuri wa sofa utauona baada ya miaka miwili, hapo unaona urembo low quality usiodumu hata miezi sita especially ukiwa na watoto.
Pendelea kuwa na vitu havivutii sana ila vinaweza maintain ule mvuto wake wa kawaida. Sio unakuwa na kitu shinny for a short period of time alafu shit quality.
 
Wee kolidi water jf expert member ndo unanunua sofa saivi?
 
Ya kwanza ni Aly Ahly FC na hio ya pili ni Mashujaa FC,
 
Kwenye miguu ningekushauri chukua ile mipana iliyojaa yaani kama mbao hivi vifupi. Alafu chukua kochi yenye spring utainjoi zaidi kuliko ya mbao au mipira..
Kimuonekano kwangu la pili
.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…