Mimi ni mtumishi wa umma mwandamizi lakini jambo hili limenipita pembeni na nahisi nimeingia kwenye tatizo kuubwa.
Niliomba mkopo bank kwa kutumia mfumo wa utumishi. Kabla mfumo haujapitisha mkopo bank wakawa wameshaniwekea kiasi Fulani Cha pesa. Sikujua kama ndo ulikua mkopo wangu au la. Nilikuja kushituka baada ya kufanya withdrawal na balance kuwa ndogo kuliko mkopo nilioomba.
Nikawapigia bank hawakunipa ushirikiano. Nikarudi kwenye mfumo wa utumishi nikakuta mkopo umekuwa cancelled. Nikajaribu kuomba tena kwa bank nyingine ikakubali mpaka hatua ya mwisho na pesa nikazitumia. Zote za bank ya kwanza na ya pili.
Tatizo limekuja sasa. Kila mshara ukiingia nakuta balance ni 0. Na bank ile ya mwanzo wanataka niende kuboresha taarifa za akaunti yangu
Nahisi watanifunga. Ila pia sina mshara mwezi wa pili sasa..Hali ngumu. NIENDE AU NIJIKAZE MPAKA PESA YAO WAIRUDISHE KWA KUNIKATALIA MSHAHARA