Naomba msaada wa sheria ya mikataba katika kesi yangu hii hapa

Omikom86

Member
Joined
Dec 17, 2019
Posts
6
Reaction score
2
Kuna mtu niliingia naye mkataba wa kunikodisha chumba cha kufanyia biashara, chumba kilikua hakijakamilika kimatengezo kwahiyo akaniomba fedha kwa ajili ya kukamilisha matengenezo tukakubaliana na mimi nikaandikishiana naye kwamba anipe chumba kikiwa kimekamilika kimatengenezo.

Mimi nikaanza maandalizi ya kununua vifaa mbali mbali kwa ajili ya biashara yangu maana nilijua kwa vile tumeshaingia mkataba hakuna kitakacho kwenda kombo.nimekaa siku kama tano nikaona hakuna matengenezo yoyote yanayoendelea nikaenda kumuliza vipi mbona sioni kinachoendelelea akaniambia wameghairi (wamehairisha) kunikodisha kile chumba cha biashara na wanataka wanirudishie fedha amabazo niliwapa kwa ajili ya kodi.

Nikiangalia kuna gharama ambazo nimeshaingia naomba msaada wa kisheria.

Je, nikienda mahakamani naweza kulipwa hizi gharama ambazo niliingia but keep in mind gharama ambazo nimeingiia ukiachia kodi ni nyingi na wala hatukuandikishiana
 
Hilo ni tatizo la madai tayari na sio jinai kwahiyo hatua ya kwanza nenda ofisi za mtaa wa eneo hilo lilipotokea tatizo katoe maelezo yako kwa kina kwa Mwenyekiti au Mjumbe, utaandika barua ya maelezo hao wataitwa kusikilizwa kama upande wa pili ikionekana kweli wamefanya kosa watapewa amri ya kurudisha kinachodaiwa na wakipinga pale pale ofisini wataandaa barua yao ya kupeleka shtaka la madai mahakamani na utafungua kesi na utaambatanisha maelezo yote ya awali ya mikataba na ofisi ya serikali ya mtaa huko ndiko utapata haki yako stahimilivu kabisa. Akikikisha ushahidi wa mchongo mzima ulivyoanza unafika nao hadi mwisho lazima wafidie na hasara walizokuongezea hata mda wako pia.
 
eo tucheze Mieleka na ulingo ni uhujumu uchumi.. Nani muhujumu uchumi mkubwa Kati ya hawa ambaye kazoeleka na JAMII Kwa mfano:!?

Umefanya shindano Kwa wanafunzi mbinu za kuboresha Kilimo, Uvuvi, na mifugo.. Baada ya kupata maoni tukaamua kuandika mpango Makati Kwa kuzingatia muda...

World Bank wakatoa HELA na fedha ikakaaa benki Kwa mfumo wa figure mfano 20000Milion dollars bila Kufanya lolote... Kiongozi mkubwa SIFANYI MAAMUZI HAPA na MTU wa Chini akatengeneza mchoko wa kuchomoa FEDHA.. SASA ukiwaweka kwenye ulingo wa Mieleka Nani ni muhujumu uchumi!?

Aliyechomoa Fedha Kwa sababu hakuna Maamuzi au ambaye hakuna maamuzi HaPA na kuchelewa utekelezaji wa miradi!?

Wazo wazua kupelekea Christmas na mwaka mpya Mwema

Hilo ni tatizo la madai tayari na sio jinai kwahiyo hatua ya kwanza nenda ofisi za mtaa wa eneo hilo lilipotokea tatizo katoe maelezo yako kwa kina kwa Mwenyekiti au Mjumbe, utaandika barua ya maelezo hao wataitwa kusikilizwa kama upande wa pili ikionekana kweli wamefanya kosa watapewa amri ya kurudisha kinachodaiwa na wakipinga pale pale ofisini wataandaa barua yao ya kupeleka shtaka la madai mahakamani na utafungua kesi na utaambatanisha maelezo yote ya awali ya mikataba na ofisi ya serikali ya mtaa huko ndiko utapata haki yako stahimilivu kabisa. Akikikisha ushahidi wa mchongo mzima ulivyoanza unafika nao hadi mwisho lazima wafidie na hasara walizokuongezea hata mda wako pia.
Nashukuru mkuu kwa maelezo yako ila mkuu kuna gharama ambazo nazo nimeingia kama kununua vifaa kwa ajili ya biashara unahis navyo wataambiwa walipe? Maana niliwahi kwenda kwenye serikali za mitaa lakini ukiwaambia kwamba kuna gharama niliingia out of kwenye mkataba wananiuliza kwani mliandikishiana nikawaambia hatukuandikishiana lakini mkataba wa mwanzo tulofunga ndio umenifanya nikanunua hivi vifaa vyengine basi wao hawaelewi kabisa izo gharama nyengine
 
Unajua mkuu viongozi wengi wa serikali za mitaa kama hao wenyeviti na watendaji hata form4 hawajafika unahisi wataelewa kuhusu mambo ya kisheria just wanakwenda kwa uzoefu tu
 
Mimi sio mwanasheria lakini, ngoja niseme kitu, kuna aina nyingi sana za ku-discharge contracts mfano inaweza kukawa na frustration Hapo Yaani kuna kitu kimetokea na hakikutarajiwa kikavuruga hayo makubaliano yenu, Labda pia kunaweza kukawa na breach of contract in the sense that, ili kuwe na breach of contract kuna takiwa kuwe na vitu viwili mosi ni kunatakiwa kuwe na Mayans na pili, kuna takiwa kuwe na kuvunjwa kwa mkataba huo, swali je hayo makubaliano yanakidhi vigezo vilivyowekwa na sheria ya mikataba sura na 345 r. e 2002 kifungu cha 10 (kama sikosei), Kama yanakidhi vigezo vilivyowekwa na sheria basi unaweza ukashitaki ili ulipwe fidia ya ulicho poteza
 
Mimi sio mwanasheria lakini, ngoja niseme kitu, kuna aina nyingi sana za ku-discharge contracts mfano inaweza kukawa na frustration Hapo Yaani kuna kitu kimetokea na hakikutarajiwa kikavuruga hayo makubaliano yenu, Labda pia kunaweza kukawa na breach of contract in the sense that, ili kuwe na breach of contract kuna takiwa kuwe na vitu viwili mosi ni kunatakiwa kuwe na Mayans na pili, kuna takiwa kuwe na kuvunjwa kwa mkataba huo, swali je hayo makubaliano yanakidhi vigezo vilivyowekwa na sheria ya mikataba sura na 345 r. e 2002 kifungu cha 10 (kama sikosei), Kama yanakidhi vigezo vilivyowekwa na sheria basi unaweza ukashitaki ili ulipwe fidia ya ulicho poteza
Kuna mtu niliingia naye mkataba wa kunikodisha chumba cha kufanyia biashara, chumba kilikua hakijakamilika kimatengezo kwahiyo akaniomba fedha kwa ajili ya kukamilisha matengenezo tukakubaliana na mimi nikaandikishiana naye kwamba anipe chumba kikiwa kimekamilika kimatengenezo.

Mimi nikaanza maandalizi ya kununua vifaa mbali mbali kwa ajili ya biashara yangu maana nilijua kwa vile tumeshaingia mkataba hakuna kitakacho kwenda kombo.nimekaa siku kama tano nikaona hakuna matengenezo yoyote yanayoendelea nikaenda kumuliza vipi mbona sioni kinachoendelelea akaniambia wameghairi (wamehairisha) kunikodisha kile chumba cha biashara na wanataka wanirudishie fedha amabazo niliwapa kwa ajili ya kodi.

Nikiangalia kuna gharama ambazo nimeshaingia naomba msaada wa kisheria.

Je, nikienda mahakamani naweza kulipwa hizi gharama ambazo niliingia but keep in mind gharama ambazo nimeingiia ukiachia kodi ni nyingi na wala hatukuandikishiana
pole sana ndugu!!!
Ikiwa mlifanya makubaliano ya namna yeyote ile na ikiwa hayakutekelezwa na upande mwingine(innocent) ukapata hasara basi yapo mambo kadha ya kujiuliza
1. Je makubaliano hayo yanakizi vigezo vya kuwa makubaliano halali kisheria?
2. km 1 hapo juu ni ndiyo, je kutotekelezwa kwa makubaliano hayo kumetokana na sababu zisizo na kinga ktk sheria ya mikataba?
3. km 2 hapo juu ni ndiyo, je ni nafuu ipi inayofaa kwa upande mwingine?
Nb: hapa zipo nafuu nyingi mojawapo ikiwa ni kuamuru upande uliokiuka makubaliano kutekeleza wajibu wake
Au kulipa hasara iliyopatikana kwa upande wa pili
Lakini ikumbukwe kua km ni kulipa hasara iliyopatikana itakuwa ni kuhusu kiwango cha hasara ambayo inao uhusiano wa karibu zaidi na tukio la uvunjifu wa makubaliano
 
Una Haki ya kurudishiwa fidia kisheria,Ila nakushauri achana na Mambo ya fidia yatakughatimu baadae, rudishiwa pesa yako ya pango tu na utafute chumba kwingine na Mungu atakubariki

Sent using Jamii Forums mobile app
ni kweli wakati mwingine km ukiona kua km akirudisha hiyo pesa ya pango unaweza kupata mahali pengine na kuendesha biashara yako vzr,,,,,bs achana na ishu za mahakamani,,,,
 
Back
Top Bottom