Naomba msaada wa tiba ya homa ya ini

Naomba msaada wa tiba ya homa ya ini

Joined
Sep 21, 2019
Posts
6
Reaction score
6
TIBA YA HOMA YA INI NI IPI?

Ndugu zangu, Wanajukwaa wenzangu Kuna Ndugu yangu amekuwa akisumbuliwa na Maumivu ya Mbavu za Kulia pamoja na Kukojoa Mkojo wenye rangi ya Kahawia na Kutokwa na Jasho Jingi wakati wa Usiku.

Baada ya vipimo alionekana ana hepatitis B na Tayari ini limeshaanza kushambuliwa hali ya kuweka viupele kwa juu japo si kw wingi.

Katika kutafuta tiba ya Shida hii amehamgaika sana na hajapata dawa mpaka sasa zaidi ya kuzunguka tu.

Kwa heshima kubwa naomba msaada wa Tiba sahihi ya shida hii?

Ahsante.
 
Mkuu Huyo ndugu yako hajapata Mtibabu wa kuweza kumtibia maradhi yake ya homa ya ini aka Hepatitis B Virus. Anitafute mimi kwa wakati wake ili niweze kumtibia na aweze kupona maradhi yake.
 
Kunywa juisi ya mbogamboga (Mchicha,majani ya maboga,chinese,matembele unayablend) asubuhi na jioni glass yenye ml 250 kwa siku 45.
 
Pole sanaaaa.....
Na kuwa makini Mzee baba KUNA WAPIGAJI HUMU.

#YNWA
 
Nimekuelewa Kaka,Lakini Hivi kweli kwa hali Kama Hii mtu anapata wapi hata uwezo wa Kumtapeli mtu?
Broh wapigaji wapo kila sehem, hata Sehemu za ibada. Lakini hiyo isiwe sababu ya ww kushindwa kupata tiba sababu ya kuhofia wapigaji.

Kama Mzee Herbalist Dr MziziMkavu amesema anaweza kukusaidia, hebu fanya namna uwasiliane nae then umskilize, kama hutomuelewa, basi achana nae. Ila nakushauri usipuuzie maswala ya kiafya, nyie ndio mnajua ni kwa kiasi gani mnapata tabu huko
 
Nimekuelewa Kaka,Lakini Hivi kweli kwa hali Kama Hii mtu anapata wapi hata uwezo wa Kumtapeli mtu?
Fikra za jinsi hii zitakuponza. Si kweli kwamba eti kwa vile haumli simba ukikutana naye, basi na yeye atasita kukutafuna!

Ulimwengu hauna huruma.
 
Pole saana, mpeleke hospital watampa dawa za kumeza maisha yake yote.
Wengine pia tukumbuke kwenda kuchoma chanjo ya ugonjwa huu wa homa ya ini.
 
TIBA YA HOMA YA INI NI IPI?

Ndugu zangu, Wanajukwaa wenzangu Kuna Ndugu yangu amekuwa akisumbuliwa na Maumivu ya Mbavu za Kulia pamoja na Kukojoa Mkojo wenye rangi ya Kahawia na Kutokwa na Jasho Jingi wakati wa Usiku.

Baada ya vipimo alionekana ana hepatitis B na Tayari ini limeshaanza kushambuliwa hali ya kuweka viupele kwa juu japo si kw wingi.

Katika kutafuta tiba ya Shida hii amehamgaika sana na hajapata dawa mpaka sasa zaidi ya kuzunguka tu.

Kwa heshima kubwa naomba msaada wa Tiba sahihi ya shida hii?

Ahsante.

Njoo inbox
 
HV huwa haiusiani na ukimwi au mm ndio cjui kitu chchote kuhusu hp b virus vzr
 
Tiba ni dawa za tenofivir
Ni expensive sana,wengi huamua kutumia ARV ambazo ndani yake inapatikana iyo tenofivir japo inakuwa kene combination na dawa zingine kama mbili (TLD or TLE)
 
TIBA YA HOMA YA INI NI IPI?

Ndugu zangu, Wanajukwaa wenzangu Kuna Ndugu yangu amekuwa akisumbuliwa na Maumivu ya Mbavu za Kulia pamoja na Kukojoa Mkojo wenye rangi ya Kahawia na Kutokwa na Jasho Jingi wakati wa Usiku.

Baada ya vipimo alionekana ana hepatitis B na Tayari ini limeshaanza kushambuliwa hali ya kuweka viupele kwa juu japo si kw wingi.

Katika kutafuta tiba ya Shida hii amehamgaika sana na hajapata dawa mpaka sasa zaidi ya kuzunguka tu.

Kwa heshima kubwa naomba msaada wa Tiba sahihi ya shida hii?

Ahsante.

Habari,

Tiba ya homa ya ini kwa hepatitis B, hutolewa kwa kufuata vigezo vya kitaaluma.

Vigezo hivyo huusisha kutambua ugonjwa kama ni Acute/muda mfupi au chronic/ muda mrefu (hii huusisha vipimo).

Pia baada ya hapojuu, yafuatayo pia huzingatiwa:
1: Kiasi cha virusi (viral load).
2: Kiasi cha shambulizi lililofanyika kwenye ini/mwonekano wa ini.
3: kiasi cha chemikali itolewayo na ini ambacho ni kipimo cha uwezo wa ufanyaji kazi wa ini pia.

Taarifa hizi ndio husaidia wataalamu kufamya maamuzi ya nini kifanyike, wakati gani na kutumia nini.

Daktari aliyebobea kwenye magonjwa ya njia ya chakula/ gastroenterologist ndiye mlengwa wa kwanza kuhusika na hili.
 
Back
Top Bottom