Naomba msaada wa Tsh.250,000/=

Poluyakhtov

JF-Expert Member
Joined
May 9, 2017
Posts
358
Reaction score
300
Habari za muda huu wana Jamii forum,
Mimi ni kijana ambaye nimechaguliwa chuo cha maji ngazi ya stashahada kozi ya Water Supply and Sanitation Engineering mwaka huu.

Naomba mchango wenu wa tsh. 250,000 ili niweze kulipia semester ya kwanza.Kwa sasa ninacho kiasi cha Shilingi.360,000 na malipo kwa Semester ni Sh.610,000.

Chuo kitafunguliwa tarehe 23 mwezi huu.
kwa yeyote atakayekuwa na nia ya kunisaidia atumie namba 0689997808,
Jina: Thomas Mbata.
Mara nyingi namba haipatikani kwa sababu natumia simu ya kuazima tu.

Ni mara ya pili sasa nachaguliwa kujiunga na chuo, mwaka jana nilipangiwa Vikindu TTC lakini sikuweza kuripoti kwa kukosa fedha.
Naambatanisha screenshot ya sehemu ya orodha ya waliochaguliwa Batch II ya chuo cha Maji, jina langu lipo namba 151.


Mungu awabariki sana!
 
Pole sana usikate tamaa utapata tuuu pia tafta mahali ata kakibarua ka kujishikiza ili uweze kuchangiapo ada najua ni ngumu kweli kupata japo kakibarua lakini jaribu ivo ivo hakuna linaloshindikana ukimuamini mungu
 
Hivi ukiwa hauna simu unaanzaje kupata hizo 360,000 ulizosema unazo? Jf ulijiungaje na hiyo fake id au pia uliazima cm? Nahisi unaogopa kupigiwa uulizwe maswali usiyoyajua.
Usipende kuhisi ndugu,nilijiunga JF kwa simu yangu mwenyewe mwezi wa nne mwaka huu,lakini simu niliiuza ili kuweza kulipia application na kutengeneza cheti cha kuzaliwa nilichokipata RITA mwezi agosti mwaka huu,simu yenyewe ilikuwa NOKIA ASHA 302 niliyoiuza kwa Tsh.35000 tu.Application 10000,B.Certificate 20000 upo! usipende kumchukulia kila mtu kuwa ni tapeli.namba kuna kipindi huwa inapatikana hasa nyakati za jioni!hiyo laki 360,000 nilifanya shughuli za kumwaga zege chini ya kampuni ya ukandarasi ya PARADIGMS na kupigilia misumari kwenye nguzo kuzuia zisipasuke pale New forests Company-Iringa.Baada ya hapo mradi ukawa umekamilika na hakuna kazi nyingine.Na ndio maana nimekwama.
 
Kwani maisha mpaka usome tu?,mambo kama yamegoma piga chini chini ya jua kuna vitu vingi vya kufanya na ukatusua tu, haya utafanikiwa ulipe kwa sasa je awamu nyingine itakuaje?
 
yaani toka mwaka Jana umeshindwa kupata hiyo hela duuuh!. huu ni uzembe kiwango cha lami but pole sana ungejaribu kumuelezea mkuu wa chuo
 
Kwani maisha mpaka usome tu?,mambo kama yamegoma piga chini chini ya jua kuna vitu vingi vya kufanya na ukatusua tu, haya utafanikiwa ulipe kwa sasa je awamu nyingine itakuaje?
Nami najiuliza awamu nyingine itakuaje, na mambo ya msosi n.k itakuaje, hali imekua mbaya
 
Dah!!...asipokuelewa kwa haya maelezo yako bhasi jamaa atakuwa......si bure.

Akhsante sana kumuelewesha vizuri
 
Wana ukoo wako umewashirikisha??? Itisha kikao kama cha harusi kwa ndugu na marafiki kisha uwashirikishe hii kitu. Kama harusi tu michango inafanikiwa na hili lako nalo litafanikiwa kwa njia hiyo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…