Naomba msaada wa ushauri wa kisheria juu ya mgogoro huu wa ardhi

dmketo

JF-Expert Member
Joined
Aug 10, 2015
Posts
646
Reaction score
1,064
Habari ndugu zangu. Kuna ndugu yangu ana nyumba huko Mbezi Msakuzi. Leo wameitwa na mwenyekiti wa mtaa na kuelezwa kuna mtu amekwenda ofisini kwake akamueleza anaomba ampatie barua ya kufufua mipaka ya eneo lake.

Kwa maelezo ya mwenyekiti, mama huyo anadai mumewe alinunua eneo mwaka 1989 na ana karatasi ya mauziano ya eneo ilo. Kwa mujibu wa mwenyekiti alimpatia barua na baada ya siku mbili akaja na watu wa ardhi ili kuangalia mipaka ya eneo husika. Kwa maelezo yake wakiwa wameongozana na mwenyekiti wakaona jiwe la mpaka hivyo wakatambua eneo lote analodai ni la marehemu mume wake. Kwa kifupi eneo tajwa lina nyumba zaidi ya 150 na wote wenye nyumba walinunua kwa wauzaji tofauti kulingana na jinsi maeneo hayo yalivyouzwa. Lakini baada ya kumuuliza mwenyekiti mtu huyu amekuletea nyaraka gani? Akasema alimpelekea karatasi ya mauziano. Akaulizwa muda wote wa miaka 40 alikuwa wapi kudai eneo ilo mpaka watu wamenunua na kujenga takribani nyumba 150+ na mbaya zaidi wengine mpaka wana hati? Akasema kwamba muda wote huo alitingwa na majukumu mengi. Hivyo anaandaa notisi ili achukue eneo lake ambalo kwa haraka haraka ni kama heka 30 na ushee.

Baada ya mwenyekiti kuleta taarifa hiyo, wananchi wachache ambao walikutana na mwenyekiti wameomba kwanza kupitishwa eneo lote ili wajiridhishe lina ukubwa kiasi gani na watambue nyumba zote zinazoangukia ndani ya eneo husika kisha waone hatua gani itachukuliwa ikiwa ni pamoja na kukutanishwa na huyo muhusika kwa ajiri ya kupata ufafanuzi zaidi sababu mwenyekiti hatoi maelezo yanayoeleweka. Watu wakamuuliza vopy za nyaraka ya mauziano aliyopewa akasema anayo ofisini kwake lakini hakuibeba wakati anakuja kwenye kikao.

Je, kwa scenario hii, wananchi wanafanyaje ili kushindana na huyu mama ambaye kwa muonekano wa mwenyekiti na maelezo yake inaonekana ni kama mtu aliyerambishwa asali hivi. Je, hiyo karatasi ya mauziano pekee inaweza kuwa na nguvu ya kisheria?

Naomba wajuzi wanipe muongozo wa kisheria kidogo ili uwasaidie wakazi wa pale kujipanga juu ya mgogoro huu. Asanteni na mniwie radhi kwa andiko refu.
 
Huyo mama hawezi kupata hilo eneo yeye akaendelee na ubize tu, Sheria ukikaa na kujenga sehemu yenye poli Kwa muda wa miaka 12 bila mtu kujitokeza kudai haki yake hiyo ni Mali Yako hata kama hukuuziwa na mtu
 
Asante sana ndugu. Kiukweli ni bora angekuwa na hati, lakini ana hati anasema ana karatasi tu ya mumewe kununua miaka 40 iliyopita. Tukajiuliza mtu aliweka jiwe miaka 40 iliyopita ambapo lilikuwa pori, leo yametapakaa majumba na anasema aliliona ilo jiwe lipo? Imetushangaza kweli hii.
 
Anaweza akashinda kama eneo ilo alikuwa analilipia ardhi na kaweka mawe yake ya ardhi
 
Hata kama ana hati kama hakuendeleza Kwa muda huo hana chale na hati yake ni batili
 
From ChatGPT …
Ndugu, hii ni kesi ambayo imewahi kutokea sehemu nyingi Tanzania, hivyo ni vizuri wakazi wajipange kwa utaratibu wa kisheria badala ya hofu.

Kwanza, karatasi ya mauziano pekee (sale agreement) ya mwaka 1989 siyo ushahidi wa mwisho wa umiliki wa ardhi, hasa kama:
  • haikusajiliwa rasmi serikalini,
  • haikufuatwa na kupimiwa na kupatiwa hati au umiliki unaotambulika.

Pili, kuna kanuni ya kisheria inayotambua umiliki kwa muda mrefu (adverse possession). Kama eneo limekaliwa na watu kwa muda mrefu sana (miaka mingi kama 12+ au zaidi), wamejenga, wengine wana hati, na mmiliki wa awali hakuwahi kudai haki yake kwa muda huo, mahakama mara nyingi hutazama hali hiyo kwa uzito.

Kwa hiyo wakazi wanaweza kufanya mambo haya:

1. Kuomba kuona nyaraka halisi
Wenye nyumba waombe nakala ya hiyo karatasi ya mauziano ili ijulikane:
- ilinunuliwa kutoka kwa nani
- ukubwa wa eneo
- mashahidi waliokuwepo
- kama iliwahi kusajiliwa.

2. Kukusanya nyaraka zao wenyewe
Kila mkazi akusanye:
- mikataba ya manunuzi
- hati za umiliki kama zipo
- risiti za manunuzi
- ushahidi wa muda waliokaa hapo.

3. Kufika Ofisi ya Ardhi ya Wilaya/Manispaa
Waombe ramani ya eneo (survey plan) na kujua:
- kama eneo hilo lina mmiliki aliyesajiliwa
- kama liliwahi kupimwa rasmi.

4. Kuunda kamati ya wakazi
Badala ya kila mtu kupambana peke yake, wachague watu wachache wa kuwasiliana na serikali ya mtaa, ardhi na mwanasheria.

5. Kupata ushauri wa mwanasheria wa ardhi
Kama kweli kuna nyumba zaidi ya 150 na baadhi wana hati, ni vigumu sana mtu mmoja kuondoa watu wote bila mchakato wa mahakama.

Muhimu pia kufahamu:
Mwenyekiti wa mtaa hana mamlaka ya kuthibitisha umiliki wa ardhi. Anaweza kusaidia taarifa tu, lakini uamuzi wa mwisho uko kwa Idara ya Ardhi au Mahakama.

Kwa hiyo wakazi wasiwe na panic kwanza, bali wachukue hatua za kukusanya nyaraka na kupata ushauri wa kisheria mapema.
 
Hawezi kushinda hiyo kesi hata kama ulikuwa unalipia lakini hukwenda kuendeza na watu wamejenga na wao wanalipia
Issue inaanza kwa hao watu wa Ardhi, unajua hapo kuna swali kwamba inawezekanaje? Unajua lazima uanze na kujiuliza maswali issue km ingekua hivyo hata hao watu wa ardhi wangemgomea kwamba how come wewe miaka yote hio unakuja leo? Ushanielewa kwa hio kuna kaharufu fulani ka rushwa kananukia hapo, kisheria ipo hivi

Kesi hii ilitoa mambo 8 ya kesi km hii uliyoileta hapa:

Mahakama ya Rufaa ya Tanzania kupitia uamuzi katika shauri la Bodi ya wadhamini ya shirika la masista wa roho mtakatifu dhidi ya January Kamili Shayo na 136 wengine, Shauri la Rufaa Namba 193 la Mwaka 2016 (Mahakama ya Rufaa Tanzania) imetoa mambo nane (08) ambayo ni lazima kuyazingatia na kuyathibitisha ili mtu apate umiliki wa ardhi kwa njia ya kujitwalia. Hivyo ili sheria iweze kumtambua kuwa mtu ana umiliki wa ardhi kwa njia ya kujitwalia ni lazima mambo yafuatayo yazingatiwe na yathibitishwe.

1.
Ardhi husika iwe imetelekezwa.

Mtwaaji au Mvamizi anahitajika kuthibitisha kuwa ardhi husika ilitelekezwa na hivyo wakati “mvamizi” anaingia hakukuwa na mtu wala uendelezaji wowote kwenye ardhi husika. Hapa lazima ifahamike kwamba mtwaaji anapaswa akute ardhi husika imetelekezwa. Lakini kama mtwaaji wakati anaingia kwenye ardhi hiyo kulikuwa na mmiliki ama maendeleo yoyote basi dhana hii haitoweza kutumika na haitokuwa na maana katika kujipatia ardhi kwa njia ya utwaaji.

2. Mtwaaji/Mvamizi awe ana umiliki endelevu kwa kuwemo ndani ya ardhi husika.

Hii ina maana kwamba mtwaaji wa ardhi atatakiwa kuthibitisha kuwa yeye ndiye aliyekuwa anamiliki ardhi husika katika kipindi chote kilichowekwa kisheria, ambapo kwa sheria ya nchi yetu ni kipindi cha zaidi ya miaka kumi na mbili (12). Hii inaweza ikawa kwa kulima, kujenga, kuishi au kwa namna nyingine yoyote ambapo jamii ya sehemu husika itatambua kwamba mtwaaji ndiye mmiliki wa eneo husika.

3. Mtwaaji/Mvamizi asiwe na haki yoyote ya umiliki wa ardhi hiyo zaidi ya kuvamia na kuikalia.

Hapa mtwaaji atahitajika kuthibitisha kuwa katika ardhi hiyo ameingia kwa kuvamia na kuikalia na wala si vinginevyo. Ikiwa itathibitika kuwa mtwaaji aliingia kwenye ardhi hiyo kwa kukaribishwa, kupangishwa, kuuziwa, kufanya ulinzi au namna nyingine yoyote kinyume na kuingia pasipo kuwa na ruhusa, basi mtu huyo hawezi kudai umiliki wa ardhi hiyo kwa dhana ya kuitwaa.

KWA MFANO: Manyota alimuomba Mayombo eneo la shamba ili aweze kulima. Mayombo alimkaribisha Manyota na kumuachia shamba hilo alime na atakapolihitaji basi atalirudisha. Baada ya makabidhiano, Mayombo alisafiri kuelekea ughaibuni ambako alikaa zaidi ya miaka ishirini huku Manyota akiendelea kulima shamba hilo kwa miaka yote. Mayombo aliporudi na kuhitaji shamba lake Manyota alikataa kulitoa akidai kuwa amelitumia shamba hilo kwa zaidi ya miaka 12 hivyo shamba hilo ni la kwake kisheria kwani amelipata kwa njia ya kujitwalia.

Kisheria Manyota hawezi kutumia dhana hii ya kwamba shamba hilo ni la kwake na analimiliki. Hii ni kwasababu, Manyota hakuvamia na wala shamba hilo halikutelekezwa bali alikaribishwa baada ya kuomba.

4. Mtwaaji/Mvamizi awe amefanya maendeleo kwenye ardhi husika.

Mtwaaji wa ardhi atatakiwa kuthibitisha kuwa ameindeleza ardhi hiyo kwa kipindi chote cha zaidi ya miaka kumi na mbili (12) kwa matakwa yake mwenyewe. Na vilevile lazima ithibitike kuwa maendeleo yaliyofanywa na mtwaaji kwa manufaa yake, yalifanyika bila ridhaa na kinyume cha uendelezwaji uliokusudiwa kufanywa na anayedai kuwa mmiliki. Lakini kama itathibitika kuwa uendelezwaji huo umefanyika kwa kufuata matakwa au maelekezo ya anayedai kuwa mmiliki wa ardhi hiyo, basi mtwaaji huyo hawezi kutumia dhana ya umiliki wa ardhi hiyo kwa njia ya utwaaji.

5.
Mtwaaji/Mvamizi awe na nia au awe amedhamiria kumiliki ardhi husika.

Mtwaaji lazima athibitishe kuwa alikuwa na nia au dhumuni la kumiliki ardhi husika na kuondoa umiliki wa mtu mwingine yoyote akiwemo anayedai kuwa mmiliki. Hii inaweza kuthibitishwa kwa gharama za uendelezwaji wa ardhi hiyo zilizoingiwa na mtwaaji kama vile kusimamisha jengo, kilimo, kuweka uzio na maendeleo mengine. Lakini hapa pia lazima izingatiwe kuwa kama maendeleo au umiliki wa ardhi hiyo katika kipindi chote cha miaka kumi na mbili au zaidi ulifanywa kwa pamoja kati ya mtwaaji na anayedai kuwa Mmiliki, basi mtwaaji hawezi kutumia dhana hii ya umiliki wa ardhi hiyo kwa njia ya utwaaji.

6. Mtwaaji/Mvamizi awe amekaa kwenye ardhi zaidi ya miaka kumi na mbili (12).

Sheria inamtaka mtwaaji wa ardhi lazima athibitishe kuwa amekaa kwenye ardhi husika katika kipindi cha zaidi ya miaka kumi na mbili (12) mfululizo. Kama itabainika kuwa mtwaaji hakuikalia ardhi husika kwa zaidi ya miaka kumi na mbili (12) mfululizo yaani kuna kipindi ambacho alikuwa akiiacha ardhi hiyo, basi mtwaaji hawezi kutumia dhana hii ya umiliki wa ardhi hiyo kwa kujitwalia.

7. Katika kipindi hicho cha miaka kumi na mbili (12) au zaidi, kusiwe na bughudha yoyote kuhusiana na umiliki wa ardhi hiyo

Mtwaaji atatakiwa kuthibitisha katika
kipindi chote cha miaka kumi na mbili (12) ambacho alikuwa ameikalia ardhi husika hakuwahi kubughudhiwa na hakuna aliyewahi kudai kuwa na umiliki wa eneo husika. Bughudha inaweza kuwa; kupeleka shauri mahakamani, serikalini, ukoo, wazee
wa kimila au namna nyingine yoyote ambapo anayedai kuwa mmiliki alishadai kurudishiwa ardhi yake. Kama itathibitika kuwa anayedai ni mmiliki aliwahi kuidai ardhi yake ndani ya kipindi hicho cha miaka kumi na mbili (12), mtwaaji hawezi kutumia dhana hii ya umiliki wa ardhi hiyo kwa njia ya kutwaa.

8.
Kwa jinsi hali ya ardhi husika ilivyokuwa, ilionyesha wazi kwamba umiliki kwa njia ya utwaaji ungetokea.

Mtwaaji atahitajika kuthibitisha kuwa ardhi husika ilikuwa ina dalili zote za kumilikiwa kwa njia ya utwaaji. Hii inamaanisha kuwa, ardhi husika haikuwa na maendelezo yoyote, mgogoro wa aina yoyote, kukabidhiwa/kupangishwa, kupewa maelekezo au mambo kama hayo.

Angalizo: Lakini vilevile lazima ifahamike kuwa mtwaaji au mvamizi hawezi kudai umiliki wa ardhi kwa njia ya kujitwalia au uvamizi kwenye ardhi ambayo imepimwa na ina hati miliki.

Ikumbukwe kuwa mmiliki wa ardhi kwa njia ya kujitwalia lazima aweze kuthibitisha hayo mambo nane (8) ndipo sheria iweze kumtambua kuwa ndiye mmiliki halali. Endapo itatokea mtwaaji ameshindwa kuthibitisha moja au zaidi kati ya hayo mambo nane, basi hataweza kupewa umiliki wa ardhi kwa njia ya kujitwalia. Vilevile, lazima ifahamike kuwa umiliki wa ardhi kwa njia ya kujitwalia hutumika kama utetezi (defence) mahakamani pale mtu anaposhitakiwa kwa kuvamia ardhi ya mtu.
 
Ongea na ChatGPT upate msaada murua wa kisheria, just copy and paste your post uanze mchakato😂😁
 
Migogoro ya ardhi mi hua sielewi kwanini serikali inakosa njia sahihi ya kuimaliza.Hivi kwani na kwa wenzetu walioendelea hua Kuna migogoro kama hii?
Shida ni Sheria zetu zilivyo kwanza Ardhi ni ya Serikali hakuna anaemiliki ardhi zaidi ya Serikali, kwa hio shida inapotokea utasikia simamisha ujenzi nyumba imekula chata kwamba fika ofisi namba ngapi sijui na hivyo, sasa ukienda kule ndio wanakwambia kwamba nini ufanye taratibu zikoje utakamuliwa hela kwanza upate kibari ndio uje ujenge ushaona hapo, sasa imagine nyumba 150+ zipo kwenye eneo miaka zaidi ya 50 na mmiliki hajawahi kubembelea eneo hilo zaidi ya miaka 40, unanielewa sijui hapo au zinaongea bia sio mimi?
 
Asante sana chief.
 
Asante sana chief. Umenipa nondo za maana sana. Nadhani wengi watafaidika pamoja nami kwa nondo hizi.
 
Hana jipya hapo, mwenyekiti akileta kelele mwambieni akafungue kesi ya madai.

Tuna nyumba mkoa fulani, tuli fata utaratibu wa kudai ofisini kesi ikaenda mahakamani.

Hakuna maridhiano ya mdomo, ikiwa mna hati na mme zilipia Kodi.
 
Mkuu kesi za aina hii ni ngumu na zipo nyingi na uchukua muda mrefu kukamilika.
Kwa ufupi akiwa na facts zinazothibitisha kuwa yeye ndiye mmiliki halali wa awali na wengine ni wavamizi anashinda kesi. Ukweli mchungu ni kuwa Negligence katika usimamizi na uendelezaji unampa Rais uhalali wa ku revoke umiliki, lakini hautoi uhalai kwa wavamizi kujitwalia.

Fact kuu ni hati au Offer letter. Kabla ya sheria ya ardhi ya 1999 Offer ilikuwa ni halali na ilikuwa halali kumiliki shamba Dar.
Ona Kesi ya Maeda Vs. wananchi takriban 300 pale Kibamba CCM. Kesi ilivuma kwa zaidi ya miaka kumi lakini hatimaye mdai ambaye ni Maeda alishinda.

Ushauri: Kama wananchi hamna facts zenye mashiko ingieni katika majadiliano ya kumaliza kesi nje ya Mahakama. Kesi ikivuma mji utadumaa kwani patapigwa stop order itakayowazuia kufanya uendelezaji wa aina yoyote.
Kwa upande Mdai kesi za aina hii huwa hata ukishinda hautafaidika, kwani jamii hutumia mbinu mbadala za aina mbalimbali ambazo mwisho wake huwa siyo mwema kwa mdai.
Katika Kesi ya Maeda: yeye hakuwepo siku hukumu ya mahakama ya rufaa inatoka na hata watoto waliokuwa wanasimamia kesi hiyo hawapo, hivyo hakuna wa kuhakikisha hukumu inatekelezwa kutokana na hali hiyo wananchi wanaendelea kuishi katika ardhi husika.
Kwa unyenyekevu nawashauri Jadirilianeni muyamalize under win-win situation
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…