Naomba mwenye kuweza kusaidia, asaidie hii jamii, kobe ni wasumbufu sana

Naomba mwenye kuweza kusaidia, asaidie hii jamii, kobe ni wasumbufu sana

Lanlady

JF-Expert Member
Joined
Feb 27, 2019
Posts
1,836
Reaction score
6,303
Nimesoma mahali kuna mchina kakamatwa kwa kukutwa na kobe watano anaowatumia kama kitoweo.

Wilayani butiama mkoa wa mara kuna mtu alishtakiwa kwa kukutwa na kobe.

Ukweli ni kwamba wilayani humo viumbe hao wako wengi sana na wanaharibu mazao hasa majani ya maharage na kunde. Kama kuna mwekezaji anayeweza kuwatumia, apewe kibali cha kuwakusanya.
 
Kwa sasa ni biashara.
Kobe yule mdogo mwenye saizi ya ngumi yako anauzwa shilingi 4000-5000 hii ni bei kwa anaekuja kuwalanguwa.
Ila walanguzi nao wanawauza kuanzia 10000-20000.
Hapo kobe mkubwa hahitaji na ni biashara ya siri sana kama bangi.
Na masharti ya hao kobe ni asiwe na alama ya kupigwa jiwe au kukatika kucha, na kuna magamba yawe yametimia.
 
Waganga wa jadi wanatumia sana Kobe Ogopa sana mtu akurogee Kobe😀😀 ni hutoboi
 
Waganga wa jadi wanatumia sana Kobe Ogopa sana mtu akurogee Kobe😀😀 ni hutoboi
Ndugu yangu Santos mbona umeiweka mbele sana hiyo Imani juu ya waganga? So wataka kuniambia hata wakimloga Mwamposa au Kakobe hawatoboi?
 
Shemeji yetu.. Ni mchina ama?

Anyways one among wedding gifts za my parents ilikua Kobe.

Huyu alikua anazunguka wee anarudi mwenyewe.

Ila akaja kupotea kabisa.
Kama yupo hai kuna siku atarudi.
Wanasema hao viumbe huwa hawasahau kwao.
 
Ndugu yangu Santos mbona umeiweka mbele sana hiyo Imani juu ya waganga? So wataka kuniambia hata wakimloga Mwamposa au Kakobe hawatoboi?
Mbona unamwamini mwamposa? Huyu si mtu tu kama wengine
 
Back
Top Bottom