Naomba mwongozo wa kwenda The Hague(ICC)

Naomba mwongozo wa kwenda The Hague(ICC)

Mushkov

JF-Expert Member
Joined
Feb 16, 2024
Posts
357
Reaction score
686
Kutokana na vitendo vya utekaji, utesaji na pengine mauaji kushamiri katika Nchi hii, nakusudia kwenda The Hague(ICC) kuwashtaki baadhi ya wenye Mamlaka ili waiambie Mahakama ni kwa nini haya mambo yanayokea na wao ambao ndo wenye dhamana ya kuyazuia, wapo kimya?
 
gentleman,
kisutu imeshindikana hata usumbue taasisi za kimataifa?

unadhani kuna mtu aliwashtaki Netanyahu na waziri wake wa ulinzi na Yule kiongozi wa Hamas ICC, au mahakama hiyo iliona iwajibike kulingana na hali inavyoripotiwa katika vyombo vya habari? :NoGodNo:
 
Unaweza. Mshtue Prosecutor aje kufanya upelelezi na kuthibitisha Kama kosa Hilo lipo Chini ya makosa ya Rome Statute 1998. Hasa kosa la uhalifu dhidi ya binadamu crimes against humanity. Sema itakuwa ngumu kifikisha vigezo vya kimataifa.
 
gentleman,
kisutu imeshindikana hata usumbue taasisi za kimataifa?

unadhani kuna mtu aliwashtaki Netanyahu na waziri wake wa ulinzi na Yule kiongozi wa Hamas ICC, au mahakama hiyo iliona iwajibike kulingana na hali inavyoripotiwa katika vyombo vya habari? :NoGodNo:

Kisutu ipi?. Hii ya kupigiwa simu.
 
Kiegezo muhimu (kama ambavyo Israel inajitetea) ni mfumo wa haki na mahakama za nchi husika kushindwa kutimiza wajibu wake kwa viwangona weledi stahiki
 
Kisutu ipo?. Hii ya kupigiwa simu.
imani potofu hizo gentleman,

kiufupi sana mahakama ya ICC inadeal specifically na mambo makuu kadhaa kama ifuatavyo

1. Crimes of genocide, yaani kuangamiza watu wa kabila, dini au rangi fulani na kuwatokomeza kabisa

2. Crimes against humanity, kudhuru na kuwaangamiza raia wasio na hatia kwa kiwango kikubwa mahospitalini, kwenye nyumba za ibada, mashuleni n.k, ubakaji, utekaji, utumikishwaji wa watu kingono au kijeshi, kupotea kwa watu kiholela n.k

3. Crime of aggression,

4. War crimes which are grave breaches of the Geneva conventions in the context of armed conflict and include, for instance, the use of child soldiers; the killing or torture of persons such as civilians or prisoners of war; intentionally directing attacks against hospitals, historic monuments, or buildings dedicated to religion, education, art, science or charitable purposes.

pamoja na hayo,
ni lazima mahakama za ndani ya nchi husika sikose uwezo wa kushughulika na mambo hayo kisjheria ndipo sasa mahakama ya ICC inaweza kuingilia kati katika kutafuta haki za waathirika.

kinyume na hapo ni makelele tu.
Tanazania hakuna shtaka lolote kwa ICC kuja kupoteza muda na rasilimali zake kulingana na majukumu yake.
Na haitakuja kutokea mahakama ya ICC kuja kushughulika na hayo mambo ya mauji kwasababu nchiu yetu ni ya amani.

na matukio ya machache ya wananchi kupoteza maisha kwenye ajali, majanga ya moto au kuporomoka majengo na migodi au fumanizi za wananchi kuibiana wake yanatokea hata kwenye nchi nyingine na ni jambo la kawaida na ICC haihusiki hata kidogo. :BASED:
 
gentleman,
kisutu imeshindikana hata usumbue taasisi za kimataifa?

unadhani kuna mtu aliwashtaki Netanyahu na waziri wake wa ulinzi na Yule kiongozi wa Hamas ICC, au mahakama hiyo iliona iwajibike kulingana na hali inavyoripotiwa katika vyombo vya habari? :NoGodNo:
Sasa key sutu si inasemekana pilato aweza pigiwa simu akapewa maagizo. Kumbuka issue ya Rost arm Aziz key stephano wa nyuma mwiko
 
Kutokana na vitendo vya utekaji, utesaji na pengine mauaji kushamiri katika Nchi hii, nakusudia kwenda The Hague(ICC) kuwashtaki baadhi ya wenye Mamlaka ili waiambie Mahakama ni kwa nini haya mambo yanayokea na wao ambao ndo wenye dhamana ya kuyazuia, wapo kimya?
Hao The Heague ndio wafadhili wa watekaji.

Huyo Putin, China, Russia, Canda na USA lao ni moja.

Usiwaamini hii mikwara wanayopigana.

Ni namna ya kuitawala dunia.
 
Back
Top Bottom