Naomba nipingane na mwandishi Erick Kabendera kuhusu hoja ya kumtaka Mbowe aende KWENYE meza ya mazungumzo.

Naomba nipingane na mwandishi Erick Kabendera kuhusu hoja ya kumtaka Mbowe aende KWENYE meza ya mazungumzo.

Beatrice Kamugisha

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2019
Posts
762
Reaction score
6,984
Naomba Chadema mnielewe vyema na mjitafakari Sana kuhusu mjadala ulioanzishwa na Zitto na baadaye Mwandishi wa habari na ndugu yetu Erick Kabendera kuingilia Kati. Kwanza tunapaswa kujua Erick Kabendera ni nani kwenye mfumo wa siasa na amechangia vipi awamu ya tano kuingia madarakani kabla awamu hiyo kumkamata na kumweka ndani.

Erick Kabendera, Januari Makamba, Kinana, Nape na wengine kumbukumbu zinaonyesha wao ndio walioshiriki kuhakikisha kwamba Lowasa anashindwa uchaguzi 2015. Hawa watu ndio walioshirikiana na baadhi ya vijana wa IT kuiba uchaguzi uliomweka madarakani JpM. Nape wiki Ili aliandika kwenye ukurasa wake wa tweeter akijinadi kwamba bila yeye Lowasa angekuwa Ikulu. Alitaka kumwonyesha Polepole kwamba yeye Nape kwenye CCM ni Nani.

Baada ya awamu ya Tano kuingia madarakani JPM Nadhani makubaliano au mategemeo ya akina Kinana yalibadilishwa na ndipo mfumo ulipoanza kupambana nao bila kujali ushiriki wao kwenye Vita ya kuwaungiza madarakani. Walisambaratishwa mmoja baada ya mwingine Hadi ilipozaliwa mfumo mpya. Na hata baada ya kusambaratishwa na kwakuzongatia Bado watu Hawa walikuwa na wafuasi nyuma Yao JPM Nadhani ndipo alipoamua kutowatumia Tena kwenye uchaguzi kama viungo wachezeshaji, in short waliwekwa bench na rigging ya election ikafanyika kwa style tuliojionea.

Kwa kuwa Erick alitambua dhambi iliyokuwa nafsini mwake kuhusu tawala za afrika ilimlazimu kuingia kwenye mazungumzo may be ikiwemo kuomba msamaha kwa sababu anajua wapi alikengeuka. Nimeona kwenye post yake anakiri walifanya vikao zaidi ya 50 na JPM Hadi yeye anatolewa gerezani. Tujiulize Erick ni nani hadi afanyiwe vikao 50 ? Alikosa Nini? Vikao vilihusu Nini? Hakuna aliyejua Erick aliwahi kufanyiwa vikao vya usuluhishi akiwa gerezani hadi Leo alipoandika mwenyewe tweeter. Na kwa muktadha huo lazima tutambue Erick SI mtu mdogo ni mtu mwenye nafasi au alikuwa na nafasi flani kwenye mfumo.

Kwanini nawataadharisha CHADEMA kuhusu Erick, nikwasbabu Mbowe Hana kosa alilotenda lakini Erick alikuwa na makosa yake yakupingana au kushindwa kukubaliana na wenzie alioshirikiana nao kwenye uchaguzi 2015.

Lakini pia nawataadharisha CHADEMA dhidi ya Erick kwa sababu kwa sasa Erick na watawala akina Januari Makamba ni kitu kimoja. Kuwa mwanaharakati sometimes Kuna saidia lakini lazima tuwaangalie vyema hawa wanaotumwa kujadili hoja ya maridhiano wanatumwa na Nani? Kukubaliana nao sometimes nikukubali kununua haki Yako.

Erick na Zitto wamewahi kupingana na utawala uliopo kwa chochote? Means kwa Sasa hawa pia ni watawala ila hawana nafasi zinazoonekana Kwa macho. Madhara ya Mbowe kwenda kwenye mazungumzo kwa kuwasikiliza akina Erick nikufungua milango ya kuzimwa kwa agenda ya katiba mpya iliyopelekea Mbowe awe ndani Leo. Lakini majadiliano yenye masharti upelekea uliyekubaliana naye kukudhibiti kwa masharti yale Yale .

Nikubaliene n wanaounga MKONO kwamba waliomweka Mbowe ndani ndio wenye makosa na ndio wenye maamuzi afungwe au afutiwe Kesi. Endapo tukiruhusu majadiliano tukubaliane na masharti ya majadiliano, lakini kwa kuwa tunaamini kama Taifa kuwa Mbowe Hana kosa basi tubaiki na msimamo wetu kwamba tuache mahakama iamue kumfunga lakini tubaki na moyo thabiti wakuendeleza mapambano dhidi ya demokrasia.

Hatuwezi tukafanya mazungumzo kuhusu mwenyekiti tukawa na nguvu yakuwanyamazisha akina mdee, lazima tutalazimika kufanya mazungumzo nao. Tuache wakosaji wafanye wazungumzo, MBOWE SIYO MKOSAJI.
 
haya ndio mambo yanafanya watawala watuone bogus na kutufanya chochote. yaani Rais anaonyesha wazi anataka kumfunga Mbowe kwa hila halafu watu badala ya kupaza sauti kukataa udikteta,eti wanashauri aombe msamaha. pumbavu kabisa.

Wa kuomba msahama ni Rais Samia sio Mbowe
 
Erick Kabendera ni mwana CCM Aidha Kwa kadi au kwa mashirikiano yakiimani na kimaslahi. Ni kweli kabisa kwamba Erick ameshiriki kubomoa mfumo wetu wa siasa hasa pale alipokubali kuingia kwenye timu ya mkakati ya CCM 2015 nakumweka JPM madarakani.

Kwa upande wa pili,Wana chadema n wanaharakati bila kujali itikadi zao walipaza sauti Sana alipokamatwa. Hakuna mwanachadema wala mwanaharakati aliyemuhukumu alipokamatwa na kuwekwa ndani Kwa makosa ya michongo. Kelele hizo ndizo zilizopelekea JPM akakubali kumsikiliza japo muda ulikuwa umekwenda sana. Aliumizwa na kinyago alichochonga mwenyewe.

Chakusikitisha, baada ya kutoka ndani hakuwahi kuendelea kuwapigania wanaoteseka Bali alikwenda likizo. Means Moja ya masharti aliyopewa nikuambiwa akae kimya na ametii maelekezo yake.

Leo wanamtandao wenzake wanaingia madarakani badala awashauri waache kuwatesa wasio na hatia anakuja kushawishi mazungumzo. Kibaya zaidi CCM wamekaa huko yeye na Zito ndio wanakesha tweeter kuleta hoja walizotumwa na watesi wetu. Huu ni uzandiki, na kwa njia hii wao ndio wanaosababisha wasio na hatia wabaki madarakani Kwa kuwa wanakubali kutumika.

Endapo Zitto na Kabendera wangepiga kelele kama walivyopigiwa kelele mitandaoni walipokuwa ndani Watawala wangesikia na wangejitokeza kusimamia haki. Kama wameshindwa kusimamia haki nakupaza sauti kama walivyopaza sauti wengine dhidi Yao basi Bora wakae kimya.

Wasiungane na watawala kwa sababu TU ni ndugu na marafiki zao, waungane n wataka haki. Nimeumizwa sana kuona wanachofanya tweeter, Hadi kupelekea Zitto kutoa taarifa za uongo kuhusu familia ya Mbowe.

Hawa watu wameonyesha usaliti na ukatili mkubwa dhidi ya wafungwa na mahabusu wa kisiasa pamoja na demokrasia Kwa ujumla
 
Wakati mwingine unakubali kujishusha kidogo ili mengine yaende. Jela si kuzuri. Sisi tunashabikia tu kwa sababu tuko nje. Ujasiri aliounesha unatosha. Aombe wakae mezani wasameheane arudishiwe uhuru wake arudi kuungana na familia yake
 
Swadakta,kukubari mazungumzo yoyote yatakayo mfanya kukubari kuwa Ana hatia,wakati hukumu ya jamii inasema Hana hatia Mbowe si gaidi. Amini amini nawaambia siku akienda tofauti au kinyume na hukumu ya jamii umaarufu wake unaisha Kama wa watu waliorejea CCM.
Awe Rowasa,Silaa Nani na Nani wote waliisha kisiasa pindi tu waliposaliti Imani ya jamii na kujisalimisha kwa watawala.
Mbowe asije fanya Hilo kosa.
Amini amini nawaambia Mbowe kwa sasa Ni mtu maarufu na anaeaminika kuliko raia yeyote wa tz.

Mh maza bwana mademu wanampinga kuliko Rais yeyote wa CCM toka tupate Uhuru.
 
Swadakta,nakubari mazungumzo yoyote yatamfanya kukubari kuwa wakati hukumu ya jamii inasema Hana makosa na siku akienda tofauti na hukumu ya jamii umaarufu wake unaisha Kama watu waliorejea CCM.
Owe Rowasa Nani na Nani wote waliisha kisiasa Mbowe asije fanya Hilo kosa.
Amino amino nawaambia Mbowe kwa sasa Ni mtu maarufu na anaeaminika kuliku raia yeyote wa tz.
Mh maza bwana mademu wanampinga kuliko Rais yeyote wa CCM toka tupate Uhuru.
Soma tena ulichoandika mkuu
 
Wakati mwingine unakubali kujishusha kidogo ili mengine yaende. Jela si kuzuri. Sisi tunashabikia tu kwa sababu tuko nje. Ujasiri aliounesha unatosha. Aombe wakae mezani wasameheane arudishiwe uhuru wake arudi kuungana na familia yake
MWANAUME, heri ufe Leo ukiwa shujaa,kuliko kufa kesho ukiwa dhariri. Over and out hayo waambieni watoto wa kike sio a man of people Kama Mbowe.
 
MWANAUME, heri I've Leo ukiwa shukaa,kuliko kufa kesho ukiwa dhariri. Over hayo waambieni watoto wa kike sio a man of people Mbowe.
Sawa, wewe si uko nje unakula chips kavu ndiyo maana unajiandikia tu hayo?Nenda kamsadie kule hata siku moja tu ndo utajijua kama manaume au mwanamke.
 
Back
Top Bottom