Naomba nipingane na mwandishi Erick Kabendera kuhusu hoja ya kumtaka Mbowe aende KWENYE meza ya mazungumzo.

Zitto analijuwa kosa la Mbowe kwa kuwa kuna taarifa alishirikishwa. Baada ya Magufuli kutangazwa mshindi na NEC kwenye uchaguzi ambao hata mimi naamini uligubikwa na wizi wa kura kupitia TISS, Mbowe, Lissu na Lema waliitisha maandamano yasiyokoma.

Lakini vile vile walipanga malipuzi Ili nchi isitawalike. Ilikuwa barabara zinazoingia mjini wana CDM wachome matairi na magogo ili wananchi washindwe kwenda kwenye shughuli zao.

Bahati mbaya kwao TISS waliwatangulia waka i abort. Then Magufuli ndiyo akaanza kuwatafuta akina Lissu, Lema na Mbowe. Kama unakumbuka vizuri Lissu ilibidi ajisalimishe Germany embassy. Lema akakamatwa Kajiado Kenya baadaye akaachiwa na Mbowe aka sneak na kuanza kuishi kati ya Nairobi na Dubai. Kimsingi alikwishaomba hifadhi ubalozi wa Canada ila alikuwa bado hajapata baada ya kukosa Denmark.

Tumshukuru Mungu yule Mwendazake hakuwakamata maana ambacho angewafanya ni kibaya kuliko cha Lissu mwanzoni. Kwa hiyo tuiachie Mahakama ndiyo iseme kuwa Mbowe hana HATIA baada ya kusikiliza ushahidi wote na kisha Mbowe kujitetea.
 
Nakubaliana na wewe kabisa
 
Mbowe Ni gaidi au si gaidi Ni mahakama ndo itaamua, nipinga kwa nguvu zote kabisa mbowe kuachiwa Bila mfumo wa sheria kufuatwa, yaan ninyi watu sijui mnajisahaulisha au mmepewa hela, sijui, kesi ya mbowe haina mahusiano yoyote na katiba mpya, na mnajua kabisa, tatzo kubwa watu wanajizima data makusudi,

Kesi ya mbowe Ni Jimbo la hai, huko walikuwa sabaya na mbowe, kila mmoja akiwa na nanafsi yake, unajua kabisa, na wote wanamashitaka yanayotokana na siasa, so kufungwa kwa sabaya hakuhalalishi hakuondoi makosa ya mbowe, kila mtu apambane na Hali yake,

Ikifika hatua tukawa tunajizima data kwa sabab ya kuwafever watu tunaowapenda hii nchi itakuwa mbaya mno kuishi, maana itakuwa na imbalance of law..

Hakuna roundtable au nn wacha mahakama itende haki, tusiinaji mahakama kwa makusudi, na hapa mama ndo kipimo chake Kama kiti kinamuenea walao kidg au lah, siku akiachiwa mbowe Bila mahakama tutaanzisha kampeni kuu ya #@freesabaya
 
Umeandika uongo usio katika mizania.
Kama hayo unayoyasema mbona ushahidi wa mahakamani hauendani.
Kama TISS walikua wanajua ukweli wa Ugaidi huo sidhani kama leo kungekua na ushahidi duni hivyo huko mahakamani.
Maandamano yasiyokoma sio Ugaidi.
Na maandamano baada ya kuibiwa ushindi yapo kila nchi inapotokea hali hiyo.
Kwa kifupi hii kesi haina uhalisia.
Ni siasa za chuki tu.
 
Wakati mwingine unakubali kujishusha kidogo ili mengine yaende. Jela si kuzuri. Sisi tunashabikia tu kwa sababu tuko nje. Ujasiri aliounesha unatosha. Aombe wakae mezani wasameheane arudishiwe uhuru wake arudi kuungana na familia yake
Atasamehewa kwa makosa gani?
 
Umemkuza sana Erick Kabendera bila sababu yoyote ya msingi , labda kwa taarifa yako ni kwamba CHADEMA INAFAHAMISHWA KILA UJINGA UNAOFANYWA NA YEYOTE KUHUSU KESI YA MBOWE .
 
Hakika ujinga wa uzeen lazma utakufa nao tu
 
Mbowe alipue nchi?

Hivi mzima wewe?

Mtu hana hata mshale,alipue nchi?

Punguza ukuda wewe!
Wyatt Mathewson jiulize kwa nini wamkamate yeye na siyo wewe au Mimi? Pili jiulize nini kilimkimbiza Dubai baada ya matokeo kutangazwa.

The fact kwamba you aren't informed doesn't entail that I am uninformed as well. You chose to defend a blank target
 
Kwani wamefunga ushahidi?
 
Umemkuza sana Erick Kabendera bila sababu yoyote ya msingi , labda kwa taarifa yako ni kwamba CHADEMA INAFAHAMISHWA KILA UJINGA UNAOFANYWA NA YEYOTE KUHUSU KESI YA MBOWE .
Sidhani kama amemkuza, ameshauri.

Amefanya analysis iliyokua backed up na facts.
 
Una akili Sana kijana
 
Uchambuzi ndo unatakiwa uwe namna hii siyo unakuja na mipasho Mingi, Hongera naamin wahusika watahusika Kama inavyopaswa kuhusika Kama wahusika🍎
 
True
 
Unampa umaarufu asiokuwa nao. Eti Michael Jordan of this shit. Labda ni Hasheem Thabeet
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…