Naomba nitolee ufafanuzi kuhusu ile mada ya Chupa yenye maji ya MOTO

AXIOM APEX VERBOSE

JF-Expert Member
Joined
Sep 12, 2022
Posts
13,769
Reaction score
23,676
Najua wengi hawakunielewa kwanini niliamka nikaanza kuuliza au kujiuliza swali fikirishi la kidadisi lenye kuonekana km kwamba ni swali la kitoto.

Lakini ni ukweli ulio wazi lile sio swali la kitoto ni swali ambalo watu wamekaa wakalofanyia uchunguzi wa kina.

Sasa ipo hivi;

Maji ya kwenye ndoo ya lita 20 ni Wananchi na raia wote nje ya Mfumo wa Serikali.

Maji ya MOTO kwenye Chupa ya Plastic ni Serikali na ile Chupa yenyewe ya Plastic yenye maji ya Moto ndani yake ni Mfumo mzima wa Serikali.

Guess what?

Ukiichukua Chupa ya Plastic yenye maji ya MOTO lita 1 au 1½ na kuizamisha kwenye ndoo yenye maji ya baridi lita 20, chupa itaenda chini kabisa kabla ya kuibuka na kukaa juu ya maji kwa muda.

Na baada ya muda kupita Chupa yenye maji ya moto, joto la maji ndani ya Chupa ya Plastic na maji ya ndoo ya lita 20 litakua sawa sawia ndio hapo utakapoona Chupa yako inazama ndani ya maji na haitoweza kuibuka tena juu, labda wewe uingize mkono kuichukua.

Swali fikirishi;

1. Chupa ya maji ya moto kua juu ya maji ya ndoo ya lita 20 inamaana gani?

2. Chupa yenye maji yaliyopoa kua chini ya maji ya ndoo ya lita 20 yaan imezama inamaana gani?

Hii inamaanisha nini?

Tafakari.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…