Kuna vijana wengi mitaani wanasubiri ajira lakini hakuna ajira ,ili waendelee kusubiri lazma tutafute utaratibu wa kuwakopesha kwa degree ya pili hii itaondoa vijana tegemezi kwenye familia zetu,maama hawana KAZI ya kufanya wanakula ugari tu
Mkuu Makwa,
makwagejo , nakuunga mkono hoja yako ya vijana wote degree holders walio mtaani, wakopeshwe kurudi shule, ila sio kwenda kusoma masters, bali waende kusoma VETA au elimu ya biashara, kusomea kitu chochote cha elimu ya kujitegemea, wakimaliza wakopeshwe mitaji, waanze kujitegemea.
Wakirudi tuu darasani kufanya masters ya walichosomea, kama kwa first degree walichosoma hakina demand kwenye job market, hata wakirudi darasani kufanya masters, itakuwa ni wastage of time and resources, baada ya miaka miwili ya masters, watarudi tena mitaani na kuwa na jobless wenye masters!.
Solution ni kwenda kusoma VETA au elimu yoyote ya kujitegemea, iwe ni elimu biashara, kilimo biashara, uvuvi biashara, wakimaliza wanapewa mikopo na kuanza kujitegemea na kuanzia sasa wanafunzi wasiendelee kusoma chochote tuu ali mradi kafika chuo kikuu, waangalie trends za demands za job market zinataka nini.
Ushauri huu wa Waziri Mkuu Mstaafu Majaliwa Kassim Majaliwa, ni ushauri kuntu na muafaka sana,
https://www.jamiiforums.com/threads...kukuza-ujuzi-wa-vijana-wa-kitanzania.2319397/
Wanabodi,
Hii ni makala yangu katika gazeti la Nipashe la leo.
Paskali
na
https://www.jamiiforums.com/threads...veta-japo-chungu-ndio-ukweli-wenyewe.2320751/
na
https://www.jamiiforums.com/threads...u-homa-veta-ndio-tiba-ya-joblessness.2319563/
Wanabodi,
Ule mjadala wa wasomi wa Chuo Kikuu, kusoma VETA, unaendelea,
Mshuhudie Mwanamke wa Shoka, Baada ya Kuhitimu Chuo Kikuu, Alikosa Ajira, Akajiongeza kwa Kusoma VETA, Sii Mwingine ni Paulina Chuma, Fundi Chuma!
View: https://youtu.be/hrFHfkk06Wk
Utafiti wangu mdogo, umebaini, hawa wasomi waliokwenda kusoma VETA, ndio wanaofanya vizuri zaidi sokoni, kuliko wasomi plain wa chuo kikuu au mafundi plain wa VETA, kwasababu hawa wana kitu cha ziada!, wanafanya ufundi kisomi zaidi, na wamefanikiwa zaidi kuliko VETA plain!.
Hii maana yake, umuhimu wa wananchi wengi kusoma kiwango cha...
Mzee Pasco