Prakatatumba abaabaabaa
JF-Expert Member
- Aug 2, 2022
- 1,842
- 6,087
Hakuna Mwalimu yoyote yule ambae anakikubali hicho chama Cha CWT kwa miaka mingi sana wameendelea kutafuna ada ya 2% kwa Kila Mwanachama ambao ni wengi mnoo, kipindi Cha Magufuli alisema inakadiriwa kwamba wanakusanya zaidi ya Tsh billion 3 kwa mwezi huku impact ya moja kwa moja kwa walimu hao wanaokatwa hiyo ada ikiwa haionekani.
Wanajineemesha kwa ada ya 2% ndio maana wanateuliwa kwenye teuzi mbalimbali wanakataa kwenda kwa sababu huku kwenye CWT Kuna fungu kubwa wanaloiba kuliko huko kwenye ukuu wa Wilaya.
Nimemsikia Rais wa CWT akisema serikali isiwaingilie kwenye mambo Yao ya wizi wawaache waendelee kuwaibia walimu na kujineemesha, naomba serikali itoe tamko Kali sana kwa CWT na Ikiwezekana wangepigwa virungu vibaya mno wakarudi mashuleni kwao kufundisha, yaani wameacha kufundisha ety wameenda dodoma kujadili jinsi ya kuiba na kupeana posho mngewapiga virungu vingi Sana.
Baada ya chama kipya kuibuka kinachowaibia walimu 5000 ambayo ni nafuu na watu wengi sana kukimbilia huko Kwa sababu Bora anayekuibia 5000 kuliko anayekuibia 32,000/= viongozi wa CWT wilaya na mkoa wamekua wakipenyeza pesa kwa Afsa utumishi wa halmashauri kuwazuia watumishi kuhamia kwenye chama Kingine, tena hao ma Afsa utumishi wamekua na kiburi sana na kuwajibu kwamba wafanye lolote lile waende popote hawachomolewi CWT, Wamekua wakifanya kazi sio kwa misingi ya sheria na katibu ya jamhuri ya Muungano inayomtaka mfanyakazi yoyote kuchagua sehemu anayopenda.
Naomba serikali itoe tamko Kali sana kwa Hawa afsa utumishi wanaopandisha mabega na kujiona Miungu watu na kujifanyia maamuzi yao wenyewe bila kujali sheria inasema nini? Naomba pia kesi yoyote itakayowafikia juu ya Hawa afsa utumishi kukaidi au kugoma kuwaondoa watu CWT washukiwe na rungu zito saana kwa sababu wanagandamiza katiba na sheria ya jamhuri ya Muungano wa Tanzania na wameshindwa kutafasiri sheria.
Mimi kama prakatatumba Nina Imani kubwa saana na serikali ya Mama Samia, so hao walimu waliojikusanya huko dodoma kwa kigezo Cha Baraza la kutafuna Hela za walimu, watimuliwe kwa virungu warudi mashuleni wakafundishe na kumaliza syllabus.