Naomba suluhisho la kuondoa kitambi

Naomba suluhisho la kuondoa kitambi

Mwendece

Member
Joined
Jun 23, 2021
Posts
35
Reaction score
47
Habari waungwana,

Kama mada inavyoonekana hapo juu naomba mwenye kujua suluhisho la kuondoa kitambi anisaidie, nilijifungua kwa operation mwaka jana 11 na sikufunga tumbo sasa badala ya kuendelea kupungua ndo kwanza tumbo linazidi kukua nakosa raha jamani hasa ukitaka kuvunja kabati nguo zinagoma!

Msaada please
 
1.Punguza kula sukari na wanga.

2. Kunywa maji ya kutosha.

3.Kula matunda, mboga mboga na protein kama Samaki, kuku na nyama.
 
1.Punguza kula sukari na wanga.

2. Kunywa maji ya kutosha.

3.Kula matunda, mboga mboga na protein kama Samaki, kuku na nyama.
Thanks,but kibongo bongo Kula proteni ni ishu sababu ya uchumi unakuta vyakula tajwa visivyo ruhusiwa ndo vipo kwa urahisi
 
KITAMBI KINA AINA YA TIBA YAKE,WEKA PICHA YA KITAMBI CHAKO TUONE
 
Wakati huohuo mimi👇
a5543f54-a04d-42f5-bc36-da6a81691ae2.jpg
 
Jiran yangu
Ana kitambi ukimuona mara ya kwanza unaweza fikiri ni mjamzito.

Alianza mazoez ila hata wiki mbili hakumaliza akaacha [emoji23]

Kuna cku alitembelewa na mdogo wake naye yuko hivo.

Nimefikiri wengine miili ya kurithi.
Hahaha jamani mazoezi nami ndo siwezi,nilivaa mkanda nikaona napata maumivu na kujisikia vibaya sasa wasio nifahamu wananiita mama Kijacho duuuuu
 
Habari waungwana,

Kama mada inavyoonekana hapo juu naomba mwenye kujua suluhisho la kuondoa kitambi anisaidie, nilijifungua kwa operation mwaka jana 11 na sikufunga tumbo sasa badala ya kuendelea kupungua ndo kwanza tumbo linazidi kukua nakosa raha jamani hasa ukitaka kuvunja kabati nguo zinagoma!

Msaada please
Dah pole jamani. Mwanao hajambo?

Nadhani ni vema ukawaona wataalamu. Wanaweza wakawa cha kukusaidia.
 
Hili ndio zoezi rahisi kwako japo na wasi wasi na mshono kuwa makini usije ufumua.

Mwili ni msosi, mtazamo na mazoezi ukiweza kuvi control hivi vitatu utapungua japo kwa mbinde sana sio rahis
IMG_20210728_135547.jpg
 
Thanks,but kibongo bongo Kula proteni ni ishu sababu ya uchumi unakuta vyakula tajwa visivyo ruhusiwa ndo vipo kwa urahisi
Protein mbona rahisi sana bongo, kuna maharagwe, samaki, dagaa, soya n.k mimi nadhani protein na wanga ndio vitu rahis zaidi bongo na ndio tunavitumia zaid
 
Hahaha jamani mazoezi nami ndo siwezi,nilivaa mkanda nikaona napata maumivu na kujisikia vibaya sasa wasio nifahamu wananiita mama Kijacho duuuuu
Hakuna njia ya mkato.
Jitahidi kuuchosha mwili kwa zoez la kutembea chapchap hata 1km mida ya jion. Jitahidi kutenga hata siku mbili kwa juma moja.

Ukizoea utashangaa unafika 2km.
Ila matokeo yake yanakuja taratibu.

Ukiwa serious baada ya miez utaanza kuona mwili mwepesi.kupungua mwili mzima sio kitambi tu.

Kula we kula tu
Narudia tena kula

Ila mazoezi yawe sehem ya maisha yako yote

Kama ni mwajiriwa jitahidi jion pale au weekend.

Ukiwa na muendelezo mzuri
Hatimaye utabadili tabia na kuwa mazoea
 
Back
Top Bottom