Naomba tofauti kati ya Nyota na maarafu(Star/famous)

Naomba tofauti hapa na mifano ili nipate elimu wanajukwaa
Unamaanisha sifa anayopewa mtu kuwa nyota au maarufu?
Kama ni hivyo, mtu akipewa sifa kuwa nyota, anafananishwa na nyota, kuwa anang'ata (avavuma), hasa kwa kipindi au wakati huo, mara nyingi muda mfupi.
Maarufu nao pia ni kutokana na alivyo mhusika, naye akivuma kwa jambo au haiba fulani iwe kwa muda mfupi au mrefu.
 
Naomba tofauti hapa na mifano ili nipate elimu wanajukwaa
Tuiweke hivi | "kuwa nyota" vs "kuwa maarufu"

"kuwa nyota" kwa kawaida huashiria kiwango maalum cha ujuzi au vipaji katika nyanja fulani

wakati

"kuwa maarufu" ni neno pana zaidi ambalo linaweza kutumika kwa mtu yeyote anayejulikana kwa sababu yoyote ile. Mfano Piere Liquid unamfahamu wewe? na alikuwa maarufu si ndio?

1676908564673.png
 
Tuiweke hivi | "kuwa nyota" vs "kuwa maarufu"

"kuwa nyota" kwa kawaida huashiria kiwango maalum cha ujuzi au vipaji katika nyanja fulani

wakati

"kuwa maarufu" ni neno pana zaidi ambalo linaweza kutumika kwa mtu yeyote anayejulikana kwa sababu yoyote ile. Mfano Piere Liquid unamfahamu wewe? alikuwa maarufu si ndio?
Ok. Labda nieleweshe ha​

Je Diamondplatnumz na milladayo nani maarufu au nyota
 
Naomba tofauti hapa na mifano ili nipate elimu wanajukwaa
Nyota hujengeka kutokana na umahiri wa mhusika kwenye shughuli au kazi fulani.

Umaarufu ni haiba ya muhusika kutokana na kuonekana anafaa kuwakilisha ama kuwasilisha taswira inayorejea reja ya umahiri pale juu.

Unaweza kuwa nyota wa mchezo lakini siyo maarufu wa mchezo huo

Haya lipia hela ya twishen
 
Je Diamondplatnumz na milladayo nani maarufu au nyota
Rejea huu mstari 👇👇
"kuwa nyota" kwa kawaida huashiria kiwango maalum cha ujuzi au vipaji katika nyanja fulani
  • Hapo utabaini kuwa Diamond na Millad - wote ni wajuzi kwenye kazi zao wanazofanya. Wana sifa zilizo sawa.
  • Wana sifa zote mbili kutegemea muktadha wa maelezo unayotoa kumuelezea muhusika.
 
Star- kuwa mbobezi kwenye shughuli fulani inayokutambulisha; iwe michezo, mziki, mitindo n.k
Famous- kujulikana kutokana na matukio; liwe zuri au baya, litakufanya ujulikane.
Nb:
Unaweza kuwa 'famous' na usiwe 'star'; ila unaweza kuwa 'star' na ukawa 'famous'​
 
Star ni nomino kwanza pia navyoelewa inatokana na status pamoja na ujuzi(talent) aliyonayo yake mfano Tanzania Diamond ni star.

Famous ni kivumishi ikiwa na maana inasimama badala ya Jina(Nomino) apo naona sifa itakuwa inatokana na alichofanya na anajulikana na wengi mfano Tanzania Pierre alikuwa maarufu kutokana na ulevi wake.
 
Rejea huu mstari 👇👇

  • Hapo utabaini kuwa Diamond na Millad - wote ni wajuzi kwenye kazi zao wanazofanya. Wana sifa zilizo sawa.
  • Wana sifa zote mbili kutegemea muktadha wa maelezo unayotoa kumuelezea muhusika.
Mbona unazunguka
 
Star- kuwa mbobezi kwenye shughuli fulani inayokutambulisha; iwe michezo, mziki, mitindo n.k
Famous- kujulikana kutokana na matukio; liwe zuri au baya, litakufanya ujulikane.
Nb:
Unaweza kuwa 'famous' na usiwe 'star'; ila unaweza kuwa 'star' na ukawa 'famous'​
📌🙏
 
Back
Top Bottom