1.idara (department) mfano idara ya usalama wa taifa
2.kurugenzi mfano kurugenzi ya mawasiliano ikulu
3.mamlaka (authority) mfano mamlaka ya bandari
5.Taasisi mfano taasisi ya elimu ya watu wazima
6.Tume mfano tume ya uchaguzi
7.baraza mfano baraza la michezo
8.wakala mfano wakala wa vipimo
Vigezo vipi vinatumika kutofautisha na mtumizi yake
Utofauti wake uko katika maeneo kadhaa nitafunguka machache;
1. Ukubwa wa majukumu
2. Mipaka ya majukumu
3. Muundo wa Taasisi
4. Idadi ya vitengo
5. Mamlaka ya uteuzi
1. Ukubwa wa majukumu:
Idara huwa ni sehemu ndogo ya Taasisi kubwa. Mara nyingi Idara inakuwa na majukumu maudhui tu na haijihusishi na mambo mengine;
Mfano Idara ya Maji. Idara ya usalama wa Taifa (siku hizi haiitwi Idara) bali ni TISS (mawakala wa ulinzi anuai) . Jina la Idara yawezekana liliasiliwa toka kwenye iliyokuwa (special Branch)
2. Mipaka ya Majukumu
Hii ndio makazini tunapewa wanaiita JOB DESCRIPTION. Hapa utakutana na neno Mamlaka zaidi kwa kuwa na mamlaka katika kutekeleza majukumu yaliyo ainishwa.
Mipaka hii ya kimajukumu inaweza ikatokea hata kwenye Idara (yaani Idara ukawa ina kitengo kidoko chenye mamlaka).
Mfano ndani ya Idara kunakuwa na watu wenye mamlaka juu sehemu Moja tu.
3. Muundo wa Taasisi
Kuna muundo ambao fulani ndio unao amua.
Mfano;
Mkurugenzi anaendesha Taasisi/shirika ambayo ndani yake inakua na Idara na mamlaka huo ukubwa ndio unaosababisha utamkwaji.
Kwenye muundo huo utakuta sheria inatamka kwamba anaueongoza Shirika/Taasisi ataitwa Mkurugenzi au Mkurugenzi Mtendaji.
4. Idadi ya vitengo
Hapa naomba nihamishe goli kidogo
(Utofauti Kati ya University na college)
Chini ya Taasisi hiyo iko complex kiasi Gani, ina idadi ngapi za vitengo na vitengo.
Mfano; BODI ya wakurugenzi inaundwa na Wakurugenzi wanaounda Taasisi/Shirika lakini wakugenzi ni viongozi wa vitengo vyao lakini wanapangiwa majukumu na Mkurugenzi Mkuu/Mtendaji na anapotamkwa kama Mtendaji ina maana naye kuna kitengo mahususi chini yake.
Tofauti na Wakurugenzi wakuu ambao wao huwa watch dog wa Taasisi/Shirika katika ngazi ya maamuzi pekee.
5. Mamlaka ya uteuzi
Taasisi/Shirika yapo ya aina mbili
Mosi lile ambalo anayeliongoza anateuliwa na Rais na
Pili wale wanaopanda vyeo hadi kufikia cheo hicho kutokana na sababu mbalimbali.
Mfano; BODI ya Sukari Mkurugenzi anateuliwa na Rais. Ila BODI YA MIKOPO YA WANAFUNZI WA ELIMU YA JUU Mkurugenzi wake anaomba Kazi na analia Mkurugenzi Mtendaji kwa kuwa kipo kitengo mahususi chini yake.
Ilihali wale wakurugenzi wanaoteuliwa na Rais wao wanakuwa ni ma overall in charge na mara nyingi huisimamia zaidi BODI YA WAKURUGENZI kuliko Taasisi husika.
NIPO TAYARI KUBORESHEWA AU KUKOSOLEWA