Naomba tofauti ya maneno haya yanayotumiwa serikalini

Pia wakala wa M pesa, Aitel money, Tigo pesa na Halopesa!!
 
Council Mfano National Council for Tech Education
Council Mfano Town Council
 
Tume ya uchaguzi bado ipo operational, inaendelea kuratibu mambo kadha wa kadha yanayohusu uchaguzi. Tume hii haijavunjwa wala haijapumzika. Majukumu yanayofanywa na tume hiyo ni pamoja na kuratibu chaguzi ndogo, kufanya marekebisho ya daftari la kudumu la wapiga kura, kugawa maeneo ya uwakilishi (majimbo) n.k n.k


Ukisema kwamba hata tume ya vyuo vikuu inaweza kuvunjwa ikiwa haihitajiki ndio kigezo cha kwamba inafanana na "tume matukio" (tume ya katiba mpya, tume ya makinikia, tume ya mfumo wa vyama vingi, n.k) unakua unakosea sana.

"Tume matukio" zinavunjika mara baada ya suala walilokua wanashughulikia kumalizika. Mara nyingi ni baada ya kukabidhi ripoti kwa aliyeiunda (Rais).

Kuvunjwa kwa tume kama TCU, NEC n.k kunafanana na kuvunjwa kwa Mamlaka, Taasisi, Wakala, idara, halmashauri za miji au majiji.

Kwahiyo uwezekano wa kuvunjwa wa tume kama TCU usiwe ndio kigezo cha kufanana na tume matukio ambazo kimsingi zina_dissolve.

Rais Magufuli alivunja Mamlaka ya Ustawishaji makao makuu Dodoma (CDA), alivunja JIJI la DSM, angeweza kuivunja au kuifuta TBS (Taasisi), NEC (tume), TRA (Mamlaka), REA (wakala), TANESCO (shirika), NECTA (Baraza) n.k
Kusema hiki na kile vinafanana kwa sababu vyote vinaweza kuvunjwa au kuvunjika sio sahihi hata kidogo.
 
Nimesoma ila hamna aliyetoa jibu mujarabu wote mnademka tu
Karibu sana kama una mchango ambao ni majibu sahihi. Vinginevyo nawewe umeamua kujiunga na hao uliotanabaisha kama "wanademka"
 
Tofauti ipo
Kila chombo kinaendeshwa kisheria
Na kinaanzishwa kisheria na sheria hazifanani, pia majukumu ya Kila chombo kulingana na sheria zilizowekwni tofauti

Wote tunakubaliana kwamba kila chombo cha serikali kimeanzishwa kwa mujibu wa sheria.
Utofauti wa sheria hizo hauwezi kuwa ndio utetezi wa tofauti kati ya yaliyotajwa katika swali la mtoa mada hapo juu.

Twende kwa mifano.
Baraza la Sanaa (BASATA)
Limeundwa kwa mujibu wa sheria namba 23 ya mwaka 1983 (na marekebisho ya mwaka 2019).
Sheria hiyo imetamka kwamba kutakua na BARAZA la sanaa, ambalo muundo wake utakua hivi, litakua na majukumu haya na yale.

Kwanini liwe ni BARAZA la sanaa na isiwe TUME ya sanaa, BODI ya sanaa, MAMLAKA ya sanaa, TAASISI ya sanaa, WAKALA wa sanaa, IDARA ya sanaa, n.k

Jibu la swali hili haliwezi kuwa ni "kwa sababu sheria imetamka BARAZA" maana sheria ingeweza kutamka MAMLAKA, BODI, TUME, IDARA n.k

Na hapo ndipo swali la mtoa mada linapokuja, je kuna tofauti gani kati ya mamlaka, wakala, taasisi, idara, tume, bodi, baraza n.k

NB: Kila chombo cha kiserikali (tume, bodi, baraza, mamlaka, n.k) ni lazima kiwepo kisheria (kipewe legal being), hakiwezi kuanza kiholela kama GROUP LA WHATSAPP
 
Mamlaka.. authority.. power... nguvu... mamlaka ya mapato... lazma ulipe kodi..
Safi sana. Hutoi gari bandarini(TPA) mpaka umuone mzee TRA. Vinginevyo litaozea kule. The authority to control certain activity regarding specific issue (large scale) given by the Government (Power)
 
Nimepata kitu ngoja waje wengne chief
 
Safi sana. Hutoi gari bandarini(TPA) mpaka umuone mzee TRA. Vinginevyo litaozea kule. The authority to control certain activity regarding specific issue (large scale) given by the Government (Power)
Endelea
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…