Naomba tumsaidie Joyce Kiria wa wanawake live. Anabomoa msingi wa taifa Bora



Kwa akili zako unafikiri wanawake wanapigwa kwenye ndoa zao hivi hivi tu?????
 
Msituchoshe...

Kungekua hakuna uhitaji,Joyce Kiria na programmes zake..zingekufa naturally....

Yupo kwa sababu kuna uhitaji...

Isingekuwa wake zenu wanahitaji kutoa frustrations zao,then Joyce asingekuwepo

Simple!

Joyce mimi nakuomba ufungue office ya counselling, ..najua perherps huna ujuzi lakini unaweza kuajiri counsellors iwasaidie wanawake kisaikolojia warudi kwenye mstari...pia inawezekana kuanzisha number ya simu ambayo inaweza kutoa msaada anonymously...utashangaa wangapi wanahitaji msaada
 
Kipofu akimuongozakipofu mwenzake wote watadumkia kwenye shimo
 
Uko sawa kabsa mkuu nakuunga mkono ktk point yako ya msingi.....mana hata nimewahi kumwambia juu ya suala la kuhamasisha wanawake kuziacha ndoa zao.....mana ni kuandaa taifa kuwa na kizaz kisicho na malez bora na kamil ya wazaz wote wawil......pia nilimwambia kuptia comments ktk post zake kuwa movements for women haiwez kufanikiwa kwa kuwapga vta wanaume au kuwafanya maadui au kuwatenga kabsa........
 
Yaan wanaume wanyanyasaji tu ndo wanaona anafanya vibaya, wanawake wangapi wameuawa mwaka huu tu kea unyanyasaji??
Kwani hao wanawake hawana akili zao wafikirie?? Ukiona anaondoka jua kachoka manyanyaso sio kea sababu Joyce kasema.
Yeye analeta ujumbe tu tena wa watu, nyie tulieni ujumbe uwaingie mpone kufia Segerea na kunyanyasa watoto
 
Kea Kwa hiyo Bora kukaa tu hata Kama hamna furaha? Au Hadi ufe?
 
Hakuna chakutenganisha mpaka waje wakute kichwa kina ning'inia mlangoni? Hakuna shujaa wa mateso ya ndoa, sizani kama mtu ana akili timamu anapendana na mmewe asikie habari hizo na ndoa yake haina changamoto za hivyo aamua kuvunja ndoa! Angejua huwa haijengi hapo tayari mke yupo kaburini
 
Lazma kila ndoa inachangamoto zake. Hakuna anayepinga harakati thidi ya manyanyaso. No nasema no Ila mawazo yake yamejikita kuvunja ndoa tu haoni utatuzi mwingine?
 
POSTS KARIBU ZOTE HUMU ZA WANAWAKE ZINAONESHA NI JINSI GANI WANAWAKE MNAPATA SHIDA KWENYE MAHUSIANO.

LAKINI PAMOJA NA SHIDA ZOTE ZA KIMAHUSIANO NI KWA NINI HAMUACHI HAYO MAHUSIANO??!!

WENGI MNA MATUMAINI YA KUWA KWENYE NDOA ISIYOKUWA NA MIFARAKANO,NI VIZURI LAKINI NI NADRA SANA AU HAKUNA KABISA.

KUSUBIRI ILI KUPATA MWENZA WAKO UNAYEMTAKA UNAWEZA JIKUTA UNAZEEKA HIVI HIVI.

NA HALI HII TUNAPOELEKEA NDO MBAYA ZAIDI.KWANI HATA VITABU VYA DINI VIMETABIRI HIVYO.

USHAURI WANGU:

TUVUMILIANE KATIKA NDOA,KUNAPOKUWA NA CHANGAMOTO BASI TUTUMIE NJIA NZURI ZA KUTATUA CHANGAMOTO HIZO.
 
Lazma kila ndoa inachangamoto zake. Hakuna anayepinga harakati thidi ya manyanyaso. No nasema no Ila mawazo yake yamejikita kuvunja ndoa tu haoni utatuzi mwingine?
Lakini huleta mifano hai! Hapo tayari mke yupo ahera au kama yule sahizi hana mkono na aliambiwa kabisa aondoke lakini hakuondoka, sahizi hana kiganja, kama mtu atavunja ndoa yake kwasababu kamsikiliza Joyce ujue naye hayupo sawa. Kuna kiongozi mmoja wa dini aliwahi sema siku una ambiwa nitakuua siku moja mama fungasha!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…