Siungi mkono kutoa kibano. Ila hili suala linahitaji kuangaliwa kwa upana wake maana linahusisha na mambo ya kimila vile vile.
Kuna mila wanawake wenyewe wanapenda kibano. Ndoa nyingi za vijijini ambazo wahusika hivi sasa ni vikongwe wenye vitukuu na vilembwe zimeishi kwa mazingira haya haya ya kibano cha hapa na pale. Wangeachana ingekuwaje?
Unless hii changamoto ya kubadili hii tabia inaangaliwa kwa upana wake, hizi jitihada za huyu dada zinaweza zisiwe na tija. Zitasababisha ndoa nyingi kuvunjika bila kubadilisha tabia ya wanaume kutoa kibano.
Ma single mama anaowazungumzia na kupromote yeye ni wale wa mazingira ya mijini, kinondoni huko, nk. Kuwa single mama kijijini kiuchumi na social pressure ni ngumu sana. Ardhi inamilikiwa na mume, ukirudi kwa wazazi unatimuliwa!!. Ni changamoto.