Ingekuwa hivyo hata wewe usingekaa na mumeo hadi leo mana kukosekana ndani ya ndoa ni sehemu ya maisha kama binadamu timilifu.Kwa hiyo mtu kama amekukosea suluhisho ni kumbonda sio?
Ingekuwa hivyo hata wewe usingekaa na mumeo hadi leo mana kukosekana ndani ya ndoa ni sehemu ya maisha kama binadamu timilifu.
Achilia mbali kupondana tu hata ukiona umekalipiwa basi ujue umemkosea mwenzako na ikibidi muda mwingine ndo kipigo kinahusika.
Narudia tena hakuna mwanamume mtimilifu anapiga mkewe bila sababu.
Kuna mahali nimesema hawakosei? Wanawake wanakosea hata wanaume wanakosea pia ..ninyi mkikosea mnafanywa nini? Narudia tena mwanaume mwenye upendo kwa mkewe option ya kupiga huwa ni ya mwisho kabisa, na sina hakika kama vipigo ndio vinarekebisha matatizo ndani ya ndoaIngekuwa hivyo hata wewe usingekaa na mumeo hadi leo mana kukosekana ndani ya ndoa ni sehemu ya maisha kama binadamu timilifu.
Achilia mbali kupondana tu hata ukiona umekalipiwa basi ujue umemkosea mwenzako na ikibidi muda mwingine ndo kipigo kinahusika.
Narudia tena hakuna mwanamume mtimilifu anapiga mkewe bila sababu.
Hahahahah, mwambie bhana....Tuambie wewe njia za kuzuia manyanyaso.....unasema ahubiri upendo wewe hujui kuwa unatakiwa kumpenda mkeo? Mlipokuwa mnafunga ndoa wimbo mkuu kwenye siku hiyo ulikuwa ni upendo mchungaji, waimbaji, wazazi marafiki na wote waliohushuria harusi yako walikuwa wanaimba neno upendo...kama yote yale hayakukuingia ndio yatakuingia leo ukiambiwa na Joyce Kiria?
Sent from my VFD 301 using JamiiForums mobile app
Ukiona mtu anakunyanyasa au kero zimezidi ni bora kuachana nae tuu kuliko kujipa murder case, nigeria kuna mama alipigwa na mume wake,huyo mama akaenda kukodi watu wakamshushia mumewe kipigo ,baada ya wiki Mbili yule baba alizidiwa akapelekwa hosp akafariki kumbe alipata majeraha ya ndani .Tatizo lake yuko biased! Kwani wanaume pia hawanyanyasiki au sababu tumekaa kimya?
Hivyo vipigo ni shauri la kuchoka kuvumilia kero zao.
Nasoma posti zake kupitia wanawake live fb. Anaposti kila uchwao story za wanawake wanasemekana kuteswa katika ndoa zao na kuamua kuachika kabisa. Pamoja na kubainisha malengo yake ni kupigania haki za wanawake, kuwainua kiuchumi nakuwatetea Ila anachofanya Sasa kinaonekana wazi NI kujenga uadui Kati ya wanawake na waume zao.
Najua aliyopitia na huenda hayuko sawa kisaikolojia kuhusu ndoa. Akiwa na ushawishi wake anaenda kubomoa taifa. Mi namshauri Leo Tena humu Jf.
Sawa sikatai pigania haki za akinadada wasinyanyasike. Lakini kwanini mwisho wa siku uhitimishe na kuachana?!! Huwezi pinga ukatili bila kuhimiza kuvunja ndoa za watu? Kila ndoa inachangamoto zake na inasemekana kiutafiti Hadi 40% ya wanaume hunyanyaswa kwenye ndoa zao na wanawake Ila hawasemi, huona aibu.
Unachokifanya ni utume wa shetani. Taifa ovu hutokana na familia mbovu au ukosefu wa familià. Dadaangu omba Mungu akujalie upendo. Himiza upendo katika familia ili kupinga ukatili. Toa mifano ya familia Takatifu zinavyoishi kwa upendo na walivyoweza kuepuka manyanyaso na wanavyotafua changamoto zao. Mungu alimpa Mariam Mama yake Yesu mimba kwa uwezo wa roho mtakatifu. Lkn baada ya hapo akampa Mume wa kumsaidia kulea Mimba na mtoto. Kama mimba iliwezekana patikana bila Mume lkn Malezi bora bila familia Mungu hakuruhusu itokee kabisa. Yeyote apingae ndoa NI nabii wa shetani.
Tuko pamoja kupinga ukatili wa wanawake kwa njia Yoyote Ile lakini sio kuhimiza kuvunja ndoa za watu.
Vibao tena jamani?I'm very good at it ila ikifikia stage nimechoka kuongea kwa mdomo ndipo vibao vitaanza.
😂😂😂😂😂😂😂 madam umeniongezea siku za kuishi! Ati wanaume tufanyeje?Wanaume mwambieni hata uchebe aanzishe wanaume live
Unataka waachike watoto walelewe na nani?Kwa hiyo unataka awaambie wavumilie manyanyaso ili kifo kiwakute wakiwa ndani ya ndoa?
Sent from my VFD 301 using JamiiForums mobile app
Wanaume muanzishe wanaume live[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] madam umeniongezea siku za kuishi! Ati wanaume tufanyeje?
Everyday is Saturday................................😎
Sasa utaninyimaje wakati hela ipo, sasa unataka nikatoe wapi![emoji23][emoji23]We shida yako ni kuchepuka tu, kunyimwa hela sio tatizo?[emoji23][emoji23][emoji23]
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] ila usimng'oe Meno wala kumharibu sura yake!Over my deadbody! Tutayamaliza mjengoni tu iwe kwa siasa au makofi ila sipeleki tatizo langu na wife kwenye media.
Mimi nimesema nataka waachike?
Hapo aliona fulsa na siyo kutatua tatizo.Tatizo Mamlaka zinazo toa na kuratibu huduma za familia hapa nchini zimelala. Kutoa Ushauri masuala ya Familia Ni Professional, tena nyeti, sio kila mTu anaweza akaamka tu kesho akaanza kufundishaa masuala ya Jamii. Ni Upotoshsji Mkubwa ,Ilitakiwa Vipindi vinavyohusu masuala ya Familia yawe yanaririwa na Waendeshaji wake wawe na Taaluma hiyo!
@KAMISHNAwa Ustawi wa Jamii!🥺
Kama msisitizo wake ni kutenganisha watu basi kaishashindwa vibaya mno....Watu wanazidi kufunga ndoa kila kuchwao..na hizo ndoa hazivinjiki kiivyo....Embu hata wewe kwenye jamii inayokuzunguka angalia idadi ya watu wenye ndoa na wanaendelea kupambana na ndoa zao kwa gharama yoyote..na wale ambao wamekimbia ndoa....Msituchoshe...
Kungekua hakuna uhitaji,Joyce Kiria na programmes zake..zingekufa naturally....
Yupo kwa sababu kuna uhitaji...
Isingekuwa wake zenu wanahitaji kutoa frustrations zao,then Joyce asingekuwepo
Simple!
Joyce mimi nakuomba ufungue office ya counselling, ..najua perherps huna ujuzi lakini unaweza kuajiri counsellors iwasaidie wanawake kisaikolojia warudi kwenye mstari...pia inawezekana kuanzisha number ya simu ambayo inaweza kutoa msaada anonymously...utashangaa wangapi wanahitaji msaada