Naomba tumsaidie mwalimu huyu wa serikali, ana taka kuacha kazi kwa hiari baada ya kutumikia miaka 20. Maafisa utumishi karibuni

Naomba tumsaidie mwalimu huyu wa serikali, ana taka kuacha kazi kwa hiari baada ya kutumikia miaka 20. Maafisa utumishi karibuni

TRAT

Member
Joined
Nov 29, 2022
Posts
73
Reaction score
160
Anahitaji kuelewa haki zake kama ataacha kazi kwa hiari, anasitahili malipo gani? Mfuko wa NHIF amechangia miaka 20 kama wataendelea kumuhudumia kama wanavyofanya kwa wastaafu na mikopo yake katika mabenki inakuwaje.

Nakaribisha wanaojua taratibu. Wakutishiana asiache kazi na majibu yasiyo na tija tukae pembeni kwanza.
 
Kiutaratibu ili uhudumiwe Kama mstaafu,inatakiwa uwe umechangia kwenye mifuko ya kijamii,miaka isiyopungua 15.
Atahudumiwa tu.Nimejibu kutokana na uzoefu,mengine watajibu wengine.
 
Huyo anachezea miaka hamsini plus...aandike barua ya kuacha kazi Kwa hiari na atapata stahiki zake zote kama aliyestaafu Kwa lazima
Mie nilidhani Ili kupata stahiki chake kama wastaafu wa lazima ni sharti awe amehudumu zaidi ya miaka 15 na awe amefikisha umri miaka 55. Sijajua huyu aliyefikisha zaidi ya miaka 15 lakini hajafikisha umri wa miaka 55. Asante kwa ufafanuzi. Bado nakaribisha wengine kuliweka vizuri zaidi hili. Hata rejeo na kanuni za kiutumishi.
 
Mikopo ya benki ina bima. Unakatwa bima kwenye hela yako unayokopa. Hivyo bima italipa.

Mengine maelekezo huko juu
 
Hii serikali ingetoa kama option wengi wangetoka leo
 
Back
Top Bottom