Naomba tuongee UHALISIA kuhusu biashara ya Real Estate kutumia mfano HAI

Naomba tuongee UHALISIA kuhusu biashara ya Real Estate kutumia mfano HAI

Sipendi kununua HISA au Kuweka Fixed account lakini Kwa hili la kwako naona Bora ungefanya hivyo.

CRDB wana program ya fixed account inaitwa Mzigo Flex wanatoa 9% of your investment. Ukiangalia hiyo 70,000,000 ungeweka ungepata 6,300,000 kwa mwaka ambayo kwa mwezi ni 525,000 kiasi ambacho ni kikubwa kidogo kuzidi unachopata kwa sasa. Bado utakuwa na faida ya kutokuwa na usumbufu wa wapangaji Wala hakuna delay yoyote.

Ingekuwa unapata faida hiyo kwa kufanya biashara ingine yenye kuhitaji ubunifu ningesema sawa utapanuka mawazo mbeleni itasaidia lakini Kwa kujenga nyumba hakuna kupanuka mawazo.

Labda sasa nishauri uchukue mkopo bank kwa kutumia hiyo nyumba Kisha ufanyike biashara zingine ili pesa ya Kodi ndiyo ibaki kuwa rejesho la mkopo.

Best wishes

Sent from my TECNO P704a using JamiiForums mobile app
Thanks mkuu.
 
Real Estate inaweza kuwa;

1. Kuwa na shamba, ukakodisha watu walime. Au ulime mwenyewe.

2. Kununua nyumba mbovu, unaimodify then unaiuza kwa bei ya juu.

3. Kununua nyumba, unajenga nyumba unai-list kwenye airbnb

4. Kununua kiwanja unajenga nyumba unakodisha kwa wapangaji.

5. Kununua viwanja, unapima then unauza.

6. Una kiwanja, wekezaji anakuja kujenga juu yake anakuwa anakupa commission ya mapato yake.

7. Una kiwanja, unajenga hoteli/ lodge/ guest house.

N.k
Mkuu Bavaria wewe ndio umetoa uchanganuzi mzuri katika huu uzi tena kwa ufupi zaidi[emoji119][emoji119][emoji120]!
 
Huwa biashara ya real estate watu wanazani ni kuuza Viwanja na Kupangisha nyumba lakini sio hivyo tu.
Real estate imegawanyika katika sehem mbalimbali kama vile Valuation, Property Management, Investment and finance analysis na Agency services.
Agency services ndio inahusisha kuuza na kupangisha Viwanja,nyumba,vyumba na apartments, hii unaweza ukafanya tuu ikaanzia locally au ukasajili kampuni kabisa.
Valuation ni uthamini hii ili ufanye lazima uwe umesomea na degree yake inatolewa pale Ardhi University inaitwa Bsc Land Management and Valuation nanusajiliwe na body ya wathamini.
Property Management inahusisha usimamizi wa majengo baada ya kujenga mwenye nyumba anakukabidhi wewe kama manager unakua unatafta wapangaji, unasimamia operation ya jengo nankumiusanyia Kodi anakualipa kiasi flani.Pia inahusisha na facilities management ambazo zipo kwenye jengo.Pia hii unaweza ukafanya lakini itakua vizuri ukiajiri wataalam waliosomea degree ya Property and Facilities Management pale Ardhi University.
Investment and Finance analysis unakua mshauri watu wanataka kununua nyumba Viwanja au kujenga. Kwa mfano mtu anataka ajenge nyumba na arudishe hela yake ndani ya miakakumi ajenge wapi na nyumba ya aina gani na ajengeje.Huwa hii ukifatilia kuhusu real estate unaeza ukafanya au uwatumie wataalam waliosomea Real estate, Investment and Finance pale Ardhi University.
Real estate developers kazi yao ni kujenga na kupangisha au kuuza.
 
Sijui tuwaambie mara ngapi kwamba hii ni biashara kichaa. Unless uwe unaitumia kama security au hizo hela umeziiba ila kama ndio biashara ya kukufanya ufanikiwe my friend hapo umefeli tiyari.

Uliwahi ona mtu kajenga nyumba ikazalisha hela ya kujenga nyumba nyingine ndani ya miaka kumi? Sasa tafuta biashara kama spare parts, electronics, vyakula, retail stores uone nyingine ndani ya miaka mitano inazaa biashara nyingine kama hiyo. Wewe hapo unataka umiliki nyumba nyingi kwa kutumia nyumba hiyohiyo nakuhakikishia utasubiri mpaka miguu iingie tumboni.

Yani bora umiliki bodaboda nyingi nitakuelewa kuliko kumiliki nyumba. Bodaboda inataka kitu kimoja tu, ROHO NGUMU basi. Nyumba ina forces ambazo ni gharama kuzipa control na return yake ndogo.

Yani hata ufanye nini, hutokaa uwe tajiri wa kwanza wa real estate hapa Bongo. Tunao matajiri wa mabasi, madini, mazao, kilimo, usafirishaji, n.k. Tajiri specifically wa biashara za nyumba ni nani hata mmoja tu? Kwanini asiwepo, ni kwa sababu biashara hiyo hailipi wala sio kuwa watu hawaoni fursa
What you think is really becomes your reality,. Kila mmoja na imani yake. Kwenye kila utakachokiamini basi utaletewa njia za kukupeleka huko kwenye hiyo imani yako. Ukiamini kwamba Real Estate investment hailipi uko sawa na atakayeamin Real estate inalipa naye yuko sawa. Kila mmoja atapata mifano ya imani yake
 
Sijui tuwaambie mara ngapi kwamba hii ni biashara kichaa. Unless uwe unaitumia kama security au hizo hela umeziiba ila kama ndio biashara ya kukufanya ufanikiwe my friend hapo umefeli tiyari.

Uliwahi ona mtu kajenga nyumba ikazalisha hela ya kujenga nyumba nyingine ndani ya miaka kumi? Sasa tafuta biashara kama spare parts, electronics, vyakula, retail stores uone nyingine ndani ya miaka mitano inazaa biashara nyingine kama hiyo. Wewe hapo unataka umiliki nyumba nyingi kwa kutumia nyumba hiyohiyo nakuhakikishia utasubiri mpaka miguu iingie tumboni.

Yani bora umiliki bodaboda nyingi nitakuelewa kuliko kumiliki nyumba. Bodaboda inataka kitu kimoja tu, ROHO NGUMU basi. Nyumba ina forces ambazo ni gharama kuzipa control na return yake ndogo.

Yani hata ufanye nini, hutokaa uwe tajiri wa kwanza wa real estate hapa Bongo. Tunao matajiri wa mabasi, madini, mazao, kilimo, usafirishaji, n.k. Tajiri specifically wa biashara za nyumba ni nani hata mmoja tu? Kwanini asiwepo, ni kwa sababu biashara hiyo hailipi wala sio kuwa watu hawaoni fursa
Haya majibu uliyatoaga kwa ujasiri utadhani ni kweli.
 
Back
Top Bottom